
Tanzania imekubaliwa rasmi katika Shirika la World Federation of Hemophilia (WFH). Ni katika kikao cha 30 cha Baraza Kuu kilichofanyika katika ukumbi wa Sheraton Buenos Aires Hotel and Convention Center, nchini Argentina.
Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi 5 yaani Bolivia, Ghana, Surinam na Ethiopia ambazo zimejiunga na shirika hilo na kufanya jumla ya nchi 118. WFH inatambuliwa na World Health Organisation (WHO). Kikao kilitanguliwa na kongamano kubwa kuliko yote ya nyuma lililohudhuriwa na watu 3,300.
Katika kikao cha baraza kuu, Rais wa shirikisho hilo Mr. Mark Skinner wa USA aliikabidhi bendera ya Tanzania kwa Raisi wa Chama cha Haemophilia Society of Tanzania Mr. Thadei Richard baada ya uanachama wake kupendekeza na kuungwa mkono na nchi wanachama.
Ujumbe mkuu ulikuwa ni "Treatment for ALL people with blood clotting disorders au upatikanaji wa Matibabu kwa wote wale ambao damu yao haina uwezo wa kuganda". Makampuni makubwa yanayotengeneza dawa kama vile Baxter, Pfizer na Grifols yalishiriki.
Nguvu kubwa katika mkutano huu inaelekezwa kwenye kuboresha maisha ya wagonjwa, elimu na uenezi, kuzuia maumivu pamoja na ulemavu wa viungo. Pia damu na madawa salama.
Baraza litahitimisha miaka 50 hapo 2012 itakayoadhimishwa 2012 jijini Paris. Pia walipiga kura kuchagua wenyeji wa mkutano wa 2014 ambapo Austalia imeishinda Marekani.
HIvi nchi hii wanaojita marais wako wangapi?? Poa. Hongera Mdau kwa kutuwakilisha ila ukirudi usisalau malengo yalokupeleka huko. Si kulamba suti na mjusi bali kuwakilisha masilahi waliokutuma. Ukirudi tuelimishe zaidi kuhusu hiyo Hemophilia.
ReplyDelete