Warembo washiriki wa Shindano la Miss Open University of Tanzania Excellence 2010,wakiwa wamejipanga kwa ajili ya picha.Shindano hilo linatarajiwa kufanyika kesho katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (Open University of Tanzania) kilichopo Kinondoni Biafra.Warembo wanaoshiriki katika shindano hilo ni Kiran Mohamed,Bahati Abdallah,Christine Justine,Veronica Allan,Salma Ally,Rehema Faraji,Zahara Muhidin,Nancy Muray,Mariana Kavishe,Jacqueline Mwombeki na Glory Mosha.FM Academia wazee wa Pamba ndio watakaopendezesha shindano hilo kwa upande wa burudani.Shindano hilo linakuja kwa udhamini wa Vodacom Tanzania,Times Fm,Clouds Fm na Mount Moriuh Hotel.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2010

    nilifikiri tutapumzika hata mwezi mmoja kutoona mamiss hawana kazi nyingine za maana

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2010

    WADAU WAZIPIGA LAIVU, MWANANYAMALA
    ******************************

    MUJOMBA ISSA MUHIDIN MICHUZI,BWANA MIMI NAKUONYA NA KAMA WEWE NI MUTU WA KUSIKIA USIKIE. USIWEKE ATIKO ZA NABII ZA YOHANA MASHAKA KWENYE HII BULOGU YAKO. KWANI LEO WATU WAMEZICHAPA KIKWELIKWELI PALE MWANANYAMALA KWENYE BAA. WALIKUWA WANAJADILI VIJANA WAKALI SANA NJE NA NDANI YA INCHI. SASA WENGINE WAKAANZA KUBISHA KWAMBA ZITTO NI MKALI KULIKO MASHAKA NA KUNDI LA MASHAKA NALO LIKAWA ALITAKA KUAMBIWA, BASI HAPO NDO NGUMI ZIKAANZA JAMAA WAWILI WAKAPIGANA KWELI KWELI, BILA SISI KUWEPO WANGUMIZANA. KWA HIYO MICHUZI KUANZNIA LEO TUNAOMBA USIWEKE MAKALA YA JOHN MASHAKA KWA MAANA JAMAA NI KONTREVESHO SANA KWENYE HII NCHI AKAE HUKO HUKO MAREKANI ASIRUDI HAPA NA VIZUNGU VINGI VYA KUOKOTA BWANA.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2010

    Kila siku naona kuna mashindano ya visura.Swala langu, hawa ni wa kila siku ni hawa hawa au kila shindano kuna wapya?. Na kama ni wapya kila siku basi TZ tuna utajiri mkubwa sana wa visura.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 24, 2010

    so what kama tuna utajiri wa visura.Hilo linatusaidia kuondoa kero tulizonazo mintarafu ufisadi, foleni kibao n.k sisemi sana lakini kama faida mpaka sasa ni kiduchu tu na hivyo kuzidi kukondesha mabinti zetu kwa vitaji vya siku mbili huku wakashindwa kusoma vema na kuandaa mstakabali wa maisha yao baadae kwa taji za mafanikio kielimu.hayeni wadau wa visura.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...