mbagala ya diamond
TANZANITE


Imezoeleka hapa Tanzania wimbo ukizuiwa kupigwa kwenye vituo vya redio au televisheni kwa sababu umeimbwa kinyume cha maadili ya taifa letu, una lugha chafu au vinginevyo.

Lakini sasa mambo yanaanza kubadilika na umuhimu wa wasanii kusajili kazi zao Chama cha Haki Miliki na Haki Shiriki Tanzania (COSOTA) unaanza kuonekana, kwani wasanii wanakuwa wakali na kazi zao, kiasi kwamba kuzichezea sasa ni ngumu.

Wimbo ‘Kafara’ unajenga mfano wa nyimbo za kuwekewa pingamizi sambamba na kuweka rekodi ya kuwa wimbo wa kwanza kuzuiwa kuchezwa kwenye vituo vya redio na televisheni nchini, kwa sababu umelalamikiwa na msanii Nassib Abdul, maarufu kama Diamond.

Wimbo huo ulioimbwa na kijana anayechipukia kwenye Bongo Fleva, Mwingereza Athumani Mwingereza anayekwenda kwa jina la usanii la Tanzanite, umelalamikiwa na Diamond kwamba umenyofolewa kutoka wimbo wake wa ‘Mbagala’.

Diamond alipeleka mashitaka COSOTA dhidi ya Tanzanite ambaye anajulikana kwa jina la Abuu Fleva, akidai ameibiwa wimbo wake, hivyo kutaka sheria za haki miliki zichukue mkondo wake.
kwa habari zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2010

    Huyo kweli fundi wa copy hata jina ameamua kuchukua kwenye category ya vito kama mwenzie.. kazi kwelikweli

    ReplyDelete
  2. Imetulia sana hiyo!!watu wanaacha kufikirisha vichwa vyao kazi yao kusafiria nyota za wenzao tu!"UNACHABO HADI NUKTA DUH!"
    Lakini huyo dogo naye mwenye wimbo wake naskia anapozi sana cku hiz!!even kwa mashabiki wake waliompa shavu kwa kura zao nyiiingiii zilizomuweka hapo alipo!kama ni tetesi za kweli hizo bac abadilike haraka!!akumbuke "akumbuke kuwa mwema kwa watu angali yupo juu!!maana aweza kukutana tena na hao hao atakaporudi chini alaf itakuwa balaatena!!"vinginevyo kama tetesi hizo zitakuwa c za kweli bac achunge acfikie huko!Na huyo mtoa kopi za watu akaze msuli fani ya muziki si lelemama,acjaribu kuwa kwenye game bali aingie kwenye game!!
    Kutoka Mwisho wa reli.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2010

    kwani lazima kila mtu aimbe? ndo mana wanaboronga wanaishia kufulia si msomee fani za uhakika? hadi mnaboa vinyimbo vingine vibaya hadi tunazima redio mnaongea hamuimbi bure kabisa

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2010

    hahahahahahah nimecheka jamani kaa mwenzake diamond yeye tanzanite oooh no jamani kaaa hana marafiki kumshauri jina hata angejiita Daudi lol hilo anaonekana fika alikwua anagezea. Imbeni na kuwa makini na uimbaji nyimbo nyingi bongo zafananaaaaaa inaboa

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2010

    UKWELI NI KWAMBA HAJAIBA WIMBO NI KUWA BEATS ZINAFANANA, KWA MTAZAMO WANGU HILO SO KOSA KOSA NI KUIBA WIMBO NENO KWA NENO SIYO BEATS TU. DUNIANI KUNA NYIMBO NYNGI TU ZINA BEATS SAWA NA WATU HAWASHITAKIANI, AFTER ALL DIAMOND PIA BEATS SI ZAKE HASA KWA STYLE YA NYIMBO ZA BONGO FLAVA AMBAZO COMPOSER ANATENGENEZA BEATS NA KUMPA MTU ATUNGIE WIMBO. NA HATA HIVYO NI KINYUME HATI MILIKI KUTOLEWA NA COSOTA DUNIANI KOTE NI KAZI YA MAHAKAMA HURU KUSAJILI NA KUTOA HAKI MILIKI. KWA MTAJI HUU HAPA DUNIANI TUSINGEKUWA NA VITU VINAVYOFANANA VIKIZALISHWA NA KAMPUNI TUFAUTI, NITOWE MFANO WA COMPUTER KUNA MAKAMPUNI MENGI YANATENGENEZA COMPUTER KWA MAJINA TOFAUTI WAKITOFAUTIANI VITU AMBAVYO SI BASIC LAKINI FUNCTIONS NI MOJA NA HAWA WOTE HAWAJAOMBA KWA MVUMBUZI WA COMPUTER HAKI YA KUTENGEZA COMPUTER KINACHOFANYIKA NI KUWA HUWA KUNA TOFAUTI KIDOGO AMBAYO MWANZILISHI HAWEZI KUMSHITAKI MWIGIZAJI NA HILI NDILO LILITOKEA KWA WIMBO HUU JAMAA HAKUNAKILI KILA KITU NI BEATS AMBAZO HUWA ZIKO TAYARI KWA COMPOSER HATA BEFORE DIAMOND

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 22, 2010

    hii nyimbo ni nzuri sana amejitahidi na hao wachumba si mchezo.lakini hiyo ndio mbagalaa?doh CCM OYEEE

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 23, 2010

    yani sisi watanzania tunatia aibu kila sekta,kuanzia muziki,nk. mtu kaiga nyimbo hadi jina lake la kisanii limefanana na huyo aliemuiga yani aibu kweli, na producer alikua nani? nae bure kabisa!!bado waiga sauti sasa, kuna mtu anaimba utadhani alikiba,kuna wengine wana nyimbo yao yani kama psquare, hivyo siyo vipaji ni aibu, ndio maana hatuendelei!!!!
    sis anjela

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 23, 2010

    Yaani huyu ata uwezo wakufikiria jina hana. Kweli kilaza utamjua tu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 23, 2010

    FUNGA HIYO MUTU INAYOJIITA TANZANITE HARAKA SANA. HIYO MUTU INATAKA KURETA CHABO MPAKA KWENYE BONGO FREVA. COSOTA FANYA HIYO MUTU RIPA HERA YA FIDIA KWA HIYO BRAZAMENI NYINGINE INAYOJIITA DIAMOND INGAWA SIIKUBARI KWA SABABU IMEREWA UMAARUFU HARAKA KAMA KIROBA

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 23, 2010

    mdau wa Thu Jul 22, 11:07:00 PM unaishi dunia gani? eti watu hawashitakiani! kuna waimbaji tele wamewahi kutaka kuwashitaki waimbaji wengine kwa kucopy beats zao na mara nyingi humalizana nje ya mahakama kwa kulipana.

    Nyimbo unazozisikia ambazo zinafanana beats huwa zimepata baraka ya mtunzi wa beats hizo.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 23, 2010

    Nimesoma maelezo ya huyo Tanzanite,anadai kwamba alikubaliana na Diamond kabla hajaurusha huo wimbo ila jamaa kabadilika baada ya wimbo kutoka.Kama huo ni ukweli basi Diamond amechemka.Huyu mshkaji kiasi flani namuona siyo creative maana kuanzia jina hadi beats na mtiririko wa mashairi ya wimbo amekopi,hata hivyo it's a nice start maana kama nakumbuka vzr hata wakina Ngwair walianza kwa kukopi nyimbo za mamtoni ili wajulikane then ndio wakaanza kuachia madude ya ukweli so kama na jamaa ndio lengo lake then well done.

    ReplyDelete
  12. WADAUMBONA UYO TANZANITE AJACOPY KABISAAAA....
    HIVI AMJASIKIA MJINGA FLAN KATKO KI2 KAMA ICHOOOOOO KNAITWA "TATIZO KWE2 TANDALE"
    EBWANA UYO JAMAA NI ZAID YA KUKOPI MMMMH!!!!!
    N ZID YA MANGWEA ANAVOKOP KAZI ZA MAMTON..
    KITAFTEN ICHO KI2

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 23, 2010

    DAAH!ALICHOBUNI CHA KWAKE NI POZI TU LA HIYO PICHA!!!...ALISAHAU KUWAEKA UA HAPO MBELE ,CHUPA YA SODA NA REDIO YA MKULIMA ILE YENYE SPIKA MBILI!!!!ILA TABASAM NA MENO TUMEYAONA BIG UP KWA KUBUNI POZI LA PICHA!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 23, 2010

    Yaani wenzako wajipinde kufikiria wewe ukopi tu. PUNDAMILIA WEYE.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 24, 2010

    huu wimbo mzuri sans. Ndio photocopy au original?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...