Tatizo la barabara mbovu si la Tanzania pekee bali ni karibu kwa nchi zote zinazoendelea. Hii ni barabara itokayo Naivasha mjini katika mkoa wa bonde la ufa nchini Kenya kuelekea tarafa ya Maiella. Kama dereva asipokuwa muangaliafu au nyakati za usiku kwa dereva mgeni gari linaweza kuingia shimoni na kusababisha maafa. Wakazi wa tarafa hiyo wameiomba serikali ya nchi yao iwasaidie kukarabati barabarakwani kipindi cha mvua imekuwa ngumu kutumika.
Daraja la Gitamayu lililopo katika barabara itokayo Naivasha mjini katika mkoa wa bonde la ufa nchini Kenya kuelekea tarafa ya Maiella lilivunjika tangu mwaka 1997 wakati wa mvua za Elinino na halijaweza kujengwa hadi leo. Wakazi wa tarafa hiyo wameiomba serikali ya nchi yao iwasaidie kujenga daraja hilo kwani wakati wa mvua maji yamekuwa yakijaa na kuzuia magari kushindwa kupita.
(Picha na Anna Nkinda)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2010

    Sasa kwavile tatizo la barabara mbovu ni la nchi zinazoendelea mnahalalisha ubovu wa barabara za Tanzania? Kwani kinachosababisha ubovu wa hizo barabara ni kuwa nchi inayoendelea au ni kukosa Leadership na matumizi mabaya ya fedha za serikali vikichanganywa na Rushwa ambayo inatokana na uongozi mbovu ambao unajihusisha na vitendo vya rushwa au kuviendekeza kwavile na wao wanafaidi kutokana na hivyo vitendo viovu vya Rushwa? Kwahiyo mnapoitoa hiyo picha kwenye hii globu mnataka kutuambia nini? Kuwa tusilalamike au mnataka kutufanya tuzoee ubovu wa barabara au mnataka kumsafisha nani? Hebu acheni u-Kalume Kenge ninyi wabongo...It doesn't matter who else has the same problem....we address our own and on our own terms and conditions...make our leaders accountable of such issues...siyo wanakaa bungeni tu na kudai waongezewe allowances...Mmenipa hasira kweli na huo usemi ati si tatizo la Tanzania tu....so what?
    Mdau-New York City, USA

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2010

    tupeni statistics za barabara mbovu na nzuri(pamoja na ubora)za Kenya na Tanzania. kenya nimefika, hatuwakii hata kwa dawa wako mbali...
    na wako aggressive in all aspects, hawadanganyiki

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2010

    KAZI KUTAKA KUJIENGEZEA MISHAHARA HATA MA MASTAA WAO WASINGEWEZA KUFANYA UPUUZI HUO...HATA NDIO TUNAPOONEKANA KAMA MTU WEUSI AKAILI KANYABOYAAAAA.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2010

    ETI KENYA NIMEFIKA!!!! WAPI NAIROBI? NENDA VIJIJINI UTAONA KENYA ILIVYO, UMEENDA KENYA YA KUELEKEA SOMALIA AU NJE TU YA NAIROBI! PAUL KAMAU UNASEMAJE?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 23, 2010

    Kwa kutumia picha hiyo pekee huwezi kutueleza kwamba barabara za Kenya ndivyo zilivyo kwani habari ni "bias" kwa kuonyesha upande mmoja.

    Kama mdau mmoja alivyosema basi linganisha na barabara za Tanzania kama ndio lengo lako. Kama hiyo ulipiga Kenya vijijini basi nenda Tanzania vijijini pia alafu ulinganishe. Tofauti na hapo unatuletea uzushi tu ambao hauna manufaa kwetu... Kwa upeo wangu mdogo labda Kenya watakuwa mbele au tofauti ya nchi hizi mbili kwa wanaokaa vijijini ni ndogo sana.

    Watu wengi wamekimbilia vijijini na kusahau vijijini au mnasemaje? Hapa sijasikia mdau kutoka kijijini wengi ni watu wa mjini tu... Ukiondoa barabara kuu... barabara nyingi Tanzania ni kazi kweli kweli hasa kipindi cha mvua abiria wanapata taabu. Pili tunaweza kusema kwamba labda mdau wa kutuma hii post ameashiria kuonesha barabara mbovu nchini Kenya bila kujali ubovu wa barabara za Tanzania. Kwa wanakijiji (Kenya na Tanzania) wengi wao wasingeweza kusoma hii post kwa kuwa huduma za internet hazipo vijijini kwao shida ya barabara lipo wazi. Ubovu wa barabara hasa vijijini ni tatizo bado na hilo ndilo la msingi siyo kutuonyesha picha moja nchini Kenya. Kwa hiyo barabara za Tanzania hazipo ambazo ni mbovu zaidi ya hiyo moja uliyotaja nchini Kenya?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 23, 2010

    Kamautanroads@gmail.com



    Nkyabo- Bongo

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 23, 2010

    Ndiyo Kenya nimefika barabara mbovu wanazo sawa lakini there's no way unaweza kucompare Kenya na tz or any other EA country wako mbali ndiyo maana wanatambulika world wide. That's why tukitaka kulinganisha tuangalie statistics no siyo barabara moja tu

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 23, 2010

    Ndiyo Kenya nimefika barabara mbovu wanazo sawa lakini there's no way unaweza kucompare Kenya na tz or any other EA country wako mbali ndiyo maana wanatambulika world wide. That's why tukitaka kulinganisha tuangalie statistics no siyo barabara moja tu..
    ............................................................................

    Hongera mdau kwa kufika Kenya!!! kwa hiyo dunia inaitambua Kenya ka sababu ya barabara zao nzuri...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...