Home
Unlabelled
raha ya shaba uswazi....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
JAMANI NAOMBA KUULIZA ,HIVI HIZO NDIZI HUWA ZINALETWA PAMOJA NA UBWABWA AU WATU WANAKUJA NAZO MIFUKONI.
ReplyDeleteNAKUMBUKA ENZI HIZO USWAZI SINIA LIKITUA TU KILA MTU ANACHUKUA NYAMA YAKE,HALAFU NDIO MNAANZA KULA,KAMA WEWE UNA MKONO MDOGO HUSHIBI,WENYE MIKONO MIKUBWA NDIO HUFAIDI.
Duu! Ankal, hizo picha zinanikumbusha miaka ya themanini wakati nikiwa mdogo kulikuwa na Mzee mmoja maeneo ya Kurasini, Dsm alikuwa hakosi kwenye minuso kama hiyo. Huyo mzee alikuwa balaa, yeye sinia moja la nguna/pilau anakula peke yake. Kwenye shughuli kama hizo watu hawakai naye karibu maana mkono na mdomo wake ulikuwa si wa kawaida. Sinia kama hilo alilobeba ustaadh, huyo Mzee alikuwa anakupigia tonge nne, nguna kwisheni na anaomba round nyingine. Mbaya zaidi, ili kuzuia watu wengine wasile naye, yeye alikuwa akitumbukiza tonge moja mdomoni basi anazamisha mkono wote mdomoni na akiutoa unakuwa umejaa mate na anaukung'utia kwenye sinia lenye chakula. Hapo lazima utamwachia chakula, hazipiti dakika mbili sinia jeupeee!
ReplyDeleteusiandike usivyovijua, NGUNA inatumiaka kwenye ugali tu, wali unaitwa kipunga,mpunga. au cha kufinya
ReplyDeletemswazi orijino mtoto wa kariakoo
"THIS IS IT" REALLY HOME, REALLY PEOPLE,REALLY FUN, REALLY ENJOYABLE, REALLY USWAZI. DAMN.. HOME IS THE DEALLY
ReplyDeletehiyo sio nguna. huo ni wali nguna ni ugali
ReplyDeletekaka michu hio sio nguna, hio inaitwa ubeche..nguna ni ugali na wali uanaitwa mpunga au ubeche kama unavyooneka..Ijumaa El Khareem
ReplyDeletenalia kwetu siku nitaenda nitakula wali wali na ndizi nitaita majirani tugomanie ili nisikie raha ya kula wali ktk sinia moja na watu kibao ila nimeshasahau kula na mikono jamani raha
ReplyDeleteMichuzi ww kweli ni "transitkid" nguna ni ugali sio ubwabwa.Matatizo ya kutaka ku-fill in ndo haya.Kama wewe hujakulia jijini bora uwe muwazi.
ReplyDeletenalia kwetu siku nitaenda nitakula wali wali na ndizi nitaita majirani tugomanie ili nisikie raha ya kula wali ktk sinia moja na watu kibao ila nimeshasahau kula na mikono jamani raha
ReplyDeletenalia kwetu siku nitaenda nitakula wali wali na ndizi nitaita majirani tugomanie ili nisikie raha ya kula wali ktk sinia moja na watu kibao ila nimeshasahau kula na mikono jamani raha
ReplyDeleteUlaji huu wa sahani moja unatakiwa upigwe marufuku maana unashibisha wachache wenye speed, kipenyo kikubwa cha ngumi, na wenye uwezo wa "kubabatiza" nyama na chede(wali). Vile vile ulaji huu unasababisha kuenea kwa "Lokasa Yambongo" (upele unaosababisha muathirika ajikune bila haibu hadharani kana kwamba anapiga gitaa)kutokana na ukweli kwamba unawaji wa walaji wengi ni wa kulowesha kiganja tu. Wizara ya chakula na afya inatakiwa ichukuwe hatua juu ya hili.
ReplyDeletewe ndumba vipi msibani na harusini sio sehemu ya kushibia wee vipi nenda kashibe kwako
ReplyDeleteHa! Ha! Michu wewe mtoto uliyekulia Upanga DSM tangu lini wali wa maji ukawa nguna!, sometimes usiwaachie kikosi kazi cha globu ya jamii photo image za watoto wa mjini, inataki wewe mwenyewe Ankal utie maneno.
ReplyDeleteIla picha ya mwisho imenipa hisia kali kama za dogo huyo, kama kweli sinia litafika kwa watoto hao.
Mdau
Honolulu, Visiwani Pasifiki.
Imenikumbushia arusi moja miaka ya 80 enzi hizo ibada ya harusi ni kutwa watu wametoka ibadani kuelekea kwenye mnuso na kusindikiza maarusi. Kule mnuso ulikuwa tayari wameshapakulia kwenye sinia. Bwana mmoja baada ya kupewa alichukua kiazi na kumeza bila hata kutafuna. Jamaa alikabwa, Hiyo ngummi aliyopigwa alianguka chini. Chakushangaza ni vile alivyoamka tu na kuingia kwenye sinia kuendelea kula bila hata kuangalia nini kilikuwa kimetokea. Nilikuwa mdogo lakini kila nikikumbuka huwa nashangaa kwani hivi yule mtu alikuwa ana njaa ya jinsi gani. KWELI kula kwenye sinia watu wote DUUU kaazi kwelikweli.
ReplyDeleteHahahhahahaaaaa!!!!
ReplyDeleteJamani nyumbani raha kweli!!!
Hahahahahahahahaa!!!!
siku hizi hakuna ulaji huu wa kugombania goli.... nakumbuka long tulikuwa tunamweka nyenyere njia panda atakapoelekea tu.. basi upande huo lazima kutakuwa na kiturubai
ReplyDeleteMimi ni mkristu lakini nikiwa mdogo one of my favourate day ilikuwa siku ya Idd. Love that thing man. Na mkao wangu wakati wakula watu walikuwa wakifiri mimi muislamu. Picha zinanikumbusha mbalisana
ReplyDeleteKUNA KITU KILIKUWA KINAITWA ZIARA NI SHEREHE AMBAYO WAISLAMU ENZI HIZO NIKO MDOGO CHITANDI-NEWALA-MTWARA ILIKUWA INAFANYIKA KILA MWAKA MARA MOJA WATU WANAKUJA TOKA MIJI NA VIJIJI MBALIMBALI KIJIJINI KWETU CHITANDI WANAKESHA USIKU KUCHA WAKIPIGA MADUFU NA KUZIKILI ASUBIHI BASI WALI WA NGUVU, SIJUWI HII INAANYIKA HADI SASA, KULIKUWA HAKUNA UBAGUZI DINI YOYOTE ULIKUWA UNARUHUSIWA KWENYE MKESHA HUO NA ASUBUHI UBECHE KWA SANA KWA STYLE HIYO HIYO INANIKUMBUSHA MBALI SANA HIYO ILIKUWA MIAKA YA 60, 7O, HADI YA 80 NILIPOTOWEKA MAENEO HAYO KUELEKEA HUKO UGHAIBUNI
ReplyDeleteHa ha ha !!!
ReplyDeleteSaafi sana mzee Mithupu kwa taswira hizi hasa ya pili.
Ustaadhi anawahi kupeleka shaba karibu na swahiba wake , na hebu angalia mimacho inayomsindikiza!!!
Hatu ndefu mno hizo ustaadh....
Mswahili kwa kuwahi ubwabwa, pilau au wali hawajambo.Hasa mitaani.
Kuliwahi tokea msiba wa mtoto mtaani, jamaamtu mzima alianza..
"alikuwa rafiki yangu sana marehemu"
Jamaa waliokuwa karibu wakamtonya we subiri shaba tu hapa hamna maneno.
Kaka michuzi hii ilikuwa CULTURE yetu ila cku hizi watu hawaiendelezi hii ni mbaya sana tunaiga wazungu 2uuu..... Inabid tupadilike wadau....
ReplyDeletemichuzi hiyo c nguna..... nguna ni ugali.... hiyo ni kipunga,mpunga, ubwabwa, ubweche na nk Sahihisha hapo......
NGUNA a.k.a KITONGE ni ugali sio wali,wali uswahilini huitwa mpunga,ubeche,kichele n.k. kiukweli hatua za ustadh zinatia shaka,japo hapa tunamwita ustadh lakini hao huitwa "waandazi" kwa hiyo huyo ni "muandazi" si ustadh,hiyo kazi huwa ina watu maalum wanakuwa wanajulikana japo huwa wanajipa tu wenyewe hiyo kazi,lengo linakua wawe wa mwisho kula baada ya wengine kuondoka,sasa hizo hatua ndefu ni muhim sana kuzipiga ili stock kule jikoni ibaki ya kutosha ili muda wao ukifika waupige mpunga kwa nafasi si utakua umebaki mwingi?alaa sasa kumbe..!halafu wanakuwa na ushirikiano mkubwa sana na mpakuaji,hivyo mpakuaji anapiga kitu kimoja kinaitwa mdamdazo(wali haujazwi siniani bali unatandazwa),lazima stock ya mzigo jikoni ibaki mpaka ya kubeba majumbani wiki nzima mzee kazi yako inakua kupasha tu kichele.
ReplyDeleteDu!kitu cha goti..mnanikumbusha mbaaaali enzi hizo kariakoo nyumba za mbavu za mbwa kibao kila mtaa,sasa hivi zimekua maghorofa ya wakinga.kula mpumga shurti upige goti moja,ilikua raha sana.asante sana michuzi kwa taswira hizo
ReplyDelete