Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Zanzibar Mhe. Dk. Amani Abeid Karume katikati, akiwatambulisha wagombea Urais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kushoto na Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilali kwa wananchi wa Zanzibar kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika leo katika uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti mjini Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein wa pili kushoto, Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilali katikati Katibu Mkuu wa CCM Taifa Yussuf Makamba kushoto na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Saleh Ramadhan Feruz, wakisoma Dua Maalum mbele ya kaburi la Muasisi na Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Abeid Amani Karume, walipowasili kwenye jengo la Ofisi kuu ya CCM Kisiwandui mjini Zanzibar leo, kwa ajili ya kutambulishwa rasmi kwa wananchi wa Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2010

    Mimi mbona sielewi? Kuna rais wa zanziba na raisi wa Tanzania? makamu wa zanzibar na makamu wa Tanzania...Na kuna raisi wa muungano pia? nakumbuka zamani ilikua raisi akitoka bara makamu natoka zzenji tu ...Hebu nielewesheni...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...