• Asema mwaka 2010 ubunge unahitaji tafsiri mpya
• Aainisha maeneo nane atayoyafanyia kazi
• Kupiga vita utumiaji wa madawa ya kulevya kwa vijana
• abainisha umuhimu wa ofisi kila kata ndani ya jimbo
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shy-Rose Sadruddin Bhanji ametangaza kujitosa katika nafasi ya ubunge jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam kupitia CCM na lengo lake kubwa ni kuwa kiungo muhimu katika jamii ya wanakinondoni.
Akitangaza azma yake ya kuomba ridhaa kwa wanachama wa CCM katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Shy-Rose alisema kwa mtazamo wake neno ubunge kwa mwaka 2010 linahitaji tafsiri mpya kabisa. `…kwa sasa mbunge anatakiwa kuwa ni kiungo cha jamii badala ya kuwa mwakilishi wa jimbo kama ilivyozoeleka` alifafanua Shy-Rose.
`Mwaka 2010 ni mwaka wa mabadiliko na ndio maana nimeona kwamba ili kila mwananchi kuweza kuwajibika, nafasi ya mbunge inahitaji kutafsiriwa upya ili iendane na wakati na matatizo ambayo yanayotukakabili wananch` alisema.
Kwa maana hiyo amesema kwamba hata sifa za mbunge zinahitaji kutafsiriwa upya kabisa, kwani majukumu yake yamebadilika kuendana na wakati. Ametaja baadhi ya sifa hizo mpya ni kuwa mhamasishaji, kiungo muhimu, kufanya kazi usiku na mchana na kuwa na ofisi katika kila kata ndani ya jimbo husika ili kuwafikia wananchi kwa ukaribu zaidi.
`naomba nitoe tafsiri mpya ya neno ubunge..mbunge anatakiwa sasa awe ni kiungo muhimu kati ya walio na kipato kikubwa, kipato cha kati na wasio na kipato kabisa ili kwa pamoja jimbo liweze kupiga hatua za kimaendeleo. Mimi nitahakikisha kwamba nina ofisi katika kila kata ili niweze kuwafikia wananchi wangu katika kata zote kwani wakati napita kuomba kura ninawafuata na baada ya kufanikiwa kutimiza azma yangu ni wakati wa kuendelea kuwafuata na si wao kunifuata` alisema.
Kada huyo amesema sera yake kubwa itakuwa ni kumshirikisha kila mwananchi wa Kinondoni katika shughuli za kuleta maendeleo ili kila mtu aweze kutoa maoni, mawazo na mchango wa hali na mali katika kuleta maendeleo ya ukweli. Amesema hata mwananchi ambaye atakuwa hana uwezo, atabeba tofali kutoka upande mmoja hadi sehemu husika.
`nimeamua kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya ubunge kwa jimbo la hili ili niweze kuleta mageuzi makubwa sana katika jimbo la Kinondoni…naomba mfahamu kwamba kila mwananchi amebarikiwa akili, vipaji uwezo na Mwenyezi Mungu lakini asiposhirikishwa hataweza kutoa mchango wake, hivyo mimi nitahakikisha kwamba kila mmoja kwa uwezo wake na nafasi yake anachangia katika kuleta maendeleo`, alifafanua.
Shy-Rose alibainisha mambo makubwa ambayo atayapigania kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi ni elimu, afya, ajira kwa vijana, kupiga vita utumiaji wa madawa ya kuleta kwa vijana, kupigania haki za wasanii, kusaidia wajane katika kujikwamua kiuchumi na kuleta msukumo mpya kabisa katika masuala ya mahusiano na jamii ambayo kwa mtazamo wake eneo hili linahitaji msukumo mpya.
Shy-Rose amesema kwamba kutokana na uzoefu wa kazi zake tangu akiwa mwandishi wa habari, mtangazaji na Meneja uhusiano katika sehemu alizofanyia kazi, anaamini amekuwa mwanafunzi mzuri katika kutambua matatizo yanayoikabili nchi nzima na hususan na jimbo la Kinondoni.
`kwa kuzingatia uzoefu wangu ndani ya jamii ya kitanzania na baada ya kufikiria ni jinsi gani nitaweza kutumia akili, elimu yangu, uwezo, busara na vipaji vingi nilivyojaliwa na Mwenyezi Mungu na nafasi yangu katika jamii, hatimaye nikafikia uamuzi wa kujitosa kuomba kuteuliwa kugombea nafasi hii.
`nimejifanyia tathmini ya kutosha, nimejiuliza maswali mengi na kutaka ushauri kutoka kwa viongozi wa chama, familia yangu, marafiki, na wanachama wenzangu. Nimefarijika kwa namna ya pekee walivyonihamasisha kutoka pande zote na ndiyo sababu ya kupata ujasiri wa kujitokeza na kuomba kuteuliwa ili nitimize azma yangu` alisema Shy-Rose.
Shy-Rose amesema ana kila sifa ya kujitosa na kuchaguliwa katika nafasi hiyo kwani yeye amekulia kwenye chama tangu akiwa kwenye Umoja wa Vijana wa CCM sehemu ambayo ni tanuri la kupika vijana kushika nafasi za uongozi na hatimaye kuiingia kwenye chama na viungo vyake.
`Mkiangalia CV yangu mtaona kwamba nimekulia kwenye chama, sijapitia tu kwenye chama, nimetokea ndani ya UVCCM, nimezunguka na viongozi mbalimbali wa chama na serikali nchi nzima na nimejifunza masuala mengi sana ya kutumikia jamii, na jinsi sera na ilani ya chama changu inavyofanya kazi zake za kila siku katika kutumikia wananchi.`, aliongeza.
Shy-Rose amesema sababu ingine iliyompa ujasiri wa kujitokeza katika nafasi hiyo ni kutokana na kauli mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na viongozi akiwemo Rais Jakaya Kikwete, za kuwataka wanawake kujitokeza katika kuwania nafasi za uongozi ili Tanzania iweze kufikia hatua ya kuwa na wabunge asilimia 50 wakiwa ni wanawake.
` kwa makusudi kabisa nimeamua kujitokeza kujitosa kwenye jimbo nikiamini kwamba ninaweza…iwapo nitashinda nitakuwa ni mfano mzuri kwa vijana wenzangu ambao wanapenda siasa lakini wametawaliwa na uoga wa kuingia hasa kwenye majimbo…kwangu mimi nataka niwe mfano wa kuigwa na kuhamasisha wanawake hasa wanawake vijana kuingia kwenye majimbo. Iwapo nitashinda basi mwaka 2015 vijana wengi zaidi watajitokeza kuingia majimboni tofauti na hivi sasa mwamko wao ni mdogo`. Alisema Shy-Rose ambaye kwa hivi sasa ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Benki ya NMB Tanzania.
`kwa kuzingatia yote haya, nina kila sababu ya kuamini kwamba nina sifa za kutosha za kuteuliwa katika nafasi ya ubunge kwa jimbo la Kinondoni hasa kwa sera ya chama chetu ya kutaka kuwezesha wanawake kuingia katika nafasi za kutoa maamuzi (decision making bodies). Naamini kwamba iwapo chama kitanipitisha na hatimaye kushinda katika uchaguzi mkuu nitaweza pasipo shaka kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo makubwa ya kutatua kero za wananchi katika jimbo hili.

Namuunga mkono Shy-Rose kwa kuwa ni mchapakazi, anapenda watu, she makes things happen, she is result-oriented. Kwa sisi tunayemjua kwa miaka mingi tunajua ana sifa zinazotakikana. God Bless you Shy. Martha M.
ReplyDeleteIt needs an individual determination,courage,wisdom,preparedness and ablity to run for a political office,this young lady seems to meet both,wishing her the best of luck
ReplyDeleteHakuna jipya, ni wale wale tu.
ReplyDeleteHongera sana na jaribu bahati yako dada. Mimi naamini unaweza sana, sasa kazi ni kwa wananchi wa kinondoni. Stay blessed
ReplyDeleteMdau blog ya jamii Helsinki
Frateline Kashaga
TUOMBE APITISHWE NA CHAMA, KWANI HAPO NDO KIZINGITI KIKUBWA AKIPITA HAPO MBELE PIOA ANAWEZA KUPITA, WAKATI UMEFIKA NDANI YA CHAMA KUWE NA CHALLENGE YA KWELI SI KUPITISHA WATU WALE WALE BILA YA KUPINGWA, INATUBIDI TUACHE TABIA YA MAZOWEYA YA KUWA SIASA ZA UBUNGE NI CAREER AND A JOB FOR A LIFE. KAMA UNATAKA KUFANYA SIASA NI CAREER NENDA CHUO KIKUU UKAFUNDISHE SIASA,UBUNGE UWE NI WA MUDA TU WATU WAPOKEZANE ILI KULETA NA KUPATA MAWAZO TOFAUTI YA KUCHANGIA MAENDELEO YETU KWA WOTE, IKIWEZEKANA PIA KUWE NA KIPENGELE KATIKA KATIBA KINACHOMRUHUSU MBUNGE KAMA ATAPITISHWA NA CHAMA CHAKE BASI IWE TWO TERMS KAMA RAIS INAVYOKUWA SASA.
ReplyDeletehivi jamani kijana ni miaka mingapi? ni miaka 18-35 ya enzi za umoja wa vijana au?
ReplyDeletekaza buti mama tunakuombea mafanikio lakini jihadhari na mafisadi papa
ReplyDeletemumbai yote itahamia dodoma.bunge litakuwa kuchekuche nahii karenge margia nahi nahi tom karenge nacho hum
ReplyDeleteSi mmbaguzi ni mwenzetu, shemeji yetu, dada yetu, mama yetu.
ReplyDeleteShe loves her country Tanzania. Tumpe kura zooote za ndiyo halafu baada ya miaka mitano tumuulize je ameyatekeleza aliyoyaahidi?. Kama bado nje kama tutakavyowafanya wale tuliowachagua 2005.
Ama kweli "Kwenye msafara wa mamba, kenge nao wamo." We need more smart people like Janury Makamba na sio hawa wengine.
ReplyDeletehongera imekaa vizuri sana hakuna mtu aliyewahi kutoa hivyo.big up shy
ReplyDeleteShy-Rose ni mchapakazi na juhudi zake zimeonekana, tumeshuhudia akizunguka nchi nzima katika kusaidia jamii..hongera sana dada utashinda tu
ReplyDeleteNani anakula huyu mhindi? Man, I wish I could hang out with her tonight. Nita save hii picha.
ReplyDeleteANONY WA 03;03 PM ACHA MANENO YASIYO NA MPANGO KAMA HUNA LA KUCHANGIA KAA KIMYA HUYU NI MMBONGO MTOTO WA KINONDONI KWA TAARIFA YAKO LEO HII HATA UKIMPELEKA MUMBAI SI AJABU HAWEZI KUISHI,UBAGUZI NI DHAMBI MBAYA KULIKO UZINZI NA UUAJI
ReplyDeleteBest Wishes! And if you win do great and memorable things for Kinondoni as the likes of Derek Bryceson.
ReplyDeleteMIMI KWA CCM NAONA WALEWALE TU.
ReplyDeletemdau Wed Jul 07, 03:03:00 PM wewe mbaguzi wa rangi , moune vile huna hata akili , kwani wahindi wakiingie bungeni ndo itakuwa nini ? tukiwa na wabaguzi kama nyie 10 tu basi hatari mbele yetu..
ReplyDeletewewe hapo masikini maisha yako yote kwa sababu ya ubaguzi wako huo , mbona nchi zingine kuna wabunge waafrica na hizo nchi haziko africa ?
MBAGUZI MKUBWA umeniudhi kweli ...
mdomo wako mchafu kama shimo la choo...
GO GO GO SHYROSE , nakuaminia ....
NIMEPENDA SANA TAFSIRI MPYA ALIYOTOA DADA SHY-2010 NI MWAKA WA MABADILIKO!
ReplyDeleteHongera Dada. Tunakutakia mafanikio mema. Imefika wakati kina mama na kina dada wakachuana on merit na akina baba na akina kaka, kwa kugombea na kuchaguliwa, badala ya kukaa na kusubiria kuteuliwa tu kwa viti maalum.
ReplyDeleteTuna imani kuwa unaweza na utayatekeleza unayopaswa ili kuleta maendeleo katika jamii yetu ya kitanzania. Mafanikio mema.
Beijing Oyeeeeeee. Power to the Ladies.
Hongera Dada. Tunakutakia mafanikio mema. Imefika wakati kina mama na kina dada wakachuana on merit na akina baba na akina kaka, kwa kugombea na kuchaguliwa, badala ya kukaa na kusubiria kuteuliwa tu kwa viti maalum.
ReplyDeleteTuna imani kuwa unaweza na utayatekeleza unayopaswa ili kuleta maendeleo katika jamii yetu ya kitanzania. Mafanikio mema.
Beijing Oyeeeeeee. Power to the Ladies.
hakuna aliezaliwa awe kiongozi uongozi ni wito,jimbo letu la kinondoni ni moja kati ya majimbo muhimu nchini mbunge wetu mmoja tu ndio alieweka rekodi ya kuleta maendeleo na na kila mwanakinondoni alimkubali,huyu si mwingine ni Dereck Bryson mtanzania mwenye asili ya ujerumani,waliofuati karibu wote longolongo wabunge biashara,sasa mama kaza buti tuko nyuma yako tunaitaji mabadiliko na hasa eneo moja limenigusa,adawa ya kulevya naamini kwa kushirikiana na kamanda Karim Bhanji tutafanikiwa kama sio kumaliza tatizo la mateja kinondoni.
ReplyDeletecongratulations shyrose...this is a big step..all the best!
ReplyDeleteNi Mtanzania... hakutoka kwenye familia tajiri -- Mwanza -- she struggles like others to be what she is now... acheni ubaguzi wa Rangi... atakuwa mbunge mzuri... na nikijana naona rushwa itaondoka
ReplyDeleteGo ShyRose --- RR -- Former Lake High School Student in US
good move Shy-Rose i support your decision.
ReplyDeleteUlaji tu hakuna jipya. Mbona haendi kugombea kijijini kwao? Ama hana kwao? Basi tuhoji uraia wake. Kwa sababu anagombea kwa CCM hawezi kuhojiwa angeingia kwa upinzani yangezuka maswali mengi tu.
ReplyDeletehongera dada ila mbona inaelekea ni mtokaji sana maana picha zako zinangaa kila sehemu utapata mda kweli wa kulitumikia taifa
ReplyDeleteif you dont value who you are, people wont value what you do..big up shyrose for setting an example...we are behind you and God bless you
ReplyDeleteHalooooo Mwaka huu MTAJIBEBAAAA !!!
ReplyDeleteshy rose huyoooo anaenda zake dodoma kwa raha zake .... mtabakia kusema na kuosha vinywa vyenu vichafu
nenda bungeni mwaya weee mafisadi wamezidi kamtoe angalau mmoja ushike nafasi yake.....
nimekuwa nikimfuatilia sana Shy-Rose na hakika ni mpiganaji. Ni mchapakazi ni mtu wa kujitolea na hana maringo. Huyu dada ameonyesha mfano kwa wengine ambao wanakimbilia viti maalum. Yeye hakutaka nafasi za upendeleo. Hongera sana Shy kwa uamuzi wako na nina hakika utaibuka mshindi na sifa yako kubwa ni kutokata tamaa..hili ni fundisho kubwa sana ndani ya jamii..TZ tuna mifano michache sana kwa wanawake waliofika mbali so tunahitaji mifano mingi zaidi. Mimi ni mmoja wa wadau wa kinondoni na naahidi kukupigia debe ile mbaya, kizuri zaidi safari hii chama kimeamua kila mwanachama atapiga kura kumchagua mgombea anayemtaka..hapa masuala ya rushwa hayapo kabisa kwani wale wachache waliokuwa wanajifanya ni chama chao mwaka huu wamekomeshwa...endelea kusaidia jamii shyrose kwani mwaka huu ni wako..tunakuombea kila lenye heri na Mungu yuko na wewe...jimbo liko wazi hilo...nikupongeze tena kwa kuchagua jimbo la wajanja. mwisho nimependa sana sera yako ya kusaidia wajane kwani hili kundi limesahaulika ndani ya jamii, wengi wao waume zao wamefariki hasa kwa ugonjwa wa ukimwi lakini leo hawana sehemu ya kukimbilia..hakika umewaza na umekuja na style mpya ya kuthamini jamii. Mdau.
ReplyDeleteshyrose u are our role model..keep going only sky is the limit
ReplyDeleteThe only thing you should knw is dat,he is just standing ryt next to you. Usiogope hata kidogo dada. Victory belongs to you. Ukishinda utaniambia. Utapata na tunajua unaweza.
ReplyDeleteAmesema kuwa ana vipaji vingi alivyojaaliwa na mwenyezi Mungu. Tunaomba avorodheshe hivyo cipaji na wengine tuvijue kabla ya kufanya uamuzi tafadhali.
ReplyDeleteMzozaji
congratulations shyrose. Mda umefika wa kuangalia mtu na c chama anachoingilia. Hata kama angegombea chama kingine mimi ningemkubali ila napata tatizo moja tu CCM ni chama cha kibaguzi wanachagua watu wao tu lakini mwaka huu tutapimpigania kufa na kupona ili tumpitishe.
ReplyDeletehongera kwa kutangaza nia shy
ReplyDeletemtoto wa kike umepigana lol!!! hukati tamaa? wish you all the best. Must admit i admire your spirit. Wish there were more courages women like you. Go girl!
ReplyDeleteShy do not be shy be bold...as people are suffering because of rushwa business. The people have a lot of expectations so do not let us down. How come at Masaki a private water supplier is able to give clean water from Dawasco while DAWASCO themselves stay mum over this issue? Incredible!!!!!!!!!!Wish you Luck Shy.
ReplyDeleteNimesoma comments 35 zilizotangulia. 34 zinaeleweka. Moja inatisha: hiyo ya anon 03:03:oo p.m. inatisha. TZ tujihadhari sana na "makaburu" ma-racist ...wawe weupe, brown au hata weusi wenzetu kama huyo wa 03:03:00 p.m. Shy-rose ni mchanganyiko: nusu mhindi nusu mwafrika menyu (mama yake anatoka kijijini kwetu). Sisi tumemkubali kwa matendo yake. Katika 1990's mimi nilibahatika kufanya utafiti wa vita vya TZ-Uganda ("vita vya kagera"). Nilishangaa kuona katika vita hivyo kulikuwa na maofisa wengi machotara kama vile kina Brigedia Walden, maofisa Katlas, Fritz, Louis, Ghalib Riyami, kina Hans Poppe, Col. kashmir (mdosi) n.k. Wakati wa Mwalimu kulikuwa na mawaziri wazungu, k.m. Bryson, na Dr. L. Stirling na wahindi k.m. Alnoor Kassam na Amir Jamal, mchanganyiko k.m. Julie Manning na Comrade Abdulrahman Babu n.k. Kama alivyosema Mwalimu "[wanasiasa] wabaguzi wamefilisika kifikra na kimaadili, wanatumia chuki za kibaguzi kujihalalisha" [Racist [politicians] are intellectually and politically bankrupt, they are using bigotry to seek legitimacy]. Tumeanza kuona "vichwa vya nyoka" vya kikaburu vimeaanza kuwashambulia machotara, who next: wacgagga, wanyakyusa, wapemba??? Apartheid imefeli South Afrika, imefeli Ujerumani wakati wa Hitler na Uganda wakati wa Aimin, bado baadhi yetu hawajifunzi??? Kila mtu ahukumiwe kwa matendo yake na si kabila au dini yake: that's TZ!!!
ReplyDeleteshyrose utashinda njia ni nyeupe kabisa. kumbuka utakatishwa tamaa sana lakini usihofu Mungu yuko pamoja na wewe. mapenzi yako ndani ya chama ni dhahiri na mapenzi yako kwa nchi hii pia ni dhahiri. God bless you shy nia yako ni njema na utafanikiwa
ReplyDeletenaona ujio mpya wa bryson
ReplyDeleteNi vema atueleze kwanza ameolewa? Umri wake na matendo yake lazima tuvipime wapiga kura ili tupate chaguo sahihi. Ni mtu wa kujirusha hovyo na viguo vifupi ataweza kutunga sheria? Shy tutoe shaka kwanza wapiga kura
ReplyDeleteHamna kitu hapo. Mweleka kwa kwenda mbele kama gari la fire hapo Magomeni. Na hao waliotoa maoni kuwa anaweza hivi wanamaanisha au wanamsanifu? Huyu hata kwenye mchujo wa awali hapiti. Hata angesema agombee udiwani asingepata. Hivi mnamfahamu au mnamsikia huyu? Tuulizeni sisi tunaomjua. Abakie huko huko NMB na publicity zake.
ReplyDeleteMdau uliyefanya utafiti wa Vita Ya Kagera/Wanasiasa wa Tanzania, tuwekee hiyo research paper yako Watanzania tuisome tufaidi historia nzuri isiyo na ubaguzi.
ReplyDeleteMaana nahofu sije ukafa na hiyo Historia (Research paper Vita ya Kagera)nzuri wakafaidi wazungu vyuoni ulaya/Marekani, badilika usiwe kama vile mababu zetu wanavyofanya siri 'utaalamu' wao, wakiaga dunia wanakwenda na siri zao kuhusu 'mahoka','mizizioloji' n.k
Mdau
Kijana
hongera shy kwa kutangaza nia, pigana utashinda
ReplyDeletehatutaki gabacholi kinondoni
ReplyDeleteHongera Shyrose twakutakia kila yalo mema
ReplyDeleteJamani Shyrose ni mtazania ni mzawa wa mwanza mtaa uitwao miti mirefu opp na shule ya pamba