Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa Benki ya Maendeleo Tanzania (TIB) Thomas Samkyi akizungumza Dar es Salaam jana na waandishi wa Habari juu ya huduma zinazotolewa na benki hiyo katika kuwainua wajasiriamali.Anayeangalia ni Ofisa Mahusiano Mwandamizi wa Benki hiyo Catherine Magambo. Ofisa Mahusiano Mwandamizi wa Benki ya Maendeleo Tanzania (TIB) Catherine Magambo akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephrahim Mafuru wakati wa Kongamno la wajasiriamali lililofanyika Dar es Salaam jana.
Ofisa Masoko wa TIB Desideria Mwegelo akifafanua jambo kwa baadhi ya washiriki wa kongamano la Wajasiriamali Tanzania lililofanyika Dar es Salaam jana walipotembelea banda la benki hiyo.TIB walishiriki wakiwa ni miongoni mwa wadhamini wa shughuli hiyo.
TIB yapokea maombi ya mikopo ya bil. 34/-
Na Mwandishi Wetu.
BENKI ya Maendeleo Tanzania (TIB) imepokea michanganuo ya mikopo inayolenga sekta ya kilimo yenye thamani ya sh. bil 34/- ambapo mikopo yenye thamani ya sh. bil 5/- tayari imeidhinishwa.

Akizungumza katika Kongamano la Wajasiriamali lililofanyika Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Mikopo wa TIB, Thomas Samkyi alisema bado wanaendelea kuyafanyia kazi maombi waliyopokea na kuwahamasisha watanzania zaidi kutuma maombi kwa ajili hiyo.

Alisema benki hiyo imejitahidi kutoa matangazo katika vyombo mbalimbali vya habari kuhamasisha watanzania kuchangamkia mikopo hiyo na kwamba tayari benki hiyo ina fedha za kutosha kwa ajili ya mikopo hiyo.
“Tayari tumepokea michanganuo inayohitaji mikopo yenye thamani ya sh. bil 34/- katika kipindi cha mwanzo wa mwaka mpaka sasa na tayari tumeifanyia kazi baadhi yake na kuidhinisha michanganuo yenye thamani ya sh. bil. 5.
“Ingawa tayari tumetoa matangazo mengi kuhusu hili lakini bado tunawahimiza watanzania katika maeneo mbalimbali nchini kuendelea kutuma maombi kwani tuna fedha za kutosha kwa ajili ya Kilimo Kwanza,” alisema.

Alifafanua kuwa maombi wanayopokea yamekuwa yakilenga sehemu tofauti ndani ya sekta ya Kilimo na kwamba vipaumbele vimekuwa vikitolewa kwa wale ambao michanganuoa yao imelenga kuleta tija na faida ndani ya sekta ya kilimo.

Kwa upande wake mgeni rasmi wa Kongamano hilo Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda,Biashara na Masoko Joyce Mapunjo aliwataka wajasiriamali kote nchini kuwa wabunifu katika kutafuta soko kwani hilo ndilo litawasaidia katika kuinua vipato vyao.

Alisema watanzania wengi wanaojiendesha kwa mitaji midogo wamekuwa wavivu kujituma katika kupanua biashara zao hivyo kufilisika mapema na kusisitiza kwamba serikali ipo tayari kusaidia pale wanapoona wamekwama.

“Wizara yangu na serikali kwa ujumla inafarijika kuona wadau mnachukua hatua katika kuhakikisha sekta ya wajasiriamali inapanuka lakini wakati fulani tunajirudisha nyuma wenyewe kutokana na uvivu, nawasihi tubadilike na serikali ipo tayari kuwaunga mkono,” alisema Mapunjo.
Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete imedhamiria kuwekeza nguvu katika kuinua sekta ya Kilimo na kwamba TIB imepewa jukumu la kuwawezesha watanzania kote nchini kwa kutoa mikopo nafuu ya Kilimo ya muda mrefu na mfupi.

Tayari Serikali imetoa sh. bil 100/- kwa TIB kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli hiyo na kwamba benki hiyo inaendelea na mpango wake wa kufungua ofisi katika maeneo mbalimbali nchini ambapo kwa sasa wapo Dar es Salaam, Mwanza na Arusha.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2010

    MHH MAFURU ALIKUWA NA KITU KWELI CHA KUULIZA AMA!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2010

    si bure analake jambo? usolijua usiku wa giza nene bila nyota na mbalamwezi

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2010

    Jamani sie tuna chama cha walima mboga2,tunaomba taratibu haswa mpaka tupate huo mkopo email:mkobole@yahoo.co.uk . Naomba maelekezo ya kina kwani mpaka sasa chama chetu kipo kwenye mchakato wa usajili.Chama hicho kipo Chamazi/Magole -Ilala.naomba taratibu kwa email hiyo hapo juu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...