Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom
Tanzania Ephraim Mafuru akiweza wazi mambo ya kupewa tafu


Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imezindua huduma mpya ya “NIPIGE TAFU” huduma inayomwezesha mteja wa Vodacom wa malipo ya kabla na Vodajaza kuomba muda wa maongezi akiwa ameishiwa na salio na anahitaji kupiga simu ya dharura.

Huduma hii ya kipekee sit u inaweka Vodacom kama kinara wa Mawasiliano Tanzania bali inaonyesha ni jinsi gani kampuni hii inajali wateja wake kwa hali na mali haswa pale wanapokuwa wamekwama.

Kuomba muda wa maongezi,mteja anapaswa kupiga namba *150*05# na Vodacom itamtumia muda wa maongezi kwa kiasi cha shilingi 500,na itakuja kumkata mteja shilingi 550 mara baada ya kuongeza salio lake,Shilingi 50 ni gharama ya huduma kutoka kwa mteja aliyeoomba msaada huo.

Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru alisema kuwa”huduma hii itasaidia sana wananchi na wateja waliojisajili kwani ni mara nyingi sana watu huwa wanakwama kwa namna moja au nyingine na wanahitaji msaada wa haraka”Mafuru aliendelea kusema kuwa tunafuraha sana kuweza kutoa huduma hii muhimu itakayowasaidia wateja wetu pindi wakiwa kwenye matatizo.
Hii inaonyesha ni jinsi gani Vodacom inajali na kuthamini wateja wake”. Huduma hii ikijumwishwa na huduma nyingine za Vodacom ka Habari Ndiyo Hii,Cheka time,Vodajamaa na M pesa na nyinginezo nyingi ndizo zinazofanya Vodacom Tanzania kuwa mtandao wenye gharama nafuu na huduma zilizo bora hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. yaliyoma yamoJuly 09, 2010

    ndio maana sihami voda ng'o!
    hii huduma itanitoa sana nikiwa sina hela kwenye m-pesa halafu ninahitaji kupiga simu ya dharura wakati sina salio kwenye simu.
    ukichanganya hii na ile ya plizi kolu mi. ebwana dah! habari ndo hii.

    naona tunakoelekea vodacom m-pesa wanaweza wakaanzisha krediti fasilite kama visa kadi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...