
Wabunge nchini Kenya wameidhinisha nyongeza ya mishahara yao ambao utawafanya kuwa miongoni mwa wanasiasa wanaolipwa mishahara minono kabisa duniani.
Chini ya sheria mpya, waziri mkuu wa nchi hiyo atalipwa zaidi ya theluthi ya mwenzake wa Uingereza.
Atakuwa na kipato cha karibu zaidi ya asilimia 10 na anacholipwa Rais wa Marekani. Waandishi wanasema suala hilo limeibua hasira miongoni mwa wananchi na waandishi wa habari. Wabunge wamepiga kura ili walipwe
dola za kimarekani 44,000 kwa mwaka.
Lakini marupurupu ya ziada yanaweza kuongeza mshahara ukafikia dola 126,000 baada ya kukatwa kodi, ambalo ni ongezeko la asilimia 18.
Marupurupu hayo ni pamoja na dola 370 kwa kuhudhuria tu kikao cha bunge kwa siku. Wastani wa mapato ya mwaka nchini Kenya ni takriban dola za kimarekani 730, huku wengi wa raia nchini humo wakiwa na kipato cha chini ya dola moja kwa siku.
Iwapo itapitishwa, sheria hiyo itaanza kutekelezwa wakati wa bunge lijalo, linalotarajiwa kuanza miaka miwili ijayo.
Mwandishi wa BBC wa Afrika Mashariki Peter Greste amesema majadiliano ya wabunge hao yalifanyika haraka kuliko ilivyo kawaida.
Mbunge mmoja alielezea nyongeza hiyo kuwa njia mojawapo ya kurudisha heshima katika siasa.
Hata hivyo, wachambuzi wanasema ni siku chache tu zilizopita benki ya dunia ilielezea bunge la Kenya kuwa ni mojawapo ya mabunge yaliyokita kwa vitendo vya ufisadi duniani.
HAYA SASA !!! ANKAL KAMUA, UR COMMENT PLIIIZZ!!
ReplyDeletenaomba wananchi waende kwenye hilo bunge walipige mawe.shame kabisa
ReplyDeletekamau yuko wapi,maana huu ni ufisadi mara milioni ya ule wa world cup,huo mshahara wa kila mbunge kwamwaka pamoja na marupurupu kila mbunge anauweza wa kuwaleta brazil na agerntina wacheze nyayo stadium,kazi kweli kweli
ReplyDeleteWhere the f**k is Mjomba Kamau talking shit about tanzania while his folks f*****g big time. Little advice Mjomba Kamau in Ankal Michuzi blog " U got the right to shut the f**k up... anything u bluff is ur ass in Ankal Michuzi blob court."
ReplyDeleteTanzania tuliuza majumba (na aridhi) ya serikali kwa wenzetu. Tanzania yetu inajenga majumba kwa wafanyakazi wake kwa gharama ya juu kabisa.
ReplyDeleteAmerika tajiri haina mfumo wa namna hii tuliorithi kwa wakoloni Waingereza waliojijengea hayo majumba mengine tuliyouza!
Kampuni ya Wallmart ya Amerika ina mapesa mengi kuliko nchi zote za Afrika Mashariki kwa pamoja! Afrika Mashariki hatuminyi makadirio yetu ya bajeti wakati huu wa hali ngumu kiuchumi.
Tuna eti wafadhili!
Tunaweza kujiongezea mafao, kama wa-Bunge wetu walivyokuwa wamependekeza.
Naona mtindo huo unafatwa na Kenya…ingawa Waziri wa Fedha Kenyata kasema serikali haina pesa!
Soma hadithi hii fupi jinsi wa California wanavyofanya leo hii:
Court sides with Schwarzenegger on minimum wage
By CATHY BUSSEWITZ and JUDY LIN, Associated Press Writers Cathy Bussewitz And Judy Lin, Associated Press Writers
SACRAMENTO, Calif. – A state appellate court on Friday sided with the Schwarzenegger administration in its attempt to temporarily impose the federal minimum wage on tens of thousands of state workers.
It was not immediately clear how the ruling would affect Gov. Arnold Schwarzenegger's order a day earlier to pay 200,000 state workers the federal minimum of $7.25 an hour as the state wrestles with a budget crisis...
bora walivyojiongezea mshahara kuliko wangejiongezea majukumu vitambi vingepungua
ReplyDeletewameona aibu kuutaja mshahara wa raisi. hawa wajumbe wa kenya hawaishi kujiongezea mishahara. ujeuri ndio kwao. kuna mjumbe mmoja aliulizwa kwanini mmejiongezea mishahara hivyo akajibu mtu yeyote kama anaona vibaya akafanye campaign ili awe mbunge. kama kuna mbunge analalamika aachie ubunge ili mtu mwingine achukue mahali pake. mishahara ya kenya ndivyo ilivyo. chief justice wao pamoja na allowances analipwa dollar million moja kwa mwaka. prime minister na vice president wakiacha kazi watalipwa 85 percent ya mishahara yao maisha yao yote. wake za president, vice president and prime minister wanapewa offices na wanalipwa mishahara na serikali. tukiungana nao huku kwetu mambo yatakua hivyo hivyo.
ReplyDelete"THE BEAUTYFUL ONES ARE NOT YET BORN".....Ayi Kwei Armah.
ReplyDeleteSadly enough there is not even a slight hope that they will ever be born in our beloved motherland - AFRIKA.
Wote tunafanana;wabinafsi,wachoyo,walafi,tunapenda anasa na ufahari bila kuvifanyia kazi,hatuna huruma,hatuna haya....nk.
Hata na MIMI au WEWE tupo vivyo hivyo.Kama unabisha jipime kwa kila dhamana na mamlaka uliyonayo hata kama ni madogo kiasi gani,vipaumbele vyako ni kutoa haki za wengine au zaidi ni kufikiria njia za kuwapora kwa namna moja au nyingine.
Wadau inaniumiza sana moyoni jinsi tulivyo Waafrika,na mbaya zaidi ni kuwa hatujifunzi na matumaini yanatoweka kila siku.
Ni mimi - Mndengestan
Wakenya walio wengi hawaungi mkono wabunge kujiongezea mshahara... Wakenya wanaopenda nchi yao hawaungi mkono kama mmefuatilia.
ReplyDeleteBro Michuzi,Waziri wa Fedha ameyatupilia mbali mapendekezo hayo ya wabunge!Tazama Nation nakala ya Jumamosi.....
ReplyDeletetunaitaji maombi ya kukombolewa kama afrika...
ReplyDelete1.sisi ndio tunawaweka hapo madarakani pia
2.na wao wanaisahau wakifika hapo!!