Asalaam Aleikhum Wadau,

Kwa furaha, heshima na taadhima naomba kutangaza rasmi libeneke jipya la www.michuzipost.com
ambalo wikiendi ilopita lilipaa hewani katika kile kiitwacho uzinduzi laini (soft launch). Kunradhi kwa kutowataarifu mapema, kwani ilibidi mambo kadhaa yawekwe sawa kwanza kabla ya kuthubutu kutia neno kama nifanyavyo sasa.

Wadau wa Globu ya Jamii naomba baraka zenu pamoja na maoni juu ya libeneke hili ambalo azma ya kulianzisha ni ile ile ya Kuendeleza Libeneke kwa njia ya kisasa zaidi na kwa upana mkubwa. Hivyo nakaribisha maoni, ushauri pamoja na neno lolote lile litalonkisaidia kuboresha libeneke hili.

Kama nilivyotamka awali, bado niko katika uzinduzi laini, kwani kama ujuavyo libeneke kama hili halitaki papara. Linahitaji subira, sikion sikivu la neno toka kwa wadau ambao sapoti yao naithamini kama lulu kwa muda wote huu.

Globu ya Jamii itaendelea kuwepo hewani kama kawaida, na itaenda sambamba na Libeneke hili la www.michuzipost.com pamoja na lile la www.michuzi-matukio.blogspot.com. Hivyo wadau Globu ya Jamii itaendelea kudunda kama kawaida, ikiwa ni chapuo la Libeneke jipya ambalo kama utavyoliona, litakuwa na habari na taarifa motomoto kwa mapana na undani zaidi.

Inshaallah panapo majaaliwa Libeneke hili jipya litazinduliwa rasmi mnamo September 8, mwaka huu - ikiwa ni siku ya kuadhimisha miaka mitano kamili ya kuzaliwa kwa Globu ya Jamii kama link hii inavyojionesha: http://issamichuzi.blogspot.com/2005/09/michuzi-and-ndesanjo.html#comments.

Namshukuru Muumba wa Yote kwa kunipa nguvu na uwezo kufikia hapa nilikofikia. Pia natoa shukrani kwa kila mdau ambaye amekuwa akinipa sapoti ya nguvu kila siku kwa kutembelea Globu ya Jamii. Ni mategemeo yangu kwamba baada ya kwikwi ya kuwa na Libeneke jipya wakati fulani huko nyuma, sasa mambo yanaonekana kuwa mswano na Libeneke litaendelea kama kawa.

Libeneke hili jipya la www.michuzipost.com limewezekana kwa ushauri na msaada pamoja na ushirikiano mkubwa wa Bw. Zubeir Masabo na Bw. Alistair Horsburgh, washirika wangu walio Uingereza ambao kwa pamoja tutaendesha Michuzi Post Ltd. kampuni rasmi itayosimamia uzalishaji wa bidhaa za www.michuzipost.com. Sambamba nasi pia kuna kikosi kazi kikubwa ambacho kitakuwa kinashughulika katika kuendeleza Libeneke hili.


Muhidin Issa Michuzi
Mkurugenzi
Michuzi Post Ltd.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. your blog kaka michuzi is the best in the world...I love it and reminds me a lot of back home...keep up the good work...mdau canada

    ReplyDelete
  2. Ankal, HONGERA sana kwa hatua hii uliyofikia. Tunakuhakikishia sapoti yetu. Mimi ni mmojawapo ya wasomaji wa globu ya jamii na kwa hakika imekuwa mojawapo ya chanzo changu cha udodosi wa masuala ya utamaduni na mitazamo ya WaTz nikipendelea jina la WaBongo.

    Sijui kama unaweza kunisaidia kuhusu dukuduku langu: ninaishi hapa US. Nilikuwa Bongo kati ya Mei na Julai mwaka huu, lakini kila nilipokuwa najaribu kufungua globu ya jamii nilipata shida sana hata kusoma maoni ya posting moja. Nilijiuliza ni Watanzania wepi walio nchini Tanzania wanaosoma globu yako kwa sababu nikisoma maoni mengi huwa naona watu wanachangia kutokea TZ!

    wasalaam,
    mdau

    ReplyDelete
  3. Congratulations my brother. Keep up the enterprising spirit and the image of an excellent role model. All success to you.

    ReplyDelete
  4. HONGERA SANA KAKA! KAZI NJEMA HIYO.
    Maggid

    ReplyDelete
  5. Mkuu nakupongeza kwa uamuzi mzuri wa kuanzisha libeneke jingine. Ila mimi ninachoshauri hiyo Michuzi Post ingeenda mbali zaidi kuwafikia hata wale wadau wasiokuwa na uwezo wa kupata hii teknolojia ya Teknohama. Ili kile ambacho wengine wanafaidi na wao wafaidi. Michuzi Post inaweza kutolewa kama jarida la kila mwezi ama gazeti la kila siku. Ninaamini unaweza. INSHAALAH!

    ReplyDelete
  6. hongera sana kaka michuzi kwa kuanzisha kampuni yako. ndio maendeleo hayo tusiridhike na tulichonacho sikju zote tutamani kusonga mbele.
    Hongera sana.
    Swali la kizushi, hapo juu vp ulikuwa unapata futari na watoto wa madrasa ?? mbona hukutukaribisha na sisi tuonje??

    ReplyDelete
  7. Hongera sana jitahidi tu kuwa neutral kwenye mambo ya SIASA, dini, jinsia, rangi na utaifa. Tunatembelea globu yako sababu tunataka taarifa na maoni BILA KUFICHA NA KUPENDELEA. Endelea na msimamo huu. Ukianza tu kuficha au kupendelea habari za aina fulani watu watakukimbia.

    ReplyDelete
  8. Ndugu yangu nakupa hongera kwa mara nyingine tena. Mwenzetu umeona mbali kwa kujua kwamba kwa miaka inayokuja magazeti ya kuchapisha yatakuwa na wasomi wachache zaidi. Tukikutana tuongee zaidi kuhusu kupanua wigo wa MichuziPost.
    Che

    ReplyDelete
  9. This is ace, its class act
    Nakutakia kila la kheri na nakuombea kila jitihada zako zifanikiwe na dua zako zipokewe
    Ramadhan mubarak
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  10. Huyo ni mpambe wa rais Kikwete ndugu zangu. Hawa ndo wanarudisha maendeleo ya hii nchi nyuma bora wao waende mbele. Lakini nasikia watu wajipanga sasa na hatma yake na safari zake za bwerere nje ya nchi zipo ukingoni.' Hili ni swahiba la Kikwete na CCMMMMMMMM! Najua hutatoa lakini ujumbe utakuwa umekufikia kwani mlengwa ni wewe.

    ReplyDelete
  11. HONGERA SANA BWANA KAKA KWA HATUA ULIYOFIKIA. NAMI PIA NAKUSHAURI ANZISHA JARIDA LA KILA WIKI AU LA MARA3 KWA WIKI. PIA TAFUTA KITUO CHA REDIO AMBACHO, KITAWEZA KUSOMA HABARI ZAKO KILA JIONI.

    ReplyDelete
  12. ANKALI HOYEEEEE LIBENEKE HOYEEEEEE WANA GLOBU JUUUUUUU JUUUUU JUUUUU ZAID BAAADA YA KUSEMA HAYA NAPENDA SANA KUKUPA HONGERA WW KAKA ANKALI MICHUZI NA WANALIBENEKE WOOTE POPOTE DUNIANI KWA HALI NA MALI TUNAKUUNGA MIKONO.....KAZI NZURI ANKALI TUNAOMBA SHEREHE HIZI ZIFANYIKE KOTE DUNIANI

    USHAURI MDOGO TUU KWA LIBENEKE JIPYAAA LA DOT COM
    MIMI BINAFSI NAOMBA WAAWZESHAJI WAPATE BALANCE HAPO MAANA NI PANA SANA WAKIFANYA IVYO ITAKUA POA SANA MANA KUNA KUSCROL APO.....ANKALI BIG UP SANA

    SHAMPAGNE YANGU IKO NJIANI TUTAWASILIANA

    ReplyDelete
  13. mchangiaji wa Wed Aug 18, 04:04:00 AM,nahisi kama swali lako halijajieleza vizuri,ulikua unashindwa kufungua blog, then wanaoangalia ni watu wa wapi, PLZ fafanua if u can.
    mara nyingi naona humu watu wanampiga madongo sana michuzi eti ooh unapendelea chama flani, sijui nini . mi ninavoijua Tz yetu, ukitaka maisha yako yaende vizuri, usiishie jela au kukamatwa na polisi basi unatakiwa usiongee mabaya kuhusu chama flani hivi wenyewe mnakijua sitaki kutaja kwa jina. so nahisi michuzi "anajipenda" jamani asije akaishia kufungiwa blog buree tukaosa habari!!
    mariam USA

    ReplyDelete
  14. Ankal, afadhali waosha vinywa hawajakunanga kama kwenye ileeee issue ya tshirt :-)Hongera sana bwana hii kitu imetulia. Kila la heri

    ReplyDelete
  15. nakutakia baraka tele lakini mimi kwa maoni yangu umeshapata jina kubwa hiyo kazi sijui unafanya wapi huko ungeachia na ufanye hizi blogs ziwe mtaji wako ungefika mbali sana. Hiyo kazi inakusensor sana na kukudrag nyuma. Si ajabu faida ya hiyo kazi ni kutalii tu lakini kama unataka watu wakukumbuke vizuri (your legacy) quit that job and put al your effort and passion in your blogs...Wafanyakazi wengi tu kwanza wengine huwa wana weekly column tu kwenye magazeti na shows muhimu hapa US. Wakishafanya kwenye magazine kama NY post, Time magazines, AMW shows etc etc wakishajulikana kidogo wanaaicha ngazi haraka haraka kabla maji hayajapoa na kuanzisha mablog yao na kuandika vitabu kuhusu kazi zao. Kwanza wewe umefanya kazi jikoni (karibu kabisa na hao washika nchi) Ungesema unaandika kitabu tu kikuhusu topic fulani "nyeti" kingekua pre-ordered hata kabla hujakimaliza. Ungetengeneza hela nyingi na kupata masaa ya kupumzika na kuenjoy na familia yako.

    Kwanza sijui labdla ni kutojiamini tu. sasa hivi ungetakiwa uwe na gazeti lako linalotoka hata mara moja kwa week au two weeks...You know kama hawajakupa uwaziri wa habari mpaka leo chance ni kuwa hawatakupa tena...basi do your things.....Fly high ndugu yangu
    .....

    ReplyDelete
  16. umenichekesha kweli naona color za chadema kwenye blog yako mpya...vipi umeshaanza kusikia upepo wa pwani ni nini? Unaanza kujibanza pembeni wasije wakakusahau?????. ..ttttteheheheheheh Na huko tutakuwa muted?

    mimi chichemi hongera bwana ila hiyo new site inaarchieve manake hii inaniboar kweli siku hizi usipowahi kusoma kitu hapa ukienda kwenye archive hamna kitu kinachotokea zaidi ya hizi hizi post zilizo hapa hapa

    ReplyDelete
  17. Hongera lakinimimi ningekushauri kill this one and keep just that one....

    Maendeleo nikuona mbele na watu watakufuta huko huko...kama na hiyo inapokea comments no need to bother reading comments kwenye blog mbili na siajabu itakua the same persona anaacha comments kwenye ile ilei..Ingekua moja inaongea kwa kidhungu na nyingine kiswahili basi ningekuelewa ukirun mbili at the same time...Au kama zingekua na topic tofauti lakini kam habari ni the same ...Baada ya kuiweka sawa hiyo kill the blog...Watu ndio wanaendelea hivyo wanatoka kwenye haya blog baada ya kupata jina na kufungua sites zao....

    ReplyDelete
  18. Ankal hongera.

    Maoni yangu

    Narketplace/social/classified etc amabazo si news necesarily ziwe moved sehemu nyingine, zischanganywe na politics katika kupanga hizo tabs.

    Weka disclaimer inayosema atiko ni maoni ya waandishi na sio necessarily msimamo wa Michuzi Post manake sisi wengine tutatuma atiko zenye utata na controversy na kushambulia system iliooza inayowafanya waTanzania kuwa masikini wakati nchi ni tajiri.

    Umekosea kusema hii ni Tanzania's most popular blog, hii blog ni certainly most popular in the whole of east Africa kama sio Afrika nzima.

    Kaz nzuri sana na asante for yet another avenue ya kutuhabarisha na kutubududisha.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  19. Michuzi pongezi kwa libeneke jipya. Nilikuwa nafikiri libeneke jipya la dot.com litakuwa na rangi nyekundu but mimeshangaa limezungukwa na rangi ya blue. Blue is the colour! Siku nikija bongo nitakuletea kit mpya ya Joe Cole! Keep it up!

    ReplyDelete
  20. Hongera sana kaka Michuzi. Kila la heri katika libeneke lako jipya.

    Nimesoma maoni ya wadau hapo juu. Mengine kama ya kuanzisha jarida la Michuzi ambalo laweza kutoka japo mara moja tu kwa mwezi ni wazo zuri sana. Jaribu kulifikiria vizuri. Wachangiaji wa makala mbalimbali tupo!

    PAMOJA....

    ReplyDelete
  21. Salamu kwa wote watanzania wenzangu walipo nchini na nje ya nchi. Sasa tunaomba route number ya account uliyotoa ilituwezekumsaidia .Pole sana Andrea na mungu akubariki sana

    ReplyDelete
  22. Kaka Hongera Sana, Sasa Funga moja wapo ubaki na moja tu, tuliendeleze Libeneke.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...