Hassan Yahaya Hussein (pichani) anawania Udiwani kata ya Mzimuni jijini Dar kupitia tiketi ya CHADEMA. Hivi tunavyoongea ameshateuliwa na kuchukua fomu za Tume ya Uchaguzi, amejaza na jana amezirejesha tayari. Anaomba kura yako ewe mkazi wa kata ya Mzimuni ili afanye kile anachotaja kuwa mabadiliko makubwa kwenye kata hiyo yenye wakazi wengi na rasilimali kibao. Hassan ni mwanae mkubwa Sheikh Yahya Hussein, mnajibu na mwanazuoni maarufu nchini na afrika mashariki na kati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. karibu sana kaka Hassan kwenye mapinduzi ya kweli, lakin kabla ya yote baba amisha tabir kama utashinda ama umeingia kichwakichwa tuu, usije ukampa lawama baadae

    ReplyDelete
  2. Ninakuatia kila heri. Umefanya uamuzi wa kijasiri. Tunahitaji watu kama nyie. Nitamtumia sms ndugu yangu mkazi wa kata hiyo kumshawishi akupigie na atafute wenzake wengine. tunakuombea. saa ya ukombozi ni hii!!!

    ReplyDelete
  3. Namtakia afya njema na killa la kheri!! lakini ukija wekewa pingamizi usishangae maana kipenga cha kuanza kampeni bado mpk kesho kutwa inakuwaje umeanza kampeni?Tunasubiri kuona maajabu ya ulivyotabiriwa

    ReplyDelete
  4. Je ukichaguliwa hutaleta ushirikina kwa wananchi wa kata hii? Toa sifa ulizonazo kielimu na uzoefu ulionao katika siasa na ushirikiano na wananchi wenzio ili tukupime kabla ya uchaguzi.

    ReplyDelete
  5. duh forecast toka kwa mzee utendaji kwa mtoto!! lol
    Hongera mwaya ila huo wasifu wa mzee wangeutoa maana kuna watu kibao wana negative attitude toka kwa mzee zisije zikakuharibia bure!! simama wewe kama wewe tu and not b'cause of ur dad behaviour!!

    ReplyDelete
  6. Hassan namfahamu zaidi ya miaka 20 tangu akiwa mtoto mdogo Nairobi. Baadaye baba yake aliporudi Dar miaka ya 1982. Hadi leo amekuwa msaidizi wa baba yake kwa maana ya kushika mikoba. Aliwahi kuwa CUF. Baadaye mwaka 2005 akahamia CHADEMA. Labda nyota zimemuonyesha atapeta. Lakini mm mmm

    ReplyDelete
  7. aakayempinga JK atakufa kwa mujibu wa Yahya Hussein, aakayempinga huyu mheshimiwa je atapona?

    Bongo bwana, badala ya watu kuleta hoja wanaleta viroja!!!

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  8. KINAJIMU JINA(Hassan Yahaya Hussein)LINA "H"TATU HII HERUFI HUTUMIKA KUSHANGAA NA KUSHANGILIA INAONYESHA UTASHINDA KWA KISHINDO, PIA JINA LAKO LINA "A"TANO HII HERUFI HUTUMIKA KATIKA KUWEKA MADARAJA YA JUU KATIKA VIWANGO VYA BIDHAA AU HUDUMA, PIA LINA "Y"MBILI HERUFI HII HUTUMIKA KUEMA "YES" PIA HUKAA NAFASI MOJA NYUMA YA "Z" AMBAYO NI HERUFI YA MWISHO KABISA, HII INAMAANISHA UTAPUNGUZA SANA SHIDA ZA WANANCHI LAKINI HUTOWEZA KUZIMALIZA KABISA, PIA HILI JINA LINA "S"NNE HII HERUFI IMEKAA KAMA NYOKA, ALAMA YA NYOKA NADHANI KILA MTU ANAJUA HUTUMIKA NA WATU GANI. KWA KUMALIZIA NAKUPONGEZA KWA USHINDI ULIOUPATA MPAKA SASA.

    NI MIMI MNAJIMU NINAYE IBUKIA IWAPO UNASHIDA YOYOTE YA KINYOTA USISITE KUWASILIANA NAMI NITA KUSAIDIA TUWASILIANE KUPITIA HAPA KWA MICHUZI.


    michuzi ukiibania hii usije ukashangaa kwikwi zitakazoikumba glob ya jamii baada ya nusu saa

    ReplyDelete
  9. Mimi ni mkazi wa Neighbour Bar, kura yangu utaipata ila changamoto iko mbele yako pamoja na Mbunge atakayeshinda.Tafadhali tuondolee kero zilizopo. Mojawapo ni ile ya Mtaa wa Idrisa kugeuka kituo cha kupakilia mizigo ya mikoani, mtaa mzima wa ng,ambo ya butiama umejaa malori. viongozi wa serikali za mitaa wapo wanaona na wanakaa kimya.UdiwaniTunakupa ila Do something kwa kata yetu.

    ReplyDelete
  10. comment nyingine zimekaa kiramli zaidi du! ha ha haaa

    ReplyDelete
  11. hilo jina la mzimuni ni hatari mie limenisismua, siwezi kuishi huko hata unipige rungu nooo!

    ReplyDelete
  12. weweee yuesiburogaa
    (US Blogger) utuachiye mbgongo yetu wenyewe tumeizoweyaa. Uikale huko hukoo!

    Chiaz Mchiiz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...