Ankal,
Mcheki huyu jamaa kwenye link hapo chini ameisifu sana Tanzania.....ni Mkenya.....ni profesa wa sheria hapa Marekani.......aliwahi kukaa Tanzania kwa miaka mitatu (nafikiri alisomea sheria Mlimani).......amesema ukweli wake na kusema kuwa hakuna Mkenya ila kuna raia wa Kenya LAKINI kuna Watanzania, siyo raia wa Tanzania.
Mdau DC

http://www.nation.co.ke/oped/Opinion/An%20open%20letter%20to%20the%20Kenyan%20nation%20/-/440808/968224/-/item/0/-/v1d88kz/-/index.html

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. nimeisoma vizuri ... iam proud to be TANZANIAN

    amesema kweli, wakenya imewauma

    wataimeza hiyo watake wasitake

    truth hurts

    ReplyDelete
  2. Kwakweli sikubaliani kabisa kua Nyerere ndiye aliyewaunganisha watu, kabla ya Uhuru watanganyika tulikua tukijiona kama watanganyika hivyo hali iliendelea kuwa hivyo hivyo tukitumia zaidi lugha ya kiswahili na ukisemea ukabila bado kuna baadhi ya makabila wachache kati yao hujiona kabila lao ni juu ya makabila mengine na yaana yanaendeleza sera ya kupendelea kabila lao katika secta kama za kuajiri kazi NK.

    ReplyDelete
  3. Kazi iliyoanzishwa na mkoloni(Jerumani/Mwingereza) kutumia kiswahili mashuleni, halafu madhehebu yote ya dini Tanzania(Tanganyika&Zanzibar)kutumia kiswahili, baadaye Mwl.Nyerere akaiendeleza kwa kuipa msukumo wa elimu ya msingi kwa wote kwa Kiswahili, bado inahitajika kutiliwa mkazo ili 'Utaifa' wa Mtanzania usije pigwa vita kwa ukabila, udini au kiingereza kikatu-'brain-washed' tujione kama sio Watanzania ila ni Black people wa UK au Afro-Amerikans.

    Tunaona huko Ufaransa, pamoja na waafrika wahamiaji kuongea Kifaransa lakini hawahesabiki ni Wafaransa au Uingereza kuwawekea kauzibe watu wa commonwealth pamoja ya kuwa tunajitahidi sasa kuongea Kiingereza lakini bado hatuhesabiki kama Waingereza kwa kuwa tunatema Kiingereza kama wao.

    Hivyo kwa kila Mtanzania kwa nafasi yake tusibweteke, bali tuendeleze mazuri yaliyoanzishwa na niliowataja ktk paragraph ya mwanzo kujitambua kuwa sisi ni Watanzania.
    Mdau
    Mtanzania1

    ReplyDelete
  4. MbwegelembwegeleAugust 02, 2010

    Kama hukubali kuwa nyerere aliwaunganisha wabongo .Then tuseme alisaidia kuleta umoja Tanzania.
    Wewe ni mmoja wa wale ambao mnambebesha lawama Nyerere kwa matatizo yaliyopo sasa, lakini hamtaki kutoa credit kwa mazuri yanayoonekana wazi .
    Kama Raisi wa kwanza , ktk wakati ule. Kama angekuwa mtu asiyejali utaifa , angeweza kutupeleka ktk migogoro kama nchi zingine za Africa .

    ReplyDelete
  5. Watanzania tunapenda sana kusifiwa!!!!

    Sijui tuna matatizo gani??

    Mdau,
    Reading, UK.

    ReplyDelete
  6. Yote yaliyofanywa na mkoloni na viongozi wa mwanzo yaliwezekana kwa sbabu ya asili yetu ni wakarimu. tunakaribishana. Hatuna umimi. sio matokeo haya bali sababu.

    Hata hivyo bado kuna ukabila japo wapigwa vita saana.

    Upo udini mkubwa mno lakini kwa watu wachache mno.

    Mi naona udini ni mbaya kuliko ukabila kwani udini unagawa watu katika maundi makubwa machache ambapo vita vyawezekana.

    Kwa ukabila kuwa na vikundi elfu 10 nani atawashindwa makundi 9999 peke yao?

    ReplyDelete
  7. Mimi sijatembelea hii web alioweka mdau lakini natoa mawazo kufuatana na maoni ya ndugu zangu hapo juu.

    Mnajua waTZ ndio tu wakarimu lakini si ukarimu kama ukarimu unavyoeleweka, sisi ukarimu wetu ni wa njaa. Tunamkirimu mtu kama tunategemea atupe chochote au vinginevyo. Ni ukarimu huu huu unatufanya watumwa ndani ya nchi yetu, ni ukarimu huu huu waTZ tunyang'anywa ardhi wanapewa wageni, wenyeji tunaishia kuhangaika na watoto wetu tusipate ukakika wa kesho, ni ukarmu huu huu watu wetu wanauawa na wageni eti wameingiza mifugo kwenye ardhi waliokirimiwa.

    Ni kwa sbb hii hata waTZ tumejifunza ukatili miongoni mwetu. Kama watu wetu hawatuthamini na sisi kuthaminiana kunaisha, kila mtu anamthamini ndugu tu.Matokeo yake, ubaguzi wa: sio kabila langu, sio mdini wangu n.k.

    Kwa sasa Ombi langu , raisi wetu ktk kipindi kinachokuja achague wenzake wa kumsaidia kazi kwa uaminifu angalau asilimia 10. tu inatutosha. Masemaji aliyesema ukabila ktk kuajiri..... hiyo haipo tena, ilikuwa zamani. Sasa hivi ni ndugu wa karibu, rafiki, mtoto wa rafiki nk. sana sana udini upo kidogo kwa madehebu machache mno, napo kama shughuli zitakuwa za kidini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...