Gari ndogo aina ya Toyota Hiace lenye nambari za usajiri T 652 ABV lifanyalo shughuli ya usafirishaji wa abiria (daladala) kati ya Makumbusho na Bunju,likiwa ndani ya mtaro mkubwa uliopo maeneo ya Magomeni Mikumi mara baada ya kugongwa na gari nyingine aina ya Nissan Sivillian lenye nambari za usajiri T 677 BEP na kusababisha kifo cha mtu mmoja anaesadikiwa kuwa ni kondakta wa daladala hili lililopo mtaroni kwa kubanwa na gari hii ndani ya mtaro huo.
Break Down likifanya utaratibu wa kulinyanyua gari hilo ili kuweza kuutoa mwili wa marehemu uliokuwa umebanwa na gari hilo asubuhi maeneo ya Magomeni Mikumi.
Gari iliyosababisha ajali hiyo ikiwa imejikita katika kinguzo cha mbezoni kwa barabara ya Kawawa rodi asubuhi hii.
wakazi wa maeneo ya jirani na wapita njia wakiwa wameuzunguka mwili wa marehemu huyo kwa kuangalia kama wataweza kumtambua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Watu wa daladala tafadhali tujitahidi kupunguza speed zisizokua na msingi!! Haraka ambazo mara nyingi mwisho wake ni huu!! Kila muendesha chombo si watu wa daladala peke yao wajitahidi kufuata sheria za barabarani kwni si kwa ajili ya Trafik wala serikali ni kwa ajili ya maisha yetu wenyewe na usalama wa vyombo vyetu!! Lats Practise "Self Defensive Driving" Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi amina. Kama alikua amefunga huyo ni direct peponi!! kwa mujibu wa hadithi na aya

    ReplyDelete
  2. Jamani si hata tutafute kitu cha kumfunikia, huo ni utu tu. Naona hata watoto wapo wanakwenda kuangalia, jamani jamii yetuuuuuuuuuuuuuu, inakwenda wapi nisaidieni jamani uweeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!.

    ReplyDelete
  3. Kumbe wenyewe kwa wenyewe! lazima kulikuwa na vituko kabla ya Ajali!

    ReplyDelete
  4. Vipanya hizi wangevipiga marufuku, humo ndani ukipata ajali ni kama uko kwenye kibiriti

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...