Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dr. Willbrod Slaa akizungumza leo jioni wakati wa uzinduzi wa kampeni na ilani ya chama chao mbele ya maelfu ya watu waliofika kuushuhudia uzinduzi huo katika viwanja vya jangwani jijini Dar.Slaa alisema kuwa akipewa ridhaa ya kuiongoza nchi hii basi atahakikisha ndani ya siku 100 za kwanza,katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafanyiwa marekebisho makubwa na pia kuhakikisha mfumo wa Elimu hapa nchini unabadilishwa kabisa.
Mgombea Mwenza wa Dr. Willbrod Slaa,Said Mzee akiwahutubia wanachama na wapenzi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliofika katika viwanja vya jangwani leo.
Mwenyeki wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe akikabidhi vitabu vya Ilani ya chama hicho kwa mgombea Urais wa chama hicho,Dr. Willbrod Slaa leo jioni katika viwanja vya Jangwani jijini Dar mara baada ya kuizindua.

kwa picha zaidi za mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Chadema leo
BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. walau leo ankal umeanza kuwa fear baada ya wasomaji wa blog yako kuanza kukupigia kelele kila siku. sasa nitaendelea kusoma habari zako.
    Jaribu kuwa unabalance news. Just do fair play kwa vyama vyote. Tunakujua kwamba wewe ni mwandish wa gazeti la serikali lakini isiwe sababu ya kukiuka maadili ya uandishi wa habari

    ReplyDelete
  2. Tanzania demokrasia inawezekana natutafika tu!

    ReplyDelete
  3. Hongera na kwa kweli nakupongeza kwani unatufanya tulio ughaibuni kuona mambo hapo nyumbani. Ila jaribu kuufanya huu mtandao uwe wa uhakika kwa kutumia kiswahili. Post a comment nadhani ina kiswahili chake na baadhi ya maneno mengine. Kuna yale ambayo huwezi epuka kiingereza ntakuelewa.

    ReplyDelete
  4. ovyo hamna jipya hapo!!CCM oyeeee

    ReplyDelete
  5. nyie CHAga DEvelopment MAnifesto,hebu muungeni mkono lipumba tende ikulu,au kwa sababu mmepewa milioni mia na chichiem ndo mnaharibu kura za upinzani makusudi.

    ReplyDelete
  6. Kwani akiwa mwaandishi wa habari wa serikali ndio anaruhusiwa kutokua fair? kwani serikali ina chama? Ni kutojua kufnay akzi na kwa vile yeye ni CCM ndi maana anaoha hata taaabu kuweka balanced news. Kaona watu wanapungua kufungu blog yalke kwa siku ndio anaamka...

    Asiyesikia la mkuu.....

    ReplyDelete
  7. mbona hujaonesha hadhira uncle? au dr. Slaa alikua anahutubia jukwaa? coome on uncle! ni maoni tu!

    ReplyDelete
  8. Unafanya vema Michuzi kukusanya habari za vyama vyote na kuzianika. Wasomaji wengine tulianza kuwa na wasiwasi kwamba nawe ni mwanachama wa chama cha mafisadi labda.

    ReplyDelete
  9. Siamini macho yangu. Yaani Michuzi umeweka habari ya CHADEMA na CUF? Au mtu kakuwekea kwa bahati mbaya? Maana ukweli ni kwamba ukoo wote wa Michuzi kuanzia wewe, Junior mpaka yule dogo wa mtaa kwa mtaa mnaweka CCM tu kwenye blogs zenu. Ama kweli mwezi mtukufu umeanza.

    ReplyDelete
  10. Mh. Michuzi tunaomba na picha za uzinduzi wa NCCR-MAGEUZI huko Morogoro tafadhali.

    ReplyDelete
  11. HONGERA KWA KUANZA KUTOA MATUKIO YA CHADEMA,CUF nk,
    ILA MBONA HAUONESHI UMATI WA WATU
    WALIVYOFURIKA JANGWANI KTK MKUTANO
    HUO WA CHADEMA ?
    AU UNATAKA KUONESHA KUWA HAPAKUWA NA WATU WENGI ?
    FANYA KAMA UNAVYOTOA UMATI WA CCM,
    USIWE BIASED KIASI HICHO, TENDA HAKI, KUMBUKA MWEZI MTUKUFU HUU !

    ReplyDelete
  12. Wewe Dr Slaa mwenzio JK kajenga wewe umeamua ndani ya siku 100 utabomoa. He! Ama kweli kubomoa ni rahisi kuliko kujenga. Kura yangu sikupi. No.

    Na wewe Tundu Lissu na Marando you are a disgrace to the legal fraternity. Unaamuaje kuwa jaji jukwaani kwa kudai kuwa JK kaiba fedha! Hivi kweli nyinyi mnjaua sheria? Shame on you all !!!

    ReplyDelete
  13. blog hii mmmh!

    ReplyDelete
  14. Jamani the look also matters, I am not a fashionista but the CHADEMA uniform or colors or whatever you call it is just not so attractive in short ugly!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...