Zamaradi Mketema ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Take One cha Clouds Tv akizungumza na wataangazaji wa kipindi cha Sports Bar kinachorushwa Clouds Tv, Shafii Dauda (shoto) na Paul James (kulia) mara baada kumaliza kutambulisha kipindi chake kwa wageni waalikwa,kipindi hicho kitakuwa kikiruka hewani kila siku ya jumanne.
Mtangazaji wa Kipindi cha Take One, ambacho kimezinduliwa usiku wa kuamkia leo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali, Zamaradi Mketema wa pili kushot0 akiwa amepozi na baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa bongo, kutoka kulia ni Maya, Anti Ezekiel, Rose Ndauka na ksuhoto kabisa ni Jackline Wolper, Hafla hiyo ilifanyika ndani ya jengo la Clouds Media Group, Mikocheni jijini Dar.Kipindi hicho kitahusu tasnia ya Filamu na mambo mengine kwa ujumla wake.

Ankal, naona dada zetu wamependeza sana wakiwa na mavazi hayo ya staha, ila nawapa ushauri wa bure kwamba wasiishie kuvaa wakati wa Ramadhani tu, wavae kila siku ili kusitiri maungo yao. Tushachoka kuona man..nyo yao.
ReplyDeleteNi hayo tu.
Mdau
Mwenge
ZAMARADI NOMBA NIKUOE TAFADHARI NINA SABABU ZANGU, NA WALA SINA HILA WA LA SITAKI SHARI ILA KHERI
ReplyDeletekWA MTU ASIE WAJUA ANAWEZA KUFIKIRI NI WAISLAM KWELI! KUMBE HAMNA LOLOTE!!!!1
ReplyDeleteINAMAANA M.MUNGU YUPO SIKUYA RAMADHANI TU? AJUE ANACHOFANYA NI KUJITIA DHAMBI MWANAMKE WA KIISLAMU ANATAKIWA AJISTIRI SIKU ZOTE SIO KWA MSIMU IWEJE SASA AWEZE KUFUNIKA KICHWA MWEZI UKIISHA AANZE KUTEMBEA UCHI KWA MWANAMKE WA KIISLAMU UNATAKI UBAKIZE USO NA VIGANJA VYA MIKONO NA MGUU SEHEMU NYINGINE ZOTE HAZIRUHUSIWI KUONEKANA NA WENGINE ISIPOKUWA MUMEO TU,HATUNA AJA YAKUONA KICHWA CHAKE AENDELEE NA USHUNGI BADO ATAKUWA YULEYULE ZAMARADI TENA ATAPENDEZA ZAIDI AKIJISTIRI KULIKO KUTEMBEA UCHI.
ReplyDeletemungu hayuko ramadhani tu , inashangaza sana sasa watu ushungi na ibada , baada ya ramadhan hamna kitu , sisi waislam kesho kuna kazi kwa mungu , yaani usikute hata sasa kiwanda cha bia kinapata hasara mwezi huu yaani bia hazitoki , wanunuzi wakubwa ni sie waislam , halafu mcheki na jaydee yuko likizo dubai,china ,newyork yaani kachagua mwezi wa ramadhan ndo aende likizo maanake wateja wake wakubwa ni waislam na hawatahudhuria shoo zake , umeona hapo mtihani tulio nao sisi waislam ,watu wanasubiri wazeeke ndo wanaanza kushika ibada , wanaona hawawezi kufa wakiwa vijana , jamani tumrudie ALLAH tukumbuke moto unatusubiri , kwani zamaradi akivaa HIJAB hatopendeza ? aangalie steshen za kiarabu wasomaji habari wanajitanda mitandio mizuri na ya aina tofauti na wanafanya kazi na hawamuudhi mungu , sasa wewe msichana / mwanamke wa kiislam unatibua minywele huko kisa nini fashion ? yote haya mi nadhani inatokana na malezi wa wazazi wanapomlea mtoto , mtoto umleavyo ndivyo akuavyo...
ReplyDeletewabilah tawfiq
hivi huyu zamaradi ana asili ya kisomali ??
ReplyDeletekhaaa !!!!1
ReplyDeletejamani ALLAH yupo siku zote sio mwezi wa ramadhan tu hee
maana kama mtu huwajui hawa utasema watu wa dini sanaaa ... kumbee..mmhhh
subiri ramadhani iishe , hizo nguo zinawekwa kwenye masanduku mpaka mwakani ...
mdau
kenya
huyo zamaradi muislamu alafu vazi aliloovaa unaweza sema nilaheshima haswaa kumbe sidiria na tumbo lote laonekana looooh wamkufuru mungu tu wewe,, nguo transparent hiyo inamaana washindwa hata kuvaa vest ndani yake.. minilidhani ndio wakukuoa kumbe ndio wale wale tu kweli wahenga wasema kizuri cha jiuza kibaya chajipendeza. USHAURI WA BURE HUO WALA SIUZI.
ReplyDeletejamani ni kweli mdau wa hapo juu ulivyosema hii stara iko wapi lakini mbona zamaradi tumbo lote laonekana.. hayo madera ni mepesi mnoo jamani.
ReplyDeleteWatu wengine bwana mnaboa sana. Kusema "aangalie steshen za kiarabu"!!!?? Huu wote ni ukoloni tu. Kwani na sisi hatuwezi kuwa na utamaduni wetu. Tuna makabila zaidi ya 120 na kila kabila lina utamaduni wao wa mavazi na kila kitu. Kwanini tusijitolee mifano wenyewe mpaka twende kwa waarabu au wazungu!!??
ReplyDeleteZamaradi naomba kukuoa.
ReplyDeleteJ. Mashaka
umeambiwa uangalie steshen za kiarabu kwa sababu makabila yote 120 ulotaja hapo ya tz hamna kabila linalositiri mwili kama waarabu , na dini imeshusha arabuni na mitume yote waarabu ,UPO HAPO !! thats fact deal with it
ReplyDeletejamani shafii mbona unajiachia hv??tulisoma wote mbuyuni primary u had a good body. slim. tafadhali. good diet ni muhimu kwa maisha. mwanamichezo weye ati.
ReplyDeleteMMEPENDEZA BWANA KWANI TUMBO LIKIONEKANA KUNAUBAYA GANI WAKATI SISI WANAUME NDIO TUNAPENDA MUONEKANE HIVYO KWETU KWANI NDIO INATUVUTIA ZAIDI,ENDELEZENI TU LIBENEKE DADA ZETU
ReplyDeleteNDUGU HAKIKA VAZI ZURI NI ZURI KWA MUNGU NA HATA JAMII PIA KUTOA MFANO KWA WAARABU HAINA UBAYA MAANA WOTE SISI NI BINADAMU YAANI WATOTO WA ADAM UBAGUZI AU UKABILA HAUNA MAANA .
ReplyDeleteSISI SOTE NDUGU NA NDIYO NENO BINADAMU LIMTOKANA NA BIN YAANI WATOTO NA ADAM NDIYE BABA YETU HII KWA KIARABU. INSHALLAH MUNGU ATUJALIE TUFUATE ALIYO AMRISHA NA TUEPUKANE ALIYO YAKATAZA AMEN.
kwa raha zenu watoto wa kike,,achaneni na manungayembe umu ndani wanaokomaa na tamaduni za kiarabu...
ReplyDeleteleo mkijisikia kuvaa buibui vaa,mkijisikia kuvaa chupi vaa,suruali vaa,pedoz vaa nk nk
nashwangaa yahusuuu!!
kumbe PJ mwarabu?safi sana
ReplyDelete......Dini hii(uislam) ni mila ya nabii Ibrahim.....mliitwa wa Islam tokea mwanzo na hata sasa.....na wala hatukuweka manbo mazito humo(Ndani ya Dini)shikamaneni na kamba hii na wala msifarakane.
ReplyDeleteEwe Mtume wa Mwenyezimungu, wake zako na mabinti zako wakitoka nje waamrishe wajisitiri kwa kufaa nguo zinazo hifadhi maungo yao.
(hakuna suala la uzungu wala uhindi wala mila na utamaduni...ni kufuata mazingatio tu)
Mdogoake Ustaadh.
Dada Zamaradi, Mola Muumba amekujalia uzuri, ucheshi, upendo na kipaji katika kazi yako. Mimi mshabiki wako namwomba Mwenyezi Mungu akulinde kila mahali na kila siku na akupe kila la heri. Amin. Keep it up girl.
ReplyDeleteWe anon wa 12:49:00 AM, wacha chuki na unafiki wako, siku zote wanawake wanatoka na vi-mini skirt hapa hamjawahi kulalamika ukoloni. Leo hii mnaonyesha chupi zenu chafu kwa kuwa hawa dada hawajavaa kizungu. Nina hakika wewe unavaa kizungu pia...hebu toa picha yako tukuone umevaaje. Wacha kutuvunga sisi, dammit!!!!
ReplyDeleteZamaradi and company, si mnajua tena Watanzania walivyokuwa na wivu. Maadam mmependeza na you look happy lazima mtapata ma-haters wanaotokota kwa wivu. Msi-wamaind hao. Kazeni buti na endelezeni libeneke. Zamaradi's No. one fan. (a.ka. Happy Mvungi.)
ReplyDeleteZamaradi, mimi niko serious kuliko hao wengine. Wewe niambie tu nikutumie wapi picha na cv yangu na nipe tarehe ya interview. Mimi sitaki kukupotezea muda, nataka ndoa. (I am 30 and successful.)MHM. DSM.
ReplyDeleteANGALIENI SANA HAO HAWANA WEMA HATA KIDOGO MCHANA INZI USIKU KUNGUNI.
ReplyDeleteNJOONI MTAANI KWETU KAMA KUNA MTU ANA HABARI NAO WANABADILI SURUALI KAMA DALADALA ZINAVYO BADILI RUTI.
KAMA UNATAKA NENDA LAKINI USIJE TOKA BILA KUAGA
nifahamisheni,huyo mfupi kulia ni nani?
ReplyDeleteZamaradi, you are the best. Umependeza na tunakupenda. Wasiofurahi watafoka kisha watachoka na usiku watalala. All the best gal. Mshabiki wako wa Moshi.
ReplyDeleteCha ajabu ni kuwa wasichan wakitoka hapa wamevaa vichupi hamna anayekereka. Leo mabinti hawa wamevaa mavazi ya heshima ma-haters wamekuwa mbogo. Au kuna ajenda ya siri kwa hao ma-haters. Haters are loosers. Onesmo. (Mwenyekiti wa Zamaradi fan club Arusha.)
ReplyDeleteZ-A-M-A-R-A-D-I, WE LOVE YOU=TUNAKUPENDA...GOD BLESS YOU!!! AMEN.
ReplyDelete