Mgombea Mwenza wa urais, Dk. Mohamed Gharib Bilal akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Mchinga, Said Mtanda, wakati wa mkutano wa Kampeni uliofanyika leo kwenye Kijiji cha Kilangala, Wilaya ya Lindi Mjini Mkoa wa Lindi.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mchinga kupitia tiketi ya CCM, Said Mtanda (kulia) akiteta jambo na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Mudhihir Mudhihir, wakati walipokuwa wakimsikiliza mgombea Mwenza wa urais, Dk. Mohamed Gharib Bilal katika mkutano wa Kamapeni uliofanyika kwenye Kijiji cha Kilangala leo
Mgombea Mwenza wa Urais, Dk. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Muhdhihir Mudhihir, baada ya kuwasili kwenye Kijiji cha Kilangala kwa ajili ya mkutano wa Kampeni leo. Mudhihir alionyesha uzalendo kwa kupanda jukwaani na kupiga debe kumuombea kura mgombea Ubunge wa jimbo hilo, Said Mtanda, aliyepita katika kura za maoni na kuongeza kuwa atakuwa naye bega kwa bega kumnadi ili kuhakikisha anashinda na kuwa Mbunge wa Jimbo hilo.
Mke wa Mgombea Mwenza, Asha Mohamed Gharib Bilal akicheza pamoja na wasanii wa Kikundi cha Siasa Makondeko, aliposimama kuwatunza baada ya kufurahishwa na ujumbe wa wasanii hao wakati wa mkutano wa Kampeni wa Mgombea Mwenza, uliofanyika kwenye Kijiji cha Kilangala Wilaya ya Lindi Vijijini leo.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kilangala wakiwa kwenye mkutano wa Kampeni wa Mgobea mwenza. (Picha na Muhidin Sufiani - LINDI)


Hii kweli ni blog ya kyama!
ReplyDeleteHe!! Kweli Bongo hakuna lisilowezekana. Hadi Said Mtanda anagombea ubunge. Anyway, najua Said ulitoka mbali. Nakumbuka enzi za UDSM, ulikuwa machachali sana kwenye stori za siasa pale kijiweni TBS. Na nakumbuka mkuu wa kaya alikuwa akikutumia kuwapata mademu wakali wa UDSM. KILA LA HERI. Madu wa TBS/ATB 200202206.
ReplyDeleteMimi tatizo langu ni kuharibiana majina tu...watanzania tuna tabia ya kuharibiana majina....Muhammed--Mwamedi,John--Joni, BILAL--BILALI!!
ReplyDeleteI take offense on that kama mwenyewe anasema anaitwa BILAL...siyo BILALI jama ni BILAL. Jina la mtu lina maana kubwa sana...herufi moja tu lakini inaharibu maana. Kha!
Yaani hebu ona.. wanakijiji wanashangilia lakini nyuma ndiyo unaweza kujua hali ya maisha yao.. nyumba ya nyasi... nadhani huduma nyingine ndiyo duni kabisa..hivi hawa wabunge wote waliopita wamewasaidia nini? na huyu atabadilisha vipi maisha ya watu? ndiyo yale yale..longolongo tu!
ReplyDeleteHiyo picha ya chini kabisa inatoka nchi gani?
ReplyDeleteMwe!!!! Hawa kweli ndio wadanganyika halisi
ReplyDeleteSamahani Mkuu wa Kaya...naomba kuuliza, hivi Mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Mudhihiri Mudhihiri hana mkono wa kulia? Maana katika picha ya tatu sioni mkono wake wa kulia. Naomba mnieleweshe.
ReplyDeleteKama sikosei, nakumbuka Muhdhihir Mudhihir alipata ajali na kukatwa mkono mmoja.
ReplyDelete