Baadhi ya Waendesha pikipiki wa Umoja wa Chama cha Mapinduzi CCM wakisindikiza Gari lililombeba Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akielekea kwenye Ofisi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC leo, kwa ajili ya kurejesha fomu baada ya kukamilisha kujaza Vipengele mbalimbali vilivyomo ndani ya fomu hizo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikabidhi fomu za kugombea Urais kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Khatib Mwinchande kwenye Ofisi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Maisara mjini Zanzibar leo, baada ya kukamilisha kujaza vipengele mbalimbali vilivyomo kwenye fomu hiyo.
Umati mkubwa wa Wana CCM pamoja na Wananchi wa Zanzibar wakisindikiza Gari lililombeba Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk. Ali Mohamed Shein lilipokuwa likipita katika mitaa ya Michenzani Zanzibar, alipokuwa akielekea kwenye Ofisi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Maisara mjini Zanzibar leo, kwa ajili ya kurejesha fomu za kugombea Urais baada ya kukamilisha kujaza Vipengele mbalimbali vilivyomo katika fomu hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hiyo picha ya kwanza mnaona tofauri jamani. Gari kubwa, msafara mkubwa, ulinzi wa gharama, mapikipiki, nk lakini pembeni ya gari nyumba ya mbavu za mbwa. Picha yenyewe tu ni kielelezo cha ufujaji wa hela za walipa kodi kwa kampeni wakati watu wana umaskini mkubwa. Lakini bado viongozi wanaona sawa na watu wanashangilia tu na kuona sawa kama mazuzu

    ReplyDelete
  2. hi!hi! naona ras makunja na gitaa akiwa pembezoni mwa gari la Dr.Sheini,si mchezo mpaka pamba aka gwanda kapewa mpya,viatu vipya

    ReplyDelete
  3. Mbona picha za wagombea wengine unazibania Michu?

    ReplyDelete
  4. mikwara hoyo hiyo ya nini !! kwani hamuwezi rudisha hizo form kikawaida tu !

    ReplyDelete
  5. Hiyo gari kwenye picha ya kwanza haiendani kabisa na mazingira yanayoizunguka.

    ReplyDelete
  6. Ama kweli watanzania hatuna la kufanya! umati wote huo umeacha kazi zao kwa nini? mtu mmoja tu kupeleka maombi ya kuwania urais!

    Laiti watanzania na viongozi wake wangelikuwa wanapitisha jitihada na kujituma namna kama hii jua na mvua naamini tanzania tungelikuwa na maendeleo makubwa mno.

    Mamilioni ya pesa za uma zinatumika kwa shuhuli hizi na wananchi wako radhi na kufurahia, hivi kweli kuna haja ya yote haya? ona magari ya serikali na ulinzi mkali! ni kiasi gani hapo kimetumika!

    Ama kweli Tanzania tambarare.

    ReplyDelete
  7. wakati kama huu si ingekuwa vizuri kama kiongozi angechukua fursa ya kutembea na wananchi ktk harakati za kuomba kura zao badala ya kukaa kwenye gari kama vile wanasindikiza jeneza. Samahani kwa mfano wangu.

    ReplyDelete
  8. Unajua ni kama cult vile ukishaingia humo kila kinachosema kwako ni yes sir, yes sir...We uliona yule leader wa Mormon aliokua anakula vizuri na kuchukua mali na wake za wale watu wengine? Unajiuliza wale watu walikua wamevurugwa akili au ni nini? Ndio hayo nchi watu wamechoka lakini wako so happy wakiona viongozi wao wanapeta tu na magari na maisha mazuri...Wakilala na njaa sawa, wakishindwa kusomesha watoto wao sawa, shule zikiwa hazina kitu sawa....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...