Mkuu wa kazi Michuzi.
Nakusabahi..
Kwa heshima na taadhima naomba unifikishie ujumbe huu kwa wadau. Hili jambo sio mara ya kwanza kutokea na kuripotiwa na kama inavyoonyesha hapa, wahusika hawapendi mambo haya yafike kwenye vyombo vya dola na vya habari. Wanapenda kuyamaliza kimya kimya ili shule zao zisiathirike ki-hadhi (reputation) na kibiashara!!!.


Hawajali na kulinda haki na utu wa watoto kwa nguvu na gharama zozote hata ikibidi kuathirika nilikokusema. Tumwamini nani? Usalama wa watoto wetu uko wapi? Ni nini kifanyike kuzuia haya mambo? Sio watoto wote watakuwa na ujasiri wa kusema.


Sio wazazi wote wenye umakini wa kuwachunguza watoto wao wanapotoka mashuleni, wengi hurudi nyumbani usiku wanakuta watoto wameshalala na watoto asubuhi huandaliwa mapema sana na haraka haraka sana kuwahi school bus (lazima wazazi tuwajibike, hakuna excuse). Tusipopata jawabu la ulinzi mashuleni na ndani ya mabasi watoto wetu kutoka kwa mamlaka za shule, watapona kweli?

Mdau Anon.....
Asante.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Uovu wowote ule hufanyika baada ya kuona udhaifu uko wapi.
    1. Mbakaji alijua kuwa bibi wa mtoto hana uelewa wa kutosha wa sheria na alikuwa na uhakika mambo yataisha hivi hivi.

    2. Mbakaji alijua uhuni wa shuleni kwao ( st mary's kwa ujumla) alijua walimu watamtetea kwa kuwa ni kawaida ya shule hiyo kubaka watoto na wasiseme majumbani.

    Tunaomba uchumguzi ufanyike ili kubaini wafanyakazi na walimu wa shule hiyo wenye tabia ya ukwale.

    Inasikitisha sana kuona mtoto miaka minne, bwana mtu mzima anamuingilia jamani... dude lote hilo kumsokomeza mtoto ndogo sijui ni starehe gani au ni mambo ya kishirikina?

    Na kiongozi wa shule hizo achunguzwe kwa kuwa kama wafanyakazi wanaamua kuwa mafilauni, ufilauni unaanzia juu.

    Kweli inauma sana .Mtoto unamzaa vema then mtu ambaye hajui hata matatizo uliyopata kumkuza mtoto mpaka hapo anamwambukiza ukimwi!!

    ReplyDelete
  2. shwain kabisa huyo dereva, jamani kama kuna ma lawyer wanasoma blog ya jamii tunawaomba msaidie hii kesi hilo zimwi lisekwe lupango, ukute bado linaendeleza ufirauni wake, haki ya nani huyo angekuwa mwanangu mshenzi huyo angejuuuta kubaka ningemuundia tume ya kukata hilo dubwasha lake pambaff!!

    ReplyDelete
  3. HILI SWALA NI KUBWA NA NILAZIMA WADUA WAJUE MWISHO WAKE. HATUA YA KWANZA INABIDI UONGOZI WA SHULE HII UWAJIBISHWE KABISA. HAIWEZEKANI viongozi wa shule ambao ni wazazi wafumbe macho kwa kosa kama hili. Swali ni kwamba je hao walimu kama mtoto wao angefanyiwa hayo mambo wangekaa kimya? Such kind of persons are really criminals.

    ReplyDelete
  4. Pole sana mtoto alebakwa na familia yake kwa ujumla. Pole kwa wazazi wote kwani najua uchungu unaotupata kwa mtoto kama huyo kubakwa. Na pole kwa taifa zima kwa kua tatizo hili linatuhusu kwa namna moja au nyingine.

    Kwa upande wetu sisi wazazi hii ni changamoto kubwa kwetu kwenye mamuuzi ya malezi ya watoto wetu. Maswali tunayotakiwa kujiuliza je kuna usalama kwenye malezi ya kila siku kwa walezi tunaowaachia wawalee watoto wetu wakati tukiwa kwenye shuguli zetu za kila siku?! Tukianzia mahausigeli, mahausiboy nyumbani, madereva na makondakta wa mabasi ya wanafunzi, wauza maduka, waalimu shuleni, wanafamilia na marafiki ambao wanazizunguka familia zetu?? Jibu ni hapana.......Cha msingi ni kuishi kwa tahadhari kubwa sana, hakuna wa kuaminika!

    Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

    ReplyDelete
  5. Tujifunze ujanja wa mjini jamani. mlezi alitakiwa kuripoti polisi haraka halafu polisi ingempeleka sibitali apimwe hadi DNA.

    au mama naye mshabiki wa shule hataki itiwe dosari?

    ReplyDelete
  6. inasikitisha na kutisha hiyo shule inabidi kweli wajibu maswali mengi sana kwanini hawakupeleka taarifa police wazazi wanatakiwa waishitaki shule pamoja na huyo dereva ni kuomba mungu ajamwachia mtoto wa watu ukimwi na kaisha mwalibu huyo mtoto akikua atajua nini kilimtokea.hope huyo dereva atachukuliwa hatua kali ya kisheria. pia asante ankal kwa kutujulisha habari kma hizi ili tuweze waeleza wanetu kujiami kama wanadanganywa na watu kama hao wawe wazi kuwaeleza wazazi bila kuona aibu au kuficha maana najua mila zetu wazazi huwa hawawafundishi watoto kutoa taarifa kama kitu kibaya kimefanyika kwake,na pia shule zingekuwa zinawajulisha watoto wawe makini wasimwamini mtu wanaweza danganywa na mia mbili au chips.ankal tujulishe kitakachoendelea na pia ankal ukiweza ungewasiliana na shule kujua hao madereva wanawaajiri huwa wanajulishwa namna ya kufanya kazi zao vizuri bila kufanya vitendo vya kinyama kama hivyo.

    ReplyDelete
  7. KWANINI SWALA KAMA HILI LISIVALIWE NJUGA KAMA UDOKOZI? WATU KAMA HAWA NI KUPIGA MAWE TU! HAKUNA KUJIULIZA, HUYO BIBI NAE JAMANI!! ETI APIMWE UKIMWI!! AMEUMIZWA HUYO MTOTO, KAVIMBA!! UNATAKA APIMWE TENA? ISHAKUWA ZALI UKIMWI OR NOT, HAKUTAKIWA KUMGUSA. JAMANI KINA MAMA CHUNGENI VIFARANGA VYENU, KUNAMIKUNGURU SHWAIN KILA ENEO, SHULE, NYUMBANI, KANISANI, MSIKITINI, ANAKOCHEZA.... CHUNGENI SANA.

    ReplyDelete
  8. Watoto hawasahau kilichowatokea utotoni.. nakumbuka nilivyokuwa na umri kama huo babangu alikuwa uk kikazi na mama alikuwa akitoka asubui kwenda kazini na kurudi jioni.. tulikuwa tunabaki mfanyakazi wa ndani,mimi(mvulana) na binamu yangu wa kike...yule dada wa ndani aliniamuru nifanye mapenzi na yule binamu yangu huku kashika fimbo, i was 4 or 5years old and binamu yangu alikuwa kama 7years...sidhani kama kuna mtu mwengine anajua mana sikuwai kusema and now nimekua sijawai muliza binamu yangu kama anakumbuka..alitufanyia ivo once badae akafukuzwa kazi au aliiba home nadhani, sikumbuki vizuri....wazazi wawe wangalifu na watoto wadogo.

    ReplyDelete
  9. Huyo mtu wa kuuliwa kabisa. halafu ati jina linahifadhiwa. Kwanini wanamuhifadhi jina bongo watu wanaoumizwa watatajwa majina lakini muumizaji jina linahifandhiwa. Huyo mtyu ni Mungu atakayemulaani na angekua amebaka mtoto wangu...honesty sasa hivi angekua historia...Nikafie jela lakini ningehakikisha hawezi kuishi hata siku moja nyingine na kuharibu watoto wa wengine. Utajua amebaka watoto wangapi? Huyo atakua sio wa kwanza...

    halafu bibi wa watu aka kaa mpaka jumatatu kwenda kumtafuta huyo mtu..Hastahili hata kuishi huyo tena..Mtoto wa miaka minne!!!!!

    Shetani mkubwa huyo na serikali iko wapi jamani? Mtoto wa miaka minne hawezi kusema uongo na kama hospital ilishaona hameumia basi huyo ni wa kufungwa maisha

    ReplyDelete
  10. YESU WANGU, JAMANI MM NIMEUMIA SANA ROHO! KWANZA NI KWANINI WALIMLAGHAI HUYU BIBI ANYAMAZE, PILI WATUMIE MADAKTARI WAO, HIZI ZOTE NI NJAMA ILI HUYO DAKTARI ATOE TAARIFA ZA UONGO KWAMBA AJABAKWA! WAZAZI TUAMKE, NASEMA HIYI HUYO BIBI KAMA ANASOMA TAARIFA HII ATOE NAMBA YAKE YA SIMU TUMPE USHAURI. HILO JANGILI LAZIMA AHASIWE!

    MUNGU AMSAIDIE HUYO MTOTO ASIWE NA VIRUS VYA UKIMWI. OH! MUNGU BABA WA ISLAEL NAOMBA UMBARIKI HUYO MTOTO AWE MZIMA.

    MAMA MLOLWA

    ReplyDelete
  11. ni wakati wa kufanya mabadiliko, hizi kesi zipo nyingi na haziripotiwi kwa sababu ya udhaifu uliopo kwenye jamii yetu. Nashauri mabasi ya shule yaendeshwe ya wanawake na makondakta wawe wanawake , kwa sababu katika jamii yetu mama ndo ana jukumu kubwa la kulea mtoto, kwa kiasi kikubwa itapunguza ubakaji

    ReplyDelete
  12. kwa kweli hili swala la madereva kubaka watoto limezidi sasa, jamani tukimbilie wapi, watoto wetu wasisome? Mhe Rais tunaomba uangalie swala hili kama ulivyoliangalia swala la uuaji wa walemavu wa ngozi (albino) kwa kweli wazazi tunateseka na wenye mashule na hawa madereva wao wa mabasi wabakaji. Imagine mtoto wa miaka minne mtu mzima ukamwigilie bila hata huruma. ee mola kisaidie kizazi cha Tanzania......

    ReplyDelete
  13. Huyu bibi nafikiri naye ni kutojali. Nani siku hizi hajui kuwa kubaka ni kosa la jinai? Hata katika jamii yetu, mtu wa kawaida tu anajua kuwa kubaka ni udhalilishaji wa hali ya juu. Huyu mjukuu ni ni kwa upande wa mtoto wake wa kiume. Angekuwa wa kikeni angemshughulikia.

    Unajua hawa mabibi hupendelea wjukuu wa kikeni.

    Naye awajibishwe kwa uzembe wa kutomjali mjukuu wake, eti anamkanda maji ya moto. Kwani alitoka kujifungua? halafu anasubiri siku zipite ndio aende kuuliza eti shuleni.. Au alitaka kumkomoa mkwe!

    ReplyDelete
  14. Watoto mara nyingi hutishwa na na wabakaji na kuambiwa wakisema watauawa. Na baada ya hapo huendelea na mchezo mpaka ha Mungu akijalia kugundulika.

    Anayesema wazazi tuwe makini, ni sawa, lakini naona huyo hana mtoto, au kama anaye hajui mambo yaliyo nyuma ya mapazia. Mtoto labda uamue asiende shule, kucheza, msikitini/kanisani n.k. vinginevyo ni ulinzi wa Mungu tu.

    Tulidhani labda wanafunzi wakipelekwa shule na kurudishwa na basi la shule itakuwa salama yao kwa wabakaji wa njiani, kumbe wanakutwa hata humo humo kwenye mabasi ya shule.

    Labda kuwe na utaratibu wazazi wapewe nafasi kazini, ili waweze kuwachukua watoto wao shuleni. Asubuhi ni rahisi kuwapeleka.

    ReplyDelete
  15. ni kweli kabisa mabasi ya shule yaendeshwe na wanawake kama marekani almost mabasi yote ya shule yanaendeshwa na wanawake.

    ReplyDelete
  16. sina uhakika kama hili suala St Mary watalishughulikia ipasavyo,mtoto si wa kwao ni wakwako kuhusu shule ina hadhi kiasi gani hiyo wala haikuhusu.Ukiwa kama mzazi wa mtoto inabidi ulishikie kidedea suala hili ikiwa ni pamoja na kuripot police kuhakikisha mtuhumiwa anatiwa hatiani haraka sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...