JK akiwashukuru kinamama wa Ngara ambao waliandaa futari kwa ajili ya msafara wake wa kampeni ulioingia usiku huu hapo mjini Ngara na kuhudhuriwa pia na wakaazi wengine wengi. Alikuwa akitokea Karagwe ambako kutwa nzima alipita sehemu mbalimbali kuomba kura na kunadi wagombea wa ubunge na udiwani. Baada ya Ngara ataelekea Kigoma



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. jk wewe ndio mgombea pekee usiye na udini wala ukabila ni bora uwa maskini kuliko kansa ya udini

    ReplyDelete
  2. jk bado anafunga?mbona tunachanganyikiwa

    ReplyDelete
  3. CUF THE PLOBLEM UDINI!CHEDEMA THE PLOBLEM UKABILA NA UKASKAZINI,VIJIJINI 98% NI CCM

    ReplyDelete
  4. kuitoa ccm madarakani itachukua miaka zaidi ya 100 kwani matajiri wote wapo ccm,vijana wasomi wote wanakimbilia ccm,karibu kila mtu maarufu hata watangazaji wote wanataka ccm

    ReplyDelete
  5. hongera jk kwa miaka 5 iliyopita ya uongozi bora ,hongera kwa dodoma university!big up usisikilize longo longo za wachache hawaitakii mema bongo

    ReplyDelete
  6. anony hapo juu sure chama gani viongozi na wafuasi karibu wote dini moja hyo siyo tanzania ya mwl nyerere

    ReplyDelete
  7. HONGERA CCM HADI SASA TAYARI WABUNGE WENU 16 WAMESHINDA KABLA YA UCHAGUZI HAPO OCTOBER HIYO INATHIBITISHA KUWA CCM NI NAMBARI ONE TUNAMUOMBEA JK USHINDI WA TSUNAMI ILI TANZANIA TUENDELEE KUISHI KWA AMANI SIO KAMA SOMALIA KWANI AMANI NDIO MTAJI NAMBA MOJA HAPA DUNIANI,GOD BLESS JK,GOD BLESS UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

    ReplyDelete
  8. Uzuri wetu wabongo ni kutokuwa na kabila wala dini.Na kizuri kikubwa ni uwezo wetu wa kusahau mambo kwa kipindi kifupi.Kuna wengi walikuwa wanaipiga vita sisiemu na Jk miaka 2 iliyopita sasa wanadai sisiemu ni chama bora. Naamini baada ya mwaka mmoja wa awamu ya pili ya Jk wengi wanaoandika na kuisifia sisiemu na Jk watakuwa wanawapiga madongo na kuapa kutoifagilia ktk uchaguzi ujao.

    ReplyDelete
  9. Mbona hutoa hoja yangu ndugu yangu, hizi ahadi anazotoa kila mara atatoa fedha wapi za kulipia vitu vyote hivyo? Ni swali rahisi tu, likini unaubavu wa kulipost?

    ReplyDelete
  10. Kinacho ikwamisha hii nchi ni kukosa mawazo mbadala ya CCM, kila mtu CCM CCM, herd mentality...swimming in ignorance!

    ReplyDelete
  11. Watanzania popote pale mlipo mjue kuwa kuomba radhi ni kujidhalilisha kwa namna flani lakini ndio njia pekee waitumiayo wastaarabu katika kurudisha heshima iliyopotea!!Hakika kuyakana maneno yako mwenyewe uliyoyasema hadharani ni sawa na kuvaa chandarua ukidhani umejisetiri!!!Wafanyakazi 350,000 na ndugu na jamaa zenu hata mkigoma kwa miaka minane......Huko kungine simo!!

    ReplyDelete
  12. wewe anoy hapo juu unayechanganyikiwa ni kwa upuuzi wako tuu, soma vizuri caption,(kwa ajili ya msafara wake) kwani asipofunga jk watu walio katika msafara hawafungi? sio lazima mradi tu uandike chochote.


    JK akiwashukuru kinamama wa Ngara ambao waliandaa futari kwa ajili ya msafara wake wa kampeni

    ReplyDelete
  13. JK HUKU MTAANI BADO KUNA TATIZO LA UJAMBAZI MITAA YA MBEZI NA HII NI TAKRIBANI MIEZI ZAIDI YA MITANO SASA INAMAANA KOVA NDIO AMESHINDWA AU ? PIA VP WAPIGA KURA WAKO NA MUSTAKABARI WAO WA PESA ZA DESI? BADO KILIO MTAANI SASA HII VIP KTK MIKAKATI YENU AU NDIO HAWA WATU WAMEZULUMIWA?

    ReplyDelete
  14. TATIZO CHADEMA ZITO MCHAGA, SLAA MCHAGA, PROFESA ALIYEFUKUZWA UDSM KWA KUWA KADA WA CHADEMA MCHAGA NA WOTE HAW NI WAKATORIKI; HUU NDIO UJINGA WALIONYWESHWA WANA CCM WAAMINI HIVYO KWANI HAWAJUI SIRI ILIYOMO NDANI YA KOFIA WANAZOPEWA.

    ReplyDelete
  15. Inakuhusu mdau wa kwanza hapo juu.

    Tusipende kuleta hisia zisizo za msingi. Unazalisha chuki ndugu yangu, mtatupeleka kubaya! Hivi Tanzania hii ya leo kuna mgombea wa uraisi, ubunge au udiwani ambaye ni mdini? Kwa vigezo vipi? Kipi cha udini anachoeneza na ni nani huyo mtu?

    Kwa jinsi ninavyojua kama angekuwepo mgombea ambaye ni mdini basi angekuwa amekwishatolewa.

    Watu msiongee nonsense kwa vile tu ni muda wa uchaguzi.

    ReplyDelete
  16. TAKUKURU.....hii imekaaje?

    ReplyDelete
  17. Nani ni mgombea wa kiti cha ubunge huko Ngara?

    ReplyDelete
  18. HONGERA NINI ZA CCM KUWA NA VITI 16 VYA WAZI HIYO NI FAULO YA TUME YA UCHAGUZI INAKUWAJE WAGOMBEA WOTE WALIOKUWA DISQULIFIED NI WA UPINZANI HAKUNA WA CCM HATA MMOJA UKIZINGATIA YULE WA NZEGA DK KIGWANGALA NI VITUKO TUPU ANATAKIWA ASIWEPO KWENYE KINYANG'ANYIRO KWA SABABU ANAKSORO?

    ReplyDelete
  19. Anon aug 26,3:21Pm
    Mimi MBIGIRI GWASSA NIYONZIMA NDAYISHIMIYE VYAMUNGU NDEREIMANA NIKIZA NZOYISABA ndiye mgombea ubunge wa Ngara pekee kupitia chama kile kile.Nawaomba mnipe kura zenu za ndiyo.Nawaahidi kuwapa Ibishibura,umuramba,imeke,imarasene wananchi wote wa Ngara.Na nina ahidi nitaangamiza IVUNJA Ngara nzima.Abwamahanga msiniulize nimeandika nini.Wangara watanielewa

    ReplyDelete
  20. kwa wachawi na majambazi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...