Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua jana rasmi mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa waliopigana vita vya Majimaji uliojengwa katika kijiji cha Nandete kata ya Kipatimu wilayani Kilwa eneo ambapo vita hivyo vilipangwa na kuanzwa.Amiri Jeshi mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka silaha za kijadi katika mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa wa vita vya Majimaji katika kijiji cha Nandete, kata ya Kipatimu wilayani Kilwa jana mchana.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuashiria kuzindua mradi wa umeme wa gesi ya asilia huko kijiji cha Somanga Fungu, mkoani Lindi jana jioni.Kushoto ni Waziri wa Nishati na madini William Ngeleja na kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa TANESCO William Mhando.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe kuzindua mradi wa Umeme unaotumia gesi ya aslia huko Somanga Fungu jana jioni.Huko waziri wa Nishati na madini William Ngeleja(watatu kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Wiliam Mhando(wane kushoto) wakiangalia.Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Said Meck Sadiq.

(picha na Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. hiki kitambaa cha kijani na mradi wa umeme kinaendaje? mimi sina chama inaniuzi kuona wahusika wanafanya vitu kwa jazba za kujipendekeza kwa mtu anaye ongoza nchi.

    ReplyDelete
  2. baada ya miaka kadhaa huu mnara utabadilishwa jina na kuitwa mnara wa JK.
    Hii inaonyesha ni jinsi gani wajinga hawautambui umuhimu wa historia.

    Shule yangu, "Kigogo Darajani" iliitwa "Gulman Rutihinda" eti kwa sababu mwalimu mkuu wa wakati ule alikuwa na urafiki "wa ndani" na muheshimiwa Rutihinda.

    ReplyDelete
  3. lakin tanesco wana ubia na rangi ya kijani we chunguza tu vizuri mkuu hapo juu.

    ReplyDelete
  4. Mbunifu wa mnara sijui kasoma wapi lakini ninavyo jua ni kwamba mnara wa matofali ya Cement si wa kudumu.Tunayo mawe ya kutosha na magumu kuweza kukaa miaka mamia kadhaa au hata elfu.Sijui kwanini hakufikiri hilo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...