Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia na kumsikiliza msichana mlemavu Joyceline Paulo huko Rusahunga wakati mgombea huyo aliposimama kuwasalimia wananchi na kunadi ilani ya CCM.Dr.Kikwete aliahidi kumpatia mlemavu huyo baiskeli maalumu ya matairi matatu ili aweze kumudu shughuli zake kwa urahisi zaidi.Dr. alikuwa njiani akitokea Ngara mkoani Kagera kuelekea Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kwa barabara
Dr.Kikwete akiwahutubia wananchi wa kijijini Rusahunga wakati aliposimama kuwasalimia na kunadi ilani ya CCM wakati alikuwa njiani akitokea Ngara mkoani Kagera kuelekea Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kwa barabara.
(Picha na Freddy Maro)
Hiyo picha ya Ndugu Jakaya na mwanamke mwenye ulemavu inaonyesha UTU, HURUMA, UPENDO na UKARIMU alionao na kwamba anawajali watu. Mungu akulipe kwa kadri yako kwa sadaka uliyoitoa.
ReplyDeleteSiyo kebehi wala nini, Rais wetu ana moyo wa utu; tatizo ni uwezo wa kufanya makubwa ya kubadili nchi.
ReplyDeleteMbona unaminya picha za vyama vingine? Biased or what?
ReplyDeletewalemavu kama hao wapo wengi sana !! si adi siku ya uchaguzi ndo kuwasaidia watu kama hao ni haki yao kusaidiwa na serekali. kweli tunashindwa kuwapatia hata basikeli how masikeli ya mlevavu ? mimi ningekuwa rahisi ninge ningesitisha hata marupurupu ya wabunge ya mwaka hili kuwasaidia walemavu !! Shame on US kweli tunashindwa kila kitu! what is there that we can do for our ppl !! hata misaada tukipewa mnatafuna kila kitu mnatafuna wenyewe, kweli hamna hata huruma!!
ReplyDeleteHizi huruma ambazo hajaziona kabla, unakuja kuziona uchaguzi unaanza. Msitudanganye hana cha huruma wala nini!!!!!!!! Ni walemavu wangapi wamejaa Dar es Salaam. Anafanya hivi kwa sababu ya uchaguzi hana lolote.
ReplyDeleteMdau USA
Basi angewaonea huruma wakina babu seya na watoto wake pia wanaokula life time jail sentence for nothing.
ReplyDeleteNaungana na mdau wa kwanza na wa pili katika safu hii. Hii ni picha inayogusa moyo sana!
ReplyDeletewewe unaesema akina babu sea wanakula life time 4 nothing ni hakimu? unajua watoto wale wenye miaka kati ya 6 na 12 sasa hivi wana umri gani? unadhani mtoto wako wa kike aingiliwe kimapenzi na mwanaume ktk umri huo na unajua kabisa si lazima ushauri wa dr. kwani hata wewe ukimchungulia unaona alivyoharibiwa ungejisikiaje? maoni mengine ni hopeless sana
ReplyDeleteninachotaka kusema ni kwamba kwenye sheria ushahidi ukithibitisha pasipo na shaka huruma inawekwa kando, hatutaki taifa la wabakaji,walawiti wala mafisadi. muhalifu hapaswi kuonewa huruma. so mdau unaehusisha huruma kwa mlemavu huyo na waharibifu wa watoto wetu wakike umenibore sana. KIKWETE OYEEEEEEEEEEEEEEEE,MI NAMFAGILIA SANA JK, BASI TU IMPLEMENTERS WANAMUANGUSHA
ReplyDeletePicha inagusa moyo and then what...Kama inagusa moyo he is a leader...He can and he is able to help out. Tz tuna watu population gani na naamini hata kama tuna watu million 10 vilema serikali kama wanataka ina uwezo kabisa wa kumpatia kila kilema means of transportation. Kama ni wheelchair, magongo au tricycle serikali ina uwezo kabisa wa kutoka kwa watu hao. Na kuna wengine wanachohitaji ni miguu tu ya bandia sasa kwanini wasiweze kuwapa? Nchi nyingine vilema wanapewa nyumba ya kuishi, chakula na jinsi ya kumwezesha kufika kutoka point a to b. Sasa hao vilema wetu kama hatuwezi kuwatunza kwanini tushindwe tu kuwapa something to make them at least mobility able na mengine watajitafutia wenyewe. Kwa nini isie haki ya kilema kupatiwa njia ya kumwezesha kumudu maisha yao. Wengine wanashindwa kufanya chochote kwa kukosa tu miwani ya dola 100.
ReplyDeleteKama tunaweza kununua magari ya serikali ya nguvu hivyo na kuwalipa wabunge na watumishi waserikali vizuri hivyo kwanini washindwe kwa watu hawa?
Upost usiposti lakini ukweli ndio huo kukaa hapo chini na huyo mtu hakutamsaidia huyo mtu chochote au kumpunguzia machungu ya maisha aliyo nayo
Hana lolote,hana cha huruma wala shangazi yake huruma.angekuwa na huruma nchi hii isingekuwa na ombaomba wala walemavu wasingetaabika ingawa asingeweza kuwasaidia wote lakini angalau angewaweka katika hali nzuri fulani hivi...anyway hapo ni katika kutafuta kula yake kwa wananchi ili baadaye akishapewa hiyo shibe siye tuendelee kutaabika huku ye ananeemeka.
ReplyDelete