Jumiya ya Watanzania nchini Japan umepata uongozi mpya ambao utaingoza Jumuiya hii kwa muda wa miaka miwili.

Uchaguzi ulifunguliwa na afisa Balozi wa Ubalozi wa Tanzania Japan bwana Francis Masongo.Nafasi zilizokuwa zinagombewa ni Mwenyekiti wa Jumuiya,Katibu Mkuu wa jumuiya,Makamu katibu Mkuu wa jumuiya na Mweka Hazina wa jumuiya.

Dr Yahaya Simba aliibuka Kidedea kwa kunyakua Uenyekiti wa Jumuiya,Nafasi ya Katibu Mkuu ilikwenda kwa Bwana Julius Mombeki,Makamu Mwenyekiti ni Bwana Rajabu Njenga,Makamu Katibu mkuu wa Jumuiya ni Bi Asmah Kobayashi na Mweka hazina Mkuu ni Ostadhi Juma Kipaya. Uongozi huu mpya Utatuongoza kwa miaka miwili.

Picha zaidi nenda kwa blog maarufu hapa Japan ambayo ni
ahmed-kidume.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Dr LusinguAugust 02, 2010

    Congratulations Comrades! Nice to see something you are passionate about happening in other places.

    ReplyDelete
  2. Ulimbukeni tu huo!! Hamna kazi za kufanya au? Acheni ushamba...

    ReplyDelete
  3. Ustaadhi juma kapuya duh hujabadilika hata kidogo duh . tangu tuachane singida DSA mpaka leo sura umbo lile lile. au ndo ma herbal(kiti moto) ya kijapan?

    ReplyDelete
  4. Dah huyo jamaa wa kushoto amekuwa kama mjapani kwa pozi lake,manake anaonekana ukimzingua tu anakupa mbili za kidevu na moja ya mbavu then unatulia kimyaaa!

    ReplyDelete
  5. NI RASHID NJENGA SI RAJABU, JAMAA TULIKUWA NAYE NBC MAKAO MAKUU NA PIA IFM, JAMAA NI KICHWA KWELI, ALIKUJA KWA MASTER IN BUSINESS ADMINISTRATION-MBA STUDIES HAPA LONDON-UK KUANZIA MWAKA JANA NA AMEMALIZA MWAKA HUU WITH FLYING COLOURS.

    ReplyDelete
  6. Mkuu Michuzi.. Tunaomba Habari za Mtikila... imekuwaje tena??
    Tumezisikia juu juu tu kwenye intaneti..
    Tupe nyeti zaidi braza.

    ReplyDelete
  7. Wewe anon. wa pili, nani kakwambia kuwa hawana kazi? ushamba si mzigo na kila mtu anao. Hata wewe unao wako!

    ReplyDelete
  8. Anony wa Aug 2, 10:39, yaani nimecheka sana na karate kid wako. Mbili za kidevu na moja ya mbavu kama Bruce Lee katika Enter the Dragon enzi za Empire Cinema,hahahahahhahahahahaha.

    Mdau wa Japan ninayemaindi muda wangu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...