Jumiya ya Watanzania nchini Japan umepata uongozi mpya ambao utaingoza Jumuiya hii kwa muda wa miaka miwili.
Uchaguzi ulifunguliwa na afisa Balozi wa Ubalozi wa Tanzania Japan bwana Francis Masongo.Nafasi zilizokuwa zinagombewa ni Mwenyekiti wa Jumuiya,Katibu Mkuu wa jumuiya,Makamu katibu Mkuu wa jumuiya na Mweka Hazina wa jumuiya.
Dr Yahaya Simba aliibuka Kidedea kwa kunyakua Uenyekiti wa Jumuiya,Nafasi ya Katibu Mkuu ilikwenda kwa Bwana Julius Mombeki,Makamu Mwenyekiti ni Bwana Rajabu Njenga,Makamu Katibu mkuu wa Jumuiya ni Bi Asmah Kobayashi na Mweka hazina Mkuu ni Ostadhi Juma Kipaya. Uongozi huu mpya Utatuongoza kwa miaka miwili.
Picha zaidi nenda kwa blog maarufu hapa Japan ambayo ni
ahmed-kidume.blogspot.com


Congratulations Comrades! Nice to see something you are passionate about happening in other places.
ReplyDeleteUlimbukeni tu huo!! Hamna kazi za kufanya au? Acheni ushamba...
ReplyDeleteUstaadhi juma kapuya duh hujabadilika hata kidogo duh . tangu tuachane singida DSA mpaka leo sura umbo lile lile. au ndo ma herbal(kiti moto) ya kijapan?
ReplyDeleteDah huyo jamaa wa kushoto amekuwa kama mjapani kwa pozi lake,manake anaonekana ukimzingua tu anakupa mbili za kidevu na moja ya mbavu then unatulia kimyaaa!
ReplyDeleteNI RASHID NJENGA SI RAJABU, JAMAA TULIKUWA NAYE NBC MAKAO MAKUU NA PIA IFM, JAMAA NI KICHWA KWELI, ALIKUJA KWA MASTER IN BUSINESS ADMINISTRATION-MBA STUDIES HAPA LONDON-UK KUANZIA MWAKA JANA NA AMEMALIZA MWAKA HUU WITH FLYING COLOURS.
ReplyDeleteMkuu Michuzi.. Tunaomba Habari za Mtikila... imekuwaje tena??
ReplyDeleteTumezisikia juu juu tu kwenye intaneti..
Tupe nyeti zaidi braza.
Wewe anon. wa pili, nani kakwambia kuwa hawana kazi? ushamba si mzigo na kila mtu anao. Hata wewe unao wako!
ReplyDeleteAnony wa Aug 2, 10:39, yaani nimecheka sana na karate kid wako. Mbili za kidevu na moja ya mbavu kama Bruce Lee katika Enter the Dragon enzi za Empire Cinema,hahahahahhahahahahaha.
ReplyDeleteMdau wa Japan ninayemaindi muda wangu.