Naibu Waziri wa Viwanda, biashara na Masoko Dk. Cyril Chami akimpa zawadi yake Mdau Victor mara baada ya kushinda mchezo wa bahati nasibu uliochezeshwa katika uzinduzi huo jioni ya leo,ambapo watu kadhaa walijinyakulia zawadi hizo za vikiwemo viatu mbalimbali vya usalama..
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Viwanda, biashara na Masoko Dk. Cyril Chami akifafanua jambo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa bidhaa za kampuni ya Beier Safety Footwear ya Afrika Kusini ikishirikiana na kampuni ya Open Sanit ya Tanzania jioni ya leo ndani ya hoteli ya Sea Cliff jijini Dar.Mh Chami alisema kuwa kiwanda hiki ni moja ya kiwanda ambacho kinachangia kuleta amani na utulivu nchini,kwa maana ya kwamba kinatoa ajira kwa vijana wengi wa hapa nchini, aidha ameongeza na kusema kuwa Serikali ya Tanzania haitasita kuunga mkono idara kama hizi za kuwavuta watu mbalimbali kuja kuwekeza.Picha zaidi Bofya Hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...