KWA NIABA YA FAMILIA YA MAREHEMU BWANA NA BIBI MWAKALASI YA KIJITONYAMA, BW RODRICK MWAMBENE NA BI JULIETH MWAKALASI WANAWATANGAZIA NDUGU NA JAMAA KUWA NDUGU YAO MPENDWA, EDWIN MBONELA MWAKALASI ALIYEKUWA ANASOMA NCHINI INDIA KATIKA CHUO CHA ACHARYA BANGALORE AMEFARIKI AGOSTI 21 BAADA YA KUUGUA KWA MUDA MFUPI.

MWILI WA MAREHEMU UMEKWISHA WASILI NCHINI NA IBADA YA KUMUOMBEA ITAFANYIKA NYUMBANI KWAO, KIJITONYAMA (KARIBU NA SHULE YA MSINGI KIJITONYAMA) NA BAADAYE MAZISHI KUFANYIKA KATIKA MAKABURI YA KINONDONI ENEO LA MWEMBENI 25 .8.2010 SAA 10.00 ALASIRI.

PIA IBADA YA HESHIMA ZA MWISHO ZITATOLEWA KUANZIA SAA 6.00 MCHANA HAPO HAPO NYUMBANI KWAO.

KWA NIABA YA FAMILIA YA WA WAFIWA, TUNAPENDA KUTOA SHUKRANI ZA DHATI KWA WAFUATAO AMBAO WALIJITAHIDI KUOKOA MAISHA YA MAREHEMU KWA UPANDE WA MATIBABU MPAKA KUSAFIRISHA MWILI WAKE KUJA TANZANIA.

SHUKRANI ZA HIZO ZIENDE KWA:-
UBALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA KUPITIA KWA AFISA WAKE BW. MWAMANENGE AMBAYE PIA NI MSHAURI WA WANAFUNZI WA TANZANIA NCHINI HUMO, TANZANIA STUDENT ASSOCIATION OF ACHARYA (TASAA) CHINI YA MWENYEKITI WAKE BW. HAMIS FUPI, TANZANIA STUDENT ASSOCIATION OF MYSORE (TASAM), KAMPUNI ILIYOSAFIRISHA MWILI, KUMAR AMBULANCE CO. & INTERNATIONAL, RAMAYA HOSPITAL NA NRR HOSPITAL ZOTE ZA BANGALORE.

BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA, JINA LA MBWANA LIHIMIDIWE, AMEN.

KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA BW RODRICK MWAMBENE KWA SIMU NAMBA 0754 362901, 0713 362901.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Poleni sana wafiwa nafahamu ni jinsi gani inavyouma kupoteza ndugu aliyembali, na pia natoa wito kwa Watanzania tulioko huku India tuzidishe ushikamano.

    ReplyDelete
  2. Rest In peace Edwin tutakukumbuka sanaa, Jina la bwana lihimidiwe

    ReplyDelete
  3. masikitiko yangu na yetu inaonesha jinsi gani edwin alivokua mtu wa watu,,,ama hakika pengo lake halitozibika.mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi,sote tu njiani kuja! amen...pole sana dada julieth.

    ReplyDelete
  4. R.I.P Edwin May god rest you in Eternal Peace Amen!!!

    ReplyDelete
  5. pole sana Kaka Rodrick kwa kujitoa kuhakikisha mwili umerudi salam Tanzania....sisi vijana wa india hasa hyderabad tutakukumbuka daima kwa mchango wako wa kutupatia jezi za timu ya Taifa Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...