Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hongera sana Makongoro Nyerere-I admire your initiative and I admire Mwalimu Nyerere's upbringing of his children very much.

    Nashangaa sana viongozi wa CCM walio wengi Tanzania. Kumekuwa na tabia au kama mashindano vile ya kuwasupport watoto wao kuingia katika siasa na kuwapigia debe washike nyadhfa mbali mbali aidha katika UVCCM au katika kugombania ubunge.
    Hii Political inheritance ni intimidation of the people of Tanzania.

    Kwanini family line iendeleze siasa kana kwamba hamna kingine cha kufanya au kana kwamba Watanzania ni wajinga hawajui kushiriki? Automatically, kumweka mtoto wa mkubwa fulani kunawavunja nguvu wapinzani wenye nafasi nzuri kugombea.
    Wanachosahau ni kwamba kichowashape na kuwashawishi wazazi waliowahi kuongoza siyo kinachowashawishi hawa vijana kuingia katika madaraka. Inaonekana wanasukumwa na kuna kampango. Wanajaribu kuclone maisha ya wazazi wao? Au ni njia nyingine ya wazazi wao kuendeleza madaraka yao kupitia kwa watoto wao mara washikapo madaraka?
    Nina imani kuna strings nyingi attached na inabidi watanzania tuamke tujitambue?

    Naona majina kama Makamba, Lusinde, Pinda, Malecela,Warioba, Msuya, Ngombale mwiru n.k nadhani hii siyo demokrasia ni Political inheritance for intimidation purposes. Hiyo nafasi ya speech writing ya January makamba ingetangazwa magazetini nina imani wapo watanzania wengi tu wangeweza lakini inaonekana wapo wanaochaguliwa na kuandaliwa.

    Familia ya Mwalimu Nyerere imejiheshimu kwa kuwa humble na kushiri katika nyanja zingine za maendeleo. Leo hii mtoto yeyote wa aliyekuwa mkubwa hata kama mtoto huyo akiwa na tabia mbaya anaweza kuwa mbunge na kutumia mabavu kwa kuwa ana support system ya wazee wake? Watanzania tunatakiwa tuwe jasiri na tusiache kugombea hizo nafasi baadae la sivyo kutakuwa na utawala wa kujuana na tusilalamike kwani tutakuwa tumeilea.

    Michuzi kama kweli uko balanced in writing your perspectives please share this on your blog.

    ReplyDelete
  2. Viongozi wetu wanaonekana wameshamsahau Mwalimu Nyerere. Hongera Makongoro kwa kudhihirisha kwamba siyo lazima ukiwa mtoto wa Rais, Waziri au mbunge eti nawe ufuate nyayo hizo. Passion yako katika maisha inaonesha matunda ya malezi mema uliyopea maishani. Kuna mengine mengi mazuri ya kufanya na yote inategemea malezi mazuri na tabia nzuri ambazo nyie watoto wa Nyerere mliamua kuwa.

    ReplyDelete
  3. Wadau mlionitangulia kuchangia, maoni yenu nimeyapenda sana, kwasababu ni ya kujenga. Watoto wa Nyerere wameishi maisha ya kawaida kabisa,maisha ambayo mtanzania mwingine yeyote angeyaishi.

    Unategemea watoto wa vigogo washindwe kwenye kinyanganyiro cha kugombea ubunge? la hasha. Kwanza elimu yao ni ya hali ya juu na pia wanafanya kazi serikalini kwenye nafasi nzuri. Mfano mtoto Makamba anafanya kazi Ikulu na mtoto wa Pinda Ofisi ya rais. Mambo kama haya yalikuwa ni vigumu kupenyeza wakati wa utawala wa baba wa taifa, Mwl. Julius Nyerere. Lakini mungu yupo kwani nani alitegemea vigogo wakongwe ndani ya CCM wamepigwa chini leo hii. Taratibu tutafika, kinachotakiwa hasa ni elimu ya urai kwa watanzania.

    ReplyDelete
  4. Malkiory, watoto wakijaliwa na mentors wazuri walioelimika halafu kamaunavyosema watoto wakasoma wakajituma na kuacquire elimu ya hali ya juu, rudini nyumbani kazi kwenu kazi kwenu. Mwenda kwao. .

    ReplyDelete
  5. Wadau huyu ni Madaraka sio Makongo.

    ReplyDelete
  6. ndio hayo hayo, mwalimu nyerere alilea wanae vizuri, yeye mwenyewe hakupenda madaraka na hakupenda kujiweka juu na watoto wake vivyo hivyo. ndio maana wadau wanamjua makongoro nyerere zaidi ya madaraka. Jamani kuna Madara (kama mnavyomuona na mnavyomsikia kwenye video) na pia kuna rosemary nyerere kati ya baadhi ya watoto wa nyerere

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...