Katika uchunguzi huo wa wanafunzi 180, karibu ama zaidi ya nusu yao, walibainika kuwa na matatizo ya mashimo katika meno na kushauriwa kwa yale meno ambayo bado ni ya utotoni yataondolewa na ambayo tayari yamekoma itafutwe tiba katika hospitali ya kuu ya serikali mkoani Arusha ya Mount Meru.
Kadhalika madaktari hao wanaunzi walitoa mafunzo ya upigaji wa mswaki na kutoa miswaki na dawa bure kwa wanafunzi hao ambao katika zoezi hilo waliandamana na wazazi wao.
Picha na habari na Novatus makunga
vipimo vya meno vya mwanae
Sisi ndiyo kichwa cha mwendawazimu na kufanywa kama specimen za kufanyia field kwa wanafunzi wao kuona kama wamequalify. Wanajua hakuna risk ya litigation kama huko kwao. maana huko kila kitu ni mahakamani tu, ukimuokoa mtu aliyepata ajali na gari linaanza kuwaka na bahati mbaya wakati wa kumvuta akachubuka baadae akadevelop complecations kwenye mchubuko anakushitaki umlipe fidia kwa kumsababishia kilema cha maisha.
ReplyDeleteWacha watufanye guinea piggy lakini just jiulize wewe check up ya meno ukiwa bongo ulifanyiwa lini? mtoto wangu just turned 3 yrs old na ameshamwona dentist mara mbili. Haya meno yataoza saa ngapi? Kwetu kumwona denstisty ni mpaka uwe unakwenda kutolewa jino..
ReplyDelete