Mama Salma Kikwete

NA MWANDISHI MAALUM, RUFIJI

WANAWAKE wanaokopa kutoka taasisi za fedha, wamekumbushwa kuzingatia masharti ya mikopo ikiwa ni pamoja na kuirejesha kwa wakati kuwezesha wengine kutumia fursa hiyo.
Akizungumza na kina mama wa wilaya za Mkuranga, Bagamoyo na Rufiji, mkoani Pwani, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete, alisema kukopa fedha na kutozirejesha ni kukwamisha jitihada za wengine ambao nao wanazitaka kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.Mama Salma alisema kwamba, mtu anapokopa fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi, ahakikishe anazitumia kwa kazi hiyo na sio vinginevyo.

"Kina mama wenzangu, mkopo ni mkopo, lengo lilokufanya uchukue mkopo ni mradi wa kujiletea maendeleo, usitumie fedha za mkopo kununua doti za khanga, huko ni kujisababishia matatizo bila sababu za msingi," alisema.

Alifafanua kwamba, serikali ya awamu ya nne ilipoingia madarakani ilikuwa na kauli mbiu ya maisha bora kwa kila Mtanzania, na fursa ya kupata mikopo, inalenga katika kuwezesha kauli mbiu hiyo kutekelezeka.

Mama Salma aliwasisitizia wanawake kuendelea kujiunga na vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS) na VICOBA, ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kupata fedha za mikopo kwa ajili ya kuendeleza na kuanzisha miradi ya uzalishaji mali.

Kuhusu elimu, alisema mataifa yote yaliyoendelea, yamewekeza katika elimu ya watoto wao ndiyo maana serikali chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete katika miaka mitano yakuwepo madarakani, iliamua kujenga shule nyingi za sekondari na kupanua elimu ya vyuo na vyuo vikuu.
Huku akiwaomba kina mama hao kumpigia kura mgombea urais wa CCM Rais Jakaya Kikwete na wagombea wa ubunge na udiwani wa chama hicho katika uchaguzi mkuu ulipangwa kufanyika Oktoba 31, mwaka huu, Mama Salma alisema miaka ya sasa siyo ya kupuuzia elimu.

"Nchi yoyote yenye mafanikio imewekeza vyema katika elimu ya watoto wao, nasi hatuwezi kubaki nyuma katika hilo, shule nyingi tumejenga kwa nguvu zetu na msaada wa serikali, lakini pia tunakabiliwa na changamoto nyingi kuziwezesha kuwa bora zaidi," alisema."Mkikichagua tena Chama Cha Mapinduzi kitafanya kazi hiyo kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi," alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Punguza vyakula vyenye nafuta mengi. Unahitaji kufanya GYM mke wa Raisi anatakiwa kuwa na mwili mdogo. Hata kama ni hela za bure za kifisadi ni lazima upunguze huo mwili umezidi kuwa kibongo, kiasi kwamba shingo imekaribia kuungana na kifua. Iga mfano mzuri kwa Mama Obama na Laura Bush na wengineo wengi tu.

    Hata kama mtanibania comment yangu lakini ukweli ndo huu.

    Mdau New York- USA




    Mdau

    ReplyDelete
  2. Huyu mama anafaa kuwa Rais baada ya JK kumaliza kipindi chake cha pili.

    ReplyDelete
  3. We kweli ni mdau wa kutoka US eti unahitaji kufanya GYM, ndio nini hiyo GYM inayotakiwa kufanywa.

    Wacha chuki zisizo na kichwa wala miguu eti mafuta wakati hao wamarekani wenyewe wanatisha kwa obesity kama ni mshauri kweli anza kujishauri mwenyewe na majirani zako wanaokuzunguka kwa kula kula. Marekani inajulikana dunia nzima kwa kula hovyo hovyo.

    Halafu ushamba na ulimbukeni mwingine bwana, malimbukeni utayajua tu, kwani huwezi kutoa maoni mpaka useme "Mdau New York, US" ndio nini sasa? Inaonyesha maishani mwako hukutegemea kama kuna siku utafika au utaishi huko kwa hiyo ni bora uje utukoge na hiyo NY yako sikazi unaishi Queensland au Harlem!

    Mdau Mbagala Charambe

    ReplyDelete
  4. mdau New York-USA kama ulikua hauna cha ku comment ungekaa kimya tu, ndio nini sasa. kwani kunenepa kwake kunakuhusu nini, kwanza inaonyesha jinsi gani hauna heshima.Eti kama mamam Obama, so wake za maraisi wote wawe kama mama Obama, kwanini? coz kila mtu ana helth status yake, anachokula mama Obama inawezekana wengine kinawadhuru, au hawapendi, au mazoezi hayawasaidii, ooh plz!!

    mdau- washington DC

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...