Kaka Michuzi,
NAOMBA WADAU WASHAURI; KUHUSU HII DOCUMENT KWA KUZINGATIA KASHFA KADHAA ZINAZOIKABILI MANISPAA HII KATIKA MASWALA YA ARDHI.

JAMAA WAMETOA “ CONSULTANCY “ KWA KAMPUNI BINAFSI KUFANYA SURVEY ILI BAADAE WAWEZE KUKUSANYA FEDHA ZA MAJENGO KAMA “WARAKA” UNAVYOSEMEKA, JE, KUNA UHAKIKA KIASI GANI KWAMBA “WARAKA HUU” NI HALALI KUFANYA ZOEZI HILO?

WALIPOFIKA KWANGU PAMOJA NA UZALENDO JUU YA NNJI YANGU NIMESITA KWARUHUSU MANAKE WANAPIGA HADI PICHA NA KUCHUKUA VIPIMO VYA NYUMBA NA VYUMBA VYAKE.
MDAU


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hata mimi nisingekuwa na imani na kumruhusu mtu aingie chumbani eti kwa vile ana barua inayoonekana kama ni rasmi. Siku zote huwa wanatangaza habari kama hizi kwenye vyombo mbalimbali vya habari kabla ya kuanza kupitapita. Wanaweza kuwa watu wanasavei nini wakombe bure.

    ReplyDelete
  2. Duh, sheria gani inayoruhusu mtu apige picha vyumba ya nyumba ili athaminishe, huu ni wizi mtupu, na hata hiyo barua haina sahihi ya huyo anayejiita "MWAMINIFU", mie sikubali waje kupiga picha nyumba na vyumba huo ni kuingilia mambo binafsi, mi nijuavyo mtu kuingia ndani ya nyumba sharti awe na order maalum ya korti na kwasababu maalum. hizo taarifa ndizo zitakatumiwa na majambazi kujua nini kimo ndani...Duh Bongo NUKSI

    ReplyDelete
  3. Pamoja na uhalali wa kituko kama hicho kisheria (kama kweli), kama watu wanaweza kutengeneza fedha feki, watashindwa kutengeneza ducument/vitambulisho Bandia? Usalama wetu na mali zetu unahakikishwa vipi?

    ReplyDelete
  4. HANA HAJA YA MTU KUINGIA NDANI KWANI RAMANI YA NYUMBA INATOSHA KUTADHIMINI JENGO MPATIE RAMANI ATAISOMA NA KUFANYA MAHESABU YAKE HAPO HAPO NA AKURUDISHIE HAPO HAPO ASIONDOKE NAYO KWANZA NI WIZI MTUPU TAARIFA ZA NYUMBA ZOTE WANAZO OFISINI KWAO

    ReplyDelete
  5. MImi siamini hiyo barua. Mbona haina muhuri hata mimi sinaweza kutoa copy nikapeta nayo tu..Ulifanya vizuri...Kama wako serious waweke barua zenye mihuri yao.

    ReplyDelete
  6. TANZANIA OYEEEEEEEEEEE! NCHI HAINA MWENYEWE! NJOONI HUKU WAJAMENIIIIIII NYUMBA UTAPATA BURE ZA KUMWAGA. NUNUA NYUMBA KWA KUANGALIA PICHA NA MAELEZO YA MAWAKALA.BONGO TAMBARAREEEEEEEEEEEEE

    ReplyDelete
  7. TUMELALA SANA SASA WANATAKA KUPIMA HADI VITANDA VYA MASTER BEDROOM ILI WAKADILIE KODI, CCM OYEEEEE. MTAANI KWANGU JIJI HALIJAWAHI KUKANYAGA KWA MATENGENEZO YA AINA YOYOTE ILE KWA ZAIDI YA MIAKA ISHIRINI NA TANO LICHA YA MTAA HUU KUWA ENEO LA KATIKATI YA JIJI! LAMI ILIKWISHA BOMOKA ZAIDI YA MIAKA ISHIRINI SASA HAKUNA DALILI YA KUWA ILIKUWEPO, TAA ZA MITAANI NAZO ZILIZIMA MIKADA MINGI TUU ILIYOPITA SASA NI WAKATI NWA KUWAKABA ILI WATUELEZE KODI TUNAZOLIPA USWAZI ZINAKWENDA WAPI, SIJUI KAMA WATANZANIA TUNAWEZA KUWAKABA KAWANI TUMELELE SANA.

    ReplyDelete
  8. Barua ikishakuwa na nembo haina haja ya kuwa na muhuri, kwa kifupi ni kuwa hiyo nembo si rasmi kwani inaonekana thahiri ni ya kuforge na barua haina sahii ya mhusika na huko chini ilitakiwa isainiwe tu kwa tite ya kny: mkurugenzi wa manispaa kwani watumishi wote wa manispaa wanafanya kazi kwa niaba ya mkurugenzi wao, kama ilivyo kwa watumishi wote wa wizara wanafanya kazi kwa niaba ya katibu mkuu wao. Pia barua hiyo inaonekana haikupangiliwa kuandikwa . Kwa jinsi hiyo unatakiwa kutoruhusu watu kama hawa kuingia ndani kwako.
    Mdau M.A

    ReplyDelete
  9. Watanzania tena watu wa Dar es salaam mnasikitisha kimataifa kwamba hamfahamu kwamba uthaminishaji ni taaluma kubwa sana kama taaluma nyingine. Waacheni wafanye kazi yao acheni kujitetea kodi ni muhimu lazima mlipe ili inchi iendelee mnapenda kudekezwa kujifanya mnajua wajanja wakati ni nchi yenu inakuwa maskini. Wenzetu wameendelea kwa sababu ya kulipa kodi na kuipenda nchi yao sasa ninyi kitu kidogo tu siasa. Mmoja anaogopa majambazi watamvamia kwa taarifa yako jambazi hategemei picha wala nini akiamua ameamua, pia kwa taarifa yenu vijana wanaofanya kazi hiyo ni wasomi kutoka Ardhi University wamebobea katika maswala ya uthamini. Acheni siasa kwenye maendeleo lipeni kodi watanzania mnadekezwa sana

    ReplyDelete
  10. weye hapo juu inaelekea umekaa uko ughaibuni mda mrefu bongo wasanii wengi sana tunaogopa kuibiwa,,kama kweli wanafanya kazi hiyo kihalalai waje na polisi mwenye kitambulisho basi ili tuiibiwa tujue wapi pa kuanzia..toka lini upimaji wa nyumba unahusisha kupiga picha makabati na vitanda eeh??

    ReplyDelete
  11. MARUFUKU NASEMA
    WEZI HAO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...