MAREHEMU
SEIF RAMADHAN ATHUMAN

JUMUIYA YA WATANZANIA UNITED ARAB EMIRATES INATOA POLE KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WA MAREHEMU NDUGU YETU BW. SEIF RAMADHAN ATHUMAN MKAZI WA ILALA QUARTERS DAR ES SALAAM ALIYEFARIKI TAREHE 6 AGOSTI 2010 NA KUZIKWA TAREHE 19 AGOSTI 2010 BAADA YA SWALA AL ASR KWENYE MAKABURI YA AL QUOZ, DUBAI UAE BAADA YA KUKAMILIKA KWA TARATIBU ZA KISERIKALI NA KUPATIKANA MWILI WA MAREHEMU
JUMUIYA INAWASHUKURU NDUGU WA MAREHEMU WALIOKO NYUMBANI TANZANIA NA WATANZANIA WOTE WA UAE KWA MSHIKAMANO TULIOKUWANAO KATIKA KIPINDI KIGUMU WAKATI WA KUSHUGHULIKIA TARATIBU ZA KISERIKALI, SHUKRAN ZA PEKEE ZIENDE KWA:
• NDUGU WA MAREHEMU KWA IDHINI ZAO
• CONSUL GENERAL WA TANZANIA KWENYE FALME ZA DUBAI NA UAE KASKAZINI BW. ALI AHMED SALEH KWA KUIWEZESHA JUMUIYA KIITIFAKI KWENYE SERIKALI YA DUBAI
• BW. RASHID ABEID SUBHA KWA WAKATI NA JITIHADA ZAKE KWENYE KUFANIKISHA MAZISHI YA NDUGU YETU

MOHAMED SHARIFF
MWENYEKITI JUMUIYA YA WATANZANIA UAE

WAKATI WA KUSUBIRI SWALA YA AL ASR NA KUMSWALIA MAREHEMU WAKATI WA KUMDINDIKIZA MWENZETU SHEIKH MUHIDIN BIN ABDULRAHMAN (ALIYEKETI) AKIONGOZA MAZISHI


















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. inshaalah mwenyezi mungu amsamehe madhambi yake na amuweke mahali pema peponi aminnnn na mwenyeezi mungu awape subra familia yake amin.

    ReplyDelete
  2. INNA LILLAHI WA INNA ILLAIHI RAJI'UN

    ReplyDelete
  3. Ahaa. Kumbe Ramadhani Bhutto uko Dubai. Salama lekhu Shehe?

    ReplyDelete
  4. Inna lillah. Sheikh Muhiddin nakukubali sisi katika twalika ya Sheikh unatu wakilisha vema huko ughaibuni

    ReplyDelete
  5. wewe anonymous wa august 20, 05:48:00 AM, salama lekhu ndio nini? hebu kamuone daktari wa masikio maana inaonyesha unasikia maneno kivyengine vyengine. watu wanasema Assalam alaykum, Salam alaykum!

    ReplyDelete
  6. Wewe Anonym wa Tarehe Fri Aug 20, 06:35:00 PM pia inabidi ukamwone daktari wa fikra!!!

    Uliyemrekebisha yuko karibu sana na usahihi kuliko wewe ambaye 'huelewi kabisa'. Usahihi ni kuwa ilibidi aseme 'As salaam aleik', kwani anamsalimia (au anam-address) mtu mmoja. Ngeli hiyo mwanangu, hihii hii, hehe heeee!

    As salaam aleykoum (aleikoum) inatumika kwa watu wengi, lakini ni salamu ile ile. Mfano mwingine ni neno 'marhababik', yaani 'karibu' ukiwa unamkariisha mtu mmoja! Kama unawakaribisha watu wengi unatakiwa kusema 'marhababikoum'! Ngeli tena hiyo, teh hee tehee he heheee!

    Chiaz Mchiiz (ngeli linapanda kudadeek, te he heee!)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...