
Registered Voters - 407,669Valid Votes - 266,064
Invalid Votes - 8,309
Total Turn Out - 274,373
Percent Turn Out - 67.00%
Polling Stations Published 1,210 of 1,292
NDIO / YES = 175,476
HAPANA / NO = 90,588
Kura za maoni katika Visiwa vya Zanzibar yanafanya kuwapo na muundo mpya wa serikali katika viswa hivyo baada ya uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa na idara ya Maelezo Zanzibar zinaonyesha kwamba asilimia 66.4 ya Wananchi waliopiga kura wameridhia serikali ya mseto, yaani Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar baada ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu.
Matokeo hayo sasa yanaashiria kuzikwa kwa mfumo wa “Westminster” wa anayeshinda kuunda Serikali kwa kuchukua kila kitu, sasa kazi iliyobaki ni kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitisha mabadiliko ya Katiba Agosti 9 mwaka huu ili kuwapo kikatiba mfumo mpya wa muundo wa Serikali ya Zanzibar.
Akitangaza matokeo hayo jana, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Khatib Mwinchande alisema waliochagua ndio wameshinda kwa kura 188,705 ikiwa ni sawa na asilimia 66.4 wakati waliochagua hapana wamepata kura 95,613 ikiwa sawa na asilimia 33.6. Mwenyekiti huyo alisema idadi ya kura zote ni 293,339 sawa na asilimia 71 wakati waliojiandikisha ni 407,669.
Kisiwani Pemba wananchi wengi wa huko wamechagua ndio wakati Mkoa wa ya Kusini Unguja kuna idadi kubwa ya watu waliochagua hapana.21,394 sawa na asilimia 66.3 waliochagua ndio 10,864 sawa na asilimia 33.7 katika Mkoa huo, kura zilizoharibika ni 934 ikiwa ni asilimia 2.8%. kura zote ni 33,192 ikiwa sawa na asilimia 69.1.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi(CUF) Seif Shariff Hamad alisema “Nimefurahishwa namatokeo ya kura ya maoni zilizopigwa na wananchi wa Zanzibar, ni matokeo yao yanayoonesha hisia za demokrasia”
Taarifa nyingine toka mitaani zinasema kuwa majimbo yaliyoshikilia kura ya HAPANA ni Amani, Chaani, Chwaka, Dole, Kwahani, Makunduchi, Muyuni na Uzini.


Hayo ni majimbo ya chama kipi ili tujuwe nani wachawi?
ReplyDeleteZANZIBAR INA POPULATION YA 1.1 MILION. HII NI KUSEMA KUWA KWA TAWKIMU HIZO ZADI YA NUSU YA WAZNZ HAWAKUSHIRIKI KUPIGA KURA KWA NAMNA MOJA AU NYENGINE. KWA HIYO MATOKEO HAYO BADO HAYANA MAANA KWA KUWA HAWAWAKILISHI HALI HALISI YA ZNZ.
ReplyDeleteKWA HIYO SI SAHIHI KUSEMA KUWA KURA HIYO ITAONDOA MIVUTANO NA SIASA ZA CHUKI KILA BAADA YA UCHAGUZI. TUTEGEMEE HALI KUENDELEA ZAIDI NA ZAIDI.
WATU WENGI HAWAKUJITOKEZA KWA KUONA KUWA MAAMUZI YALISHAFANYWA NA HIYO ILIKUWA NI UBABAISHAJI TU.
ANKAL TUNAOMBA PIA ORODHA YA MAJINA YA WALIOPITA KUGOMBEA UBUNGE MAJIMBONI KUPITIA CCM.
ReplyDeletewaliojiandikisha ni laki 4 na waliopiga kura ni laki 260,.bado kuna utata,.tusishabikie coz si mawazo ya wengi, tujiulize kwanini wengi hawakujitokeza kupiga kura?
ReplyDeleteAfrika hii tangu mtindo wa serikali za shirikisho zianze nchi gani imefanikiwa? Zimbabwe naona vurugu tu, Kenya vilevile...nwei..ndo kutafutiana KULA uko, MAPINDUZIIIIIIIIIIIIIIII
Kila mmoja alikuwa na haki ya kupiga kura, na wote walijua kama kuna kitu kinaitwa kura za maoni. sasa kama hawakujitokeza kwenda kupiga kura basi ni tatizo lao wenyewe nawasitafute mchawi.
ReplyDeleteBinafsi ni Mbara, lakini nawapongeza sana wazanzibari kwa hatua walofikia, adhabu ya kaburi anaijua MAiti , kwa kuwa ADHA ya wazanzibari wanaijua wao wenyewe na sio sisi wabara. kwahiyo tunawaombea sana kuwa muwafaka walofikia uwe ni sahihi na ulete kweli maendeleo ya Zanzibari na wazanzibari woote yaani waunguja na wapemba na kamwe pasitokee kukosa uadilifu baina ya pande mbili ili kuleta amani na utulivu katika visiwa hivyo. Mungu ibariki Zanzibar Mungu ibariki TAnganyika....na watu wake
niulize tu
ReplyDeletebendera ya zanzibar inamaanisha nini?na ni ya wakati gani?na wimbo wa zanzibar badala ya wimbo wa taifa ina maanisha nini?
nilishawai ulizwa swali na foreigners nikashindwa jibu maana walitaka kujua kama zanzibar si nchi iko ndani ya tanzania inakuweje ina wimbo wake na bendera?na vime-origin wapi?
ofkoz nilizuga kiaina ila nakawaaidi nitawapa jibu
na hizi kura za maoni iyo idadi ya watu vs population mh?!!!
mnijuze
Anonymous wa pili
ReplyDeleteNdiyo population ya Zanzibar ni watu 1.1 milion. Sasa ulitaka mpaka watoto wachanga waende kupiga kura ?
Chekecha bongo kwanza!!
Hao wasiopiga kura ina maana ndio wamekubali matokeo kwa kuwa kama wasingekubali wangeenda kuonesha uamuzi wao -B population kuna watu wanakufa wengine wagonjwa wengine wanasafiri na pia kuna watoto wadogo sasa hao pia unataka wapige kura?Jengine huyo alosema maana ya wimbo wa taifa na bendera yeye na alouliza wote hawana akili -KWANI UK imeundwa na nchi ngapi? na mbona Nothern ireland wana bendera ZAO 2-NA YA TATU NI YA UK-NA pia wana wimbo wao wa taifa hiyo ukiwacha REPUBLIC OF IRELAND-naomba mdau ukasope politics kitu kinachoitwa UNIONIST NA NATIONALISTS usituharibie mazungumzo humu ndani sio. cha kushangaza POUND YA IRELAND AU YA SCOTLAND HAITUMIKI ENGLAND AU UNAPATA TABU NA PIA NI NCHI MOJA.
ReplyDeleteMimi ninachangie kwa kuwambia wachangiaji wanaoponda hii kura ya maoni ya Zanzibar; kuwa hata kama itasaidia angalau kufanyika kwa uchaguzi wa salama na amani na tume kutoa matokeo kwa uadilifu kama ilivyofanya hapa basi itaisaidia sana Zanzibar;
ReplyDeleteBila shaka hatutegemei mabadiliko makubwa hivyo; still we are in Africa; lakini kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu, adhabu ya kaburi aijuae maiti! Wazanzibar tumechoka na mateso ya miaka nenda miaka rudi ya siasa za chuki na fitna na watu kutesana.
Matunda ya mwanzo tu baada ya kufikiwa muwafaka kati ya Rais Karume na Katibu Mkuu Seif basi zimepelekea kufika hapa tulipo; na si pabaya kulinganisha na tulikotoka na bado tunategemea kusogea pazuri zaidi in near future inshaallah.
UKIACHA MAONI YA KUHUSU MATOKEO YA HII KURA. MIMI NASHINDWA KUELEWA KATIKA SIASA ZA ZANZIBAR HII KURA NI KWA FAIDA YA CCM AU CUF? VIONGOZI WA VYAMA VYOTE WALIKUWA WANATAKA MATOKEO YA NDIYO. KUNA MTU MWENYE MAELEZO YA KUTOSHA KUHUSU JINSI SERIKALI YA MSETO ITAKAVYOUNDWA?
ReplyDeleteKWA MFANO CUF WAKISHINDA UCHAGUZI, NANI ATAKUWA RAIS WA ZANZIBAR, NANI ATAKUWA WAZIRI KIONGOZI NK? MASWALI HAYA WANANCHI WANAJUA MAJIBU?
Mon Aug 02, 11:02:00 AM sasa wewe ndio bwege mtozeni...unapoulizwa kitu jibu kwa ufasaha kama hujui nikate uko...eti unafananisha tanzania na UK una akili wewe?nani ana muungano kama wa tanzania?na kama ndo ivo wafikiri ilikuweje vilitoweka apo katikati na sasa vimerudi???tatizo umezoea madesa ya prof wako ya kufaulia mitihani afu unasimama apa na pointelss zako
ReplyDeletefikiri kabla hujajibu
Wenzetu Wazenji ni vituko vitupu... yaani kura 8,300 zote kuharibika maana yake nini? mjione mlivyo wa ajabu ajabu.
ReplyDeleteSijui lini mtabadilika. Mkielezwa mnajifanya kuja juu. Haya tuone kama ndio mtaweza "kupara miwa" ... tunasubiri mabadiliko kwa hiyo katiba mnayoitaka.
michu naomba nimjibu huyo anosema TUSIFANANISHE TANZANIA na UK.sasa kwani UK watu wake wana miguu mitatu mitatu? PILI-anashangaa nini kuwa na bendera huyo alitembea jamani,NENDA SPAIN HAPO-WAKATALUNIA WANA BENDERA YAO-VALENCIA NA MAJIMBO MENGINE NA NI NCHI MOJA,vipi USA sio MUUNGANO? MBONA KILA JIMBO LINA BENDERA AU KWA KUWA HAKUNA KITU KINAITWA REPUBLIC? MAANA YA REPUBLIC NI HII:A republic is a form of government in which at least a part of its people have some element of formal control over its government,Most often a republic is a sovereign country" SASA ANATAKA NINI CHENGINE.UAE NI MUUNGANO WA NCI ZA KIARABU N AZO TE HIZO ZINA BENDERA NAOMBA MICHUZI UIWEKE APATE ELIMU.MUUNGANO SI UADUI JAMANI NI USTAARABU WA KUKAA PAMOJA
ReplyDelete