NIMEFANIKIWA KUWA MGOMBEA WA KITI CHA UBUNGE WA JIMBO LA KINONDONI, DAR-ES-SALAAM KUPITIA TIKETI YA CHADEMA.


NILIZALIWA WILAYANI KINONDONI, NIKASOMA CHUO KIKUU CHA DAR-ES-SALAAM, NIMEJENGA WILAYANI KINONDONI NA NAISHI WILAYANI KINONDONI PIA.

BOFYA HAPA

KUENDELEA NA HABARI HII

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Philip, unasatahili kushinda! Umejieleza vizuri, unauzoefu wa kutosha na itakuwa aibu kubwa kwako, familia na chama kama ukishinda na kushindwa kubadilisha kinondoni! Mapato ya manispaa ni makubwa na inashangaza hakuna mengi ya maendeleo yanayofanyika, kero nyingi zipo kama uuzwaji wa viwanja vya wazi, uchafu uliokithiri, huduma mbovu ktk hosipitali kama mwananyamala,n.k vyote hivi vinahitaji MPAMBANAJI SHUPAVU asiyeona haya wala kuweka mbele maslahi ya chama na vigogo wake, najua watanzania wengi tunachagua chama bila kuangalia uwezo wa mtu, U ARE THE RIGHT PERSON FOR KINONDONI!! Mimi naongea haya kwa uchungu wa yale yanayotokea kinondoni na mbunge wao kamwe hakusimama imara kuwatetea wananchi wake bali aliishia kuvaa sare za chama!!

    ReplyDelete
  2. CHADEMA OYEEEE!!

    UMEPATA KURA YANGU!!!

    ReplyDelete
  3. Punguza U mimi!


    NITAZISHUPALIA
    NITAZITATUA

    EVERYTHING OF ABOUT YOU!

    I HAVE DEGREES
    I HAVE COMPANIES.....

    WHAT ABOUT THE PEOPLE?
    WHA ABOUT THE PARTY?
    WHICH PROBLEMS?
    WHAT STRATEGIES?

    ReplyDelete
  4. Bwana umeniangusha kitu kimoja Master ya MIS halafu unatype hii habari yote kwa herufi kubwa? Kwenye IT tunafundishwa kuwa ukiandika kwa herufi kubwa ni kama unashout nadhani unakumbuka hilo.

    Nakutakia mafanikio mema...

    ReplyDelete
  5. Hongera sana bwana Mogendi kwa uamuzi huo. CV yako inatosha kabisa nikupe kura yangu. Tafadhali tunaomba upinzani wa kweli bungeni ili serikali ifanye maamuzi kwa maslahi ya taifa na siyo ya chama.

    ReplyDelete
  6. HUYU JAMAA ANATUFAA WATU WA KINONDONI. TUSIDANGANYIKE NA AHADI HEWA ZA CCM,KAMA TUNATAKA MAENDELEO YA KWELI TUSICHAGUE CHAMA, TUCHAGUE MTU ANAYEWEZA KUTULETEA MAENDELEO.

    ReplyDelete
  7. Sasa taratibu naanza kuona mwanga wa Jimbo la Kinondoni kuondoka kwa "wahuni". Chini ya Idd Azan, sana sana tulichokisikia ni kuuzwa kwa viwanja vya wazi yeye akiwa mmoja wa wahusika wakuu!! Sawa kijana naona nondo zako nimezikubali, lakini je, ni kwa niniunafikiri wewe ni bora zaidi na si mhuni kama Azan...una lipi jipya?

    ReplyDelete
  8. Unaomba KULA na pesa duh! chagua moja..

    ReplyDelete
  9. Jamaa namkubali ana-qualification kali sana.Nimezaliwa wilayani kinondoni,nimesoma wilayani kinondoni,nimejenga wilayani kinondoni,nimeowa wilayani kinondoni,ninafanyakazi wilayani kinondoni,ninalala wilayani kinondoni.Ninapata ulaji wilayani kinondoni,natoa rushwa wilayani kinondoni.Njemba ina sifa kubwa kuliko wapinzani wake waliohamia wilayani kinondoni.Hahahahahaha.

    ReplyDelete
  10. Mume Wangu, Mikanjuni TangaAugust 25, 2010

    Haaaa!!!, kumbe mwenzetu umeshajenga nyumba katika umri huo?? Lazima nawe una chembechemmbe za ufisadi. Unafanya kazi gani, wapi? cheo chako ni kipi?? Una mke? yuko wapi
    ?

    ReplyDelete
  11. Tukuchangie hela sisi ndio tumekutuma ukagombea?? kama huna fedha kwanini usitulize boli? CV kubwa kumbe upo majalala haa haaa, achia ngazi sio lazima wote tuwe wabunge

    ReplyDelete
  12. haaaa!kizuri chajiuza kibaya mtadeal na michuzi tu,unaomba hela si uuze nyumba yako ufanye kampeni!nyie chadema mnanengeneka tu kama mkuu wenu anayerudi jimbo la hai,njaa kali matafanyaje maendeleo na njaa zenu kama sio mtajifaidisha kwanza, CCM OYEEE,IDD AZAN OYEEEE,

    ReplyDelete
  13. Afadhali anayeomba mchango kuliko anayeiba.

    ReplyDelete
  14. Idd MwanakatweAugust 26, 2010

    Philip wacha usanii, huko Kansas umewachangisha hazijatosha tu? Na pia uliwaeleza unaenda kugombea ubunge Tarime, ghafla uko Kinondoni??? Kwa kuwa una uchungu sana na maendeleo ya Taifa letu (Maana we mwenyewe Mmarekani according to reliable sources)uza kampuni au nyumba ufanye kampeni. Unless otherwise go back to the U.S.A. and take care your family. Ushauri wa bure kaka.

    ReplyDelete
  15. Watu wa Dar(Kinondoni) hawako serious, na nina wasi wasi humu kwenye kisemeo cha Ankal kama wako. Katika wabunge wote waliopita ni Derek Brycen anaekumbukwa mpaka leo.....wengine ni uhuni mtupu na uvulana bassss.
    Wakununa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...