Ramadhan Maqbul Issa Michuzi na waislam wote

Juzi nilikuwa kwenye gari jioni baada ya Al-a-Sr. Redioni nadhani ilikuwa ni TBC walikuwa wameweka mawaidha ya Al Marhum Hemed Bin Jumaa Bin Hemed. Lakini kile kipindi kilikuwa only 30 minutes. Sasa nimetembelea websites mbali mbali kama Al Hidaaya na zinginezo sijapata mawaidha by Al Marhum Sheikh Hemed. Je waweza au wasomaji wa blog yako wanaweza kutusaidia links za websites ambazo naweza kusikiliza mawaidha yake huyu...na hasa zinazohusiana na mwezi huu Mtukufu?

Pili , kama kutakuwa na mwenye kujua, je miskiti ipi inatoa Darsa au mawaidha jioni baada ya Alaasiri hapa mjini (central Dar es salaam)

wako katika uislam.
Muslam mwenzio.




wabillahi Taufiq

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. http://ukweli.ning.com/ hapo utapataa mawadha ya mashekh mbali mbali

    ReplyDelete
  2. Tembelea misikiti mikubwa kama Msikiti wa Manyema, Msikiti wa Maamur Upanga, wewe jaribu kwenda kusali Alasiri misikiti tofauti tofauti kisha utajua upi wana darsa za jioni. Wahi ndugu yangu siku zenyewe zimeisha hizi. WAWEZA ULIZA MAIMAM WA HIYO MISIKITI PIA WATAKWAMBIA!

    ReplyDelete
  3. pia tembelea www.tanzil.info usikilize kurani tukufu na tafsiri yake kwa lugha uitakayo, ikiwemo kiswahili...!

    ReplyDelete
  4. Kuna Msikiti wa Rawdha ambao uko mtaa wa Mkunguni, karibu na soko la kisutu. Hapo panakuwa na Darsa baada ya sala za Dhuhri na Asr kila siku.

    Jitahidi uhudhurie tupate kuvuna kwenye mwezi wa Mavuno

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...