mtaa wa aggrey jijini dar kama unavyoonekana leo ambapo kuna nyumba mbili tu za kawaida zimebakia, pamoja na shule ya msingi ya lumumba. nyumba zote sasa ni vikwangua anga kama ilivyo sehemu yote ya kariakoo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. dar-es-salaam is a time bomb...........!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Kwangua anga!! lakini hebu ona huo msongomano hapo chini. Hebu fikiri hiyo adha utakayopambana noyo kama unataka kukatisha toka Lumumba hadi Masimbazi, kwa gari huwezi na kwa miguu kama ukifika mwisho hado simu uanayo umshukuru mola!!!

    ReplyDelete
  3. Tatizo mji hauvutii sababu ya uchafu.

    ReplyDelete
  4. Mdau, BloomsburyAugust 06, 2010

    Hilo trekta nalo linafanya nini katikati ya mji?

    ReplyDelete
  5. kwetu sie tunaoishi hapa hapa bongo hatuoni uchafu wala nini tunapeta tu kana ney yaka bana vikwanguzwa anga no building Quality just quantity tumezoea harufu haitusumbui

    ReplyDelete
  6. Wewe unaesema umezoea uchafu ndio nyie mnaotupa maganda ya machungwa popote. Hata mimi nipo Bongo lakini nakerwa sana na uchafu wa mji. Tubadilike wenyewe kwanza!!

    ReplyDelete
  7. We mdau unaulizia trekta la nini hujui tuko kwenye Kilimo Kwanza?

    ReplyDelete
  8. no city planning, no use of census, decisions made by politicians instead of technocrats....what do you expect? shida tupu nchi ina wataalam lakini wenye maamuzi hawasikilizi manake ni personal benefit ndio inawekwa mbele. MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA, LOL!! sad , we need to change mind set zetu, tuwaze jamii kwanza.bila hivo hatuendelei kamwe!

    ReplyDelete
  9. Halafu hebu fikiri huo ndiyo mtaa ambao anaishi mbunge wa Ilala Mhe Zungu. Pamoja na hayo bado atapigiwa kura. Halafu kuna diwani yule ana asili ya kisomali sijui kama alipeta kwenye kura ya maoni. Yeye mwenyewe alivyo hana tofauti na dampo. Halafu bado naye atapigiwa kura. Very pathetic. Jiji la Dar halihitaji madiwani. Linahitaji kuongzwa na tume ambayo yenye maamuniz ya mwisho. Haki ya nani?

    ReplyDelete
  10. Hizi lawama ni zetu sote watanzania kwa ujumla kwa kushindwa kudumisha usafi wa mazingira katika miji yetu.

    ReplyDelete
  11. hayo maghorofa yana meet design specs au ndio baada ya ya miaka mitanao yanaanz akubomoka kama yale ya kariakoo...home is home though, i wouldnt say any thing against my country ..i love this country to death...

    ReplyDelete
  12. Embu sikizeni!! Hanko hakiona hits zinadumaa basi hubandika mapicha hau newz sinazousu vikwagua hanga! Apo watu watahandika tu, tena sana!

    Hits zikihanza kushuka tena ataweka nyuuz hau hambali za foreni za magali na msogamano balabalani!

    Ameshatusoma na kutuhelewa vema wasomanji wake. Siku izi niuz zimekuwa hadimu.

    Chiaz Mchizi

    ReplyDelete
  13. ...damn-we ANONY wa ''Fri Aug 06, 06:16:00 PM'' ludi CLASS....aiseee!!

    ReplyDelete
  14. Michuzi umekumbuka ulipokulia mtaani kwako. kama sijakosea kwenu ilikuwa nyumba ya tatu au ya pili kutoka shule ya msingi ya Lumumba kushoto. tafuta picha basi za kaka zako kina Chamenya na Melaboni uziweke.

    ReplyDelete
  15. kila anayejenga gorofa atenge na fllor moja ya parking, ni ushauri tu

    ReplyDelete
  16. Vkwangua anga ndiyo majengo marefu? kama ndiyo maana yake mimi nitasema ni msemo wa watu wasio jua maana ya ke kwani majego marefu katika majiji , miji yote duniani lazima yawe tall building policy jiji mnayo? jibu hakuna basi hizvi ni vikaribisha vifo, je wenye majengo na design team wanafuata code of practice from feasibility to completion? jibu hapana, je kuna pre-construction information za majengo haya? jibu hapana, sasa utaratibu wa mchoraji na materials ya kutumika kutokana na mazingira/ material yapi yatumike ili aliangaliwi sasa ni vipi planning application wanapewa hawa wajenzi na wenye majengo? jibu ni rushwa, hili tumeliona jengo moja lilipoporomoka na kuua hili lilimtoa Waziri mkuu kipindi hicho Edward Lowasa kwenda na kutoa amri pale ya mwenye jengo kukamatwa, mimi nilifikira hiyo sio kazi ya waziri mkuu, pale watu wote pale jiji waliohusika walitakiwa kufukuzwa kazi, na ingekuwa kuanzisha taasisi ya health and safety in construction labda ikiwa chini ya mtu kama profesa Sunga kilonde hii ingetoa mwongoza nini kinatakiwa kabla mtu ajaanza kikwangua vifo.Ushauri serikali ya Tanzania watumieni wataalamu waliopo, kwanini hamtaki kumtumia kilonde kwenye matatizo ya ardhi na ujenzi? wazungu wanamtumia huyu mzee, sasa serikali hamtaki au mpaka siku akitangaza nia?
    MDAU UK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...