Bw. Frederick Mwakalebela akiongea na waandishi

Na Francis Godwin
Mbele wa katibu wa CCM mkoa na waandishi wa habari mgombea nafasi ya ubunge Iringa mjini aliyeenguliwa Frederick Mwakalebela amekubali yaishe na kuwa hajashawishiwa na mtu yeyote wala hajapokea fedha yoyote ili kuyakubali matokeo hayo ila ni heshima yake kwa CCM na kuwa hana mpango wa kuhama chama.

“Ndugu zangu kweli nayakubali matokeo ya NEC na kuyaheshimu …mimi sina kinyongo nitaendelea kuwa mwana CCM….ila kuhusu kesi yangu ninaomba nisihukumiwe kabla ya mahakama kunihukumu japo kuna maneno mengi yanasemwa juu yangu kuwa mimi kesi yangu ni mbaya ….

"Naomba tuiachie mahakama sio mtu ama mwana chama mwingine kuhukumu nje ya mahakama mambo mengi yamesemwa dhidi yangu na ndio yaliyonifikisha mahakamani leo ”alisema Mwakalebela huku akiwa mnyonge tofauti na alivyozoeleka.

Alisema kuwa ana amini kuwa bado umri wake ni mdogo hivyo ataendelea kuwepo ndani ya CCM, na pia atetea hatua ya wenzake kutokubali matokeo na kuwa yeye anakubaliana na NEC.
Kwa habari kamili za mahakamani Iringa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. michuzi hizi post kwa sisi tusiofuatilia kwa karibu uchaguzi zinatuzingua...hii post iko very very vague and it does not really make any sense on both michuzi blog na michuzi post
    swali: Huyu jamaa katoa au kapokea hio rushwa? hebu nisimulie mwaya michu

    ReplyDelete
  2. maadamu sisiemu ndio serikali kama ilivyowaona watu wengine hawana hatia chenge, mramba na wengine wengi. basi nashawishika kuwa huyu jamaa ni mharifu asubiri kutumikia kifungo chake. idumu rushwa.

    ReplyDelete
  3. SINA MENGI ZAIDI YA KUSEMA KWAMBA.....HIYO NDIO CCM,UKILETA ZAKO UNAFINYWA CHINI CHINI UNATULIA

    ReplyDelete
  4. bongo tambarale,
    mtaka yote kwa pupa hukosa yote.

    sasa kaka utamisi zile za uwanja wa taifa.

    ila usikonde lazima watakutoa kuuua so.

    Ila kwa jinsi vijiweni wanavyo kusifia ulivyo na sera nzuri , ungetimukia chadema tu, jimbo lilikuwa la kwako.
    UMEKUWA MWOGA kuJITOSA.unapenda urahisi inavyoonekana.

    Dr. Slahaaa, alipita kura za maoni sisiem akaenguliwa, akaenda Chadema akashinda ubunge hadi leo anapeta.
    kaka timuka bado muda upo.

    ReplyDelete
  5. Kaka unayo personality. Tulia utapewa Udc au Urc

    ReplyDelete
  6. Haya Maisha ya serikali yetu na Vyombo vyake mbali mbali kama pccb ni kama Tamthilia isiyo na mvuto kwa wafuatiliaji,
    Serikali imejaa wasomi kibao wakiwemo maprofesa, tunawaheshimu wazee hawa ila woooote wamekuwa wapuuzi kupindukia, hawatumii elimu zao kukwamua nchi hii, bali wamejaa ubinafsi wanataka siasa tuuuu, hakuna point wanazoongea..wamekuwa kama watoto wa primary.
    Wakina Mramba, Chenge na wengine weeengi wanafanya maigizo na mahakama na pccb.
    AMKENI WATANZANIA....Haya mambo mpaka lini Ulimwengu wa sasa si wa siasa za kipuuzi kama za Tanzania bali ulimwengu wa SAYANSI.

    ReplyDelete
  7. ivi kwanini mnang'ang'ania sisiemu?
    na ivo wanavowashuka ngiri bado mpo tu

    ila siku moja tutafika

    ReplyDelete
  8. ..........yANGU UMEIBANIA EE, POA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...