Mkurugenzi wa PSET, Osman Kazi akizungumzia bonanza ambalo amaenadaa kwa mara ya kwanza kwa ajili ya watoto yatima siku ya Idd pili katika viwanja vya leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Watoto wanaoishi katika mazingira magumu wataandaliwa michezo na burudani mbalimbali ikiwa ni pamoja na chakula na vinywaji.Kushoto kwake ni Bi Mwanaisha Magambo wa New Life Orphanage. na picha ya chini kulia kwake ni Mwakilishi wa Movenpick Seraphin Lusala.
Taasisi ya michezo ya Popular Sports and Entertainment (PSET) ya Jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza imeandaa bonanza maalum kwa ajili ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu na yatima litakalofanyika katika viwanja vya Leaders Club siku ya Idd pili.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ambaye ni referee mashuhuri nchini, Osman Kazi alisema Jijini jana kuwa bonanza hilo limeandaliwa kwa ajili ya kuwathamini na kutoa nafasi kwa watu wenye mapenzi mema kuweza kushirikiana nao katika siku kuu hiyo muhimu hususan mwa waislam.

Kazi alisema PSET inafanya kazi ya kuratibu bonanza hilo ambalo litashirikisha watoto wapatao 500 kutoka vituo mbalimbali vinavyowalea jijini Dar es Salaam na wataandaliwa michezo mbalimbali kwa siku nzima kuanzia saa 09:00 asubuhi hadi jioni.

Mbali na michezo pia watoto hao watapata burudani mbalimbali ikiwemo vyakula, vinywaji na mashindano ya kuonyesha vipaji vya aina tofauti ambapo watakuwa wakizawadiwa.

“Sisi PSET tumeona watoto hawa wamekuwa wakikaa katika vituo vyao na hawajawahi kukutana pamoja, kikubwa ni wao kujumuika na kufurahi kama watoto wengine wanaoishi na wazazi wao” alisema Kazi.

Aliongeza kuwa kutakuwa na michezo kama vile soka, riadha ,mbio za magunia, kuruka kamba , kutembea , mbio za vijiko, kupuliza vuvuzela, kukimbiza kuku na mingine mingi.

Hivyo ili kufanikisha bonanza hilo Kazi aliomba taasisi mbalimbali, mashirika, kampuni na watu binafsi kujitokeza kusaidia maandalizi ya bonanza hilo ikiwa ni sehemu ya sherehe hizo za dini ya kiislam ambazo huwataka waumini kuwasaidia wasio na uwezo.

Alisema si lazima kugharamia kila kitu lakini watu wanaweza kutoa vyakula, maji soda, juisi na vitu vingine kwa watoto hao, pia vifaa vya michezo vitakavyotumika siku hiyo na hata usafiri kwa ajili ya watoto hao kutoka vituoni kwao hadi viwanja vya leaders.

“Hii hatufanyi kama biashara bali ni kukusanya watu wenye moyo mmoja wa kujitolea ili kuweza kuwafanya watoto yatima kujisikia kuwa kuna watu wanaowathamini” alisisitiza.

Tayari Hoteli ya Movenpick ya jijini Dar es Salaam imejitolea kusaidia tamasha hilo kwa vinywaji na ukumbi wa mikutano.

Kikubwa ni watu kujitokeza na kujumuika na watoto hao pamoja na familia zao katika siku ya tukio ili kuifanya iwe ya mafanikio zaidi. Hotel Movenpick Royal Palm imejitolea uku,nbi wa mikutano na vinywaji kwa jili ya maandalizi.

Kwa mawasiliano piga simu namba
0713 477300 ama 0715 732333.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Matumizi ya maneno: Samahani naomba kwa wale mliobobea katika lugha yetu tukufu ya kiswahili mnisaidie kufahamu maana ya neno BONANZA. Neno hili nimekuwa nikilisoma mara kwa mara, linatumiwa na waandishi wa habari lakini mimi sifahamu tafsiri yake. Nimetafuta kwenye mtandao (WEB DEFINITIONS), lakini sijaona maana hata moja inayoendana na namna linavyotumika kwenye kiswahili. Je asili yake ni kibantu? kiingereza? kiarabu? Kireno? Naomba mchango wenu wadau

    ReplyDelete
  2. Matumizi ya maneno: Samahani naomba kwa wale mliobobea katika lugha yetu tukufu ya kiswahili mnisaidie kufahamu maana ya neno BONANZA. Neno hili nimekuwa nikilisoma mara kwa mara, linatumiwa na waandishi wa habari lakini mimi sifahamu tafsiri yake. Nimetafuta kwenye mtandao (WEB DEFINITIONS), lakini sijaona maana hata moja inayoendana na namna linavyotumika kwenye kiswahili. Je asili yake ni kibantu? kiingereza? kiarabu? Kireno? Naomba mchango wenu wadau

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...