Na Mary Kweka –Maelezo
Msajili wa Vyama Vya Siasa Nchini John Tendwa amesema atatoa uamuzi wake dhidi ya malalamiko yaliyowasilishwa ofisini kwake jana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu mgombea wa urais kupitia chama cha mapinduzi (CCM) baada ya siku tano.
Bwana Tendwa ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam baada ya kupokea malalamiko hayo rasmi leo.
‘’Nitatoa maamuzi hayo baada ya kupokea maelezo kutoka kwa mlalamikiwa dhidi ya mlalamikaji yaliyowasilishwa,na nitatoa nakala ya maamuzi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi na Katibu Mkuu wa chama cha CHADEMA’’,Alisema Tendwa.
Akifafanua suala hilo Tendwa amesema baada ya maamuzi yake mlalamikaji na mlalamikiwa kama hawataridhika na uamuzi wake wanayo haki ya kwenda kutafuta haki yao kwenye vyombo vya sheria.
Aidha Msajili huyo wa Vyama ameongeza kuwa amepokea malalamiko hayo kwa mujibu wa sheria ya gharama za uchaguzi inachomkataza mgombea yeyote ambaye yeye mwenyewe, wakala wake au Chama chake kitafanya kitendo ambacho kimekatazwa kama ilivyoelekezwa kwenye sheria hiyo atakuwa au kitakuwa kimepoteza sifa za kushiriki mchakato wa uteuzi au uchaguzi.
Pingamizi hilo liliwasilishwa jana ofisi ya msajili huyo na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika wakimlalamikia Mgombea urais wa chama cha mapinduzi,Jakaya Mrisho Kikwete kutumia madaraka yake kutoa ahadi kwenye kampeni na kutangaza nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi wakati wa kampeni.

hiki ni kitendawili cha kuku na yai
ReplyDeleteKwa nchi zinazo fuata sheria JK angeenda na maji lakini kwa nchi za funika kombe mwanahalamu anapita ni sawa na kesi ya ngedere umpelekee nyani. Mdau mchwechwele
ReplyDeletekazi kweli kweli. Yangu Macho na masikio
ReplyDeleteYaani tendwa kashindwa kuweka jino bandia????????????????????????????
ReplyDeleteAnatoa uamuzi gani wakati, uamuzi unajulikana kuwa JK ataendelea kuwa mgombea na atashinda/shindishwa kwa vyovyote. Ushindi ni lazima. Kesi ya nyani hawezi kuihukumu ngedere kwani wote ni wezi wa mazao
ReplyDeleteKesi ya mbuzi inapelekwa kwa fisi. Mbuzi atatendewa haki kweli? Yeye si nyama tu mbele ya fisi. Yetu macho.
ReplyDeleteUnamshitaki Mwajiri kwa mfanyakazi wake. Unategemea mfanyakazi kumhukumu mwajiri wake. Akifanya hivyo atakuwa hana kazi.
ReplyDeleteNadhani tendwa anapaswa kusimamia kwenye ushahidi, vidhibi kama video au tape za hotuba, watu waliokuwepo na baadaye kuamua sawa sawa na sheria. Asianze kutoa maamuzi kama ya yule jaji anayesema mtu anapendwa wakati kura hazijapigwa bado, hata majambazi kama akina kipagate walipendwa sana lakini bado walikuwa majambazi. Naamini kwa demkrasia yetu changa huu utakuwa ni mtihani mgumu kwa Tendwa, akifauru kwenye hili Tanzania nzima tutavuka hatua moja kutoka huku kwenda kule
ReplyDeletesheria ni msumeno na hakuna aliye juu ya sheria, kama ccm wameenda kinyume na sheria mpya ya uchaguzi hawana budi kuwa kicked out. Think about it, ni mara ngapi wamekuwa wakiwadaganya watanzania wakati wa kampeni ili kupata kura zao, na baada ya wao kuchaguliwa maofisini hizo ahadi hazionekani huku wao wakila kuku kwa mrija. wakati umefika kwa watanzania walio wengi kubadilika na kufikiria long term sio ahadi zisizokuwa na vichwa.
ReplyDeleteKWA HAKIKA TENDWA HANA MAAMUZI MAPYA, NI YALE YALE KWAMBA JK HANA HATIA. NA KAMA MNABISHA NGOJENI MUONE! HAWEZI KUCHEZA NA KIBARUA CHAKE ATALALA NJAA! NAMFAHAMU TENDWA ANAIPENDA FAMILIA YAKE SANA, KIBARUA KITAMU BWANA. KAMUA TENDWA USIOGOPE SEMA JK HANA HATIA, USIJE LALA NJAA BURE KWA MICHEZO YA SIASA.
ReplyDeleteTendwa ataweza kumvika Paka kengele ndugu zangu!!!!?
ReplyDeleteTENDWA HAWEZI KUBADILI SHERIA KATIKATI YA MCHEZO. TUMESHASEMA WASANII TUMEWATENGEA MILIONI HAMSINI TU. HIVI NI VIJISENTI TUMETAMKA LAKINI SIO RUSHWA. WATAALAMU WANAKUJA HII SIO KISHAWISHI NI SERA YETU SISI WANA CCM. JUMA NATURE,PROFESA J. SAIDIENI JAMANI
ReplyDeleteNAJUA WAZI KABISA KABISA KUWA RAISI WANGU MPENDWA AMETELEZA KATIKA SUALA HILO: LAKINI NAJUA PIA KUWATENDWA HANA UBAVU WOWOTE WA KUMNYOOSHEA KIDOLE JK.
ReplyDeleteVYAMA VYA UPINZANI NYIE MUENDELEE KULALAMIKA TUU, LAKINI SIE WANA- CCM TUTAENDELEA KUPETA HATA TUKIVUNJA SHERIA YOYOTE.
C C M HOYEEEEE
Hapa hakuna jipya,uamuzi utakaotolewa hata mtoto wa primary anaweza akakwambia utakuwaje.Sio kwa nchii hii bwana,hii tayari ina wenyewe na wenyewe ni wao kama wanavyotamba.
ReplyDeleteMnyika. Kwa hilo mlilolifanya kweli naapa kura yangu sikupi wala padre mwasi siwapi. No!!!
ReplyDeleteMheshimiwa Msajili, wajua mfa maji haachi kutapatapa. Nakushauri wasikupotezee muda kwa hoja zisizo na mashiko. watafute hoja nyingine zenye mashiko au wasubiri kimbunga hapo Oktoba.
ReplyDeleteNina hakika hatuongei tusichojua. na daima tutakuwa mbele....CCM nambari wani
Hahah Hvi Hapa Jamni kuna mtu anatarajia matokeo tofauti hapa!! Naungana mkono na mchangiaji alopita kwamba kibarua kitamu plus familly loves!! Haya tendwa tunakusikiliza kama umekomaa kiasi gani ki democrasia na uko imara kiasi gani katika kazi yako.
ReplyDeleteHiyo kesi kwa brother Tendwa ni sawa na Mike "iron" Tyson wa 1995 dhidi ya Francis Cheka, Unategemea nini? Francis Cheka kumpiga Tyson? Acheni masihala wadau. Majibu ya kesi tayari yanajulikana, KINGS NEVER DO WRONG, au mmesahau usemi huu?
ReplyDeleteNaomba kuanzisha opinion poll hapa wadau mchangie.
ReplyDeleteSwali : Je,unadhani maamuzi ya Tendwa yatakuwa kumuengua JK katika kinyang'anyiro cha ugombea urais kutokana na kukiuka sheria ya uchaguzi. A.NDIO
B.HAPANA
C.SIJUI
JIBU NI D:NAJUA
ReplyDeleteC
ReplyDelete