Tonny akifikishwa mahakama ya Kisutu jijini Dar

Tonny George Rugabandana Tzamburakis amefikishwa mahakamani leo kujibu tuhuma za kujipatia Sh milioni 424 kwa njia za udanganyifu.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Globu ya Jamii imezipata usiku huu, Tonny ni binamu yake Kinjeketile Ngombale Mwiru, na ni mtoto wa marehemu George Rugabandana Tzamburakis, ambaye ni shemeji yake Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, yaani mtoto wa kaka yake Mama Kingunge Ngombale Mwiru, ambapo yeye na dada zake kwa pamoja na Kinje wamelelewa na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru baada ya baba yao kufariki dunia.

Akisomewa mashitaka yake leo na Inspecta wa polisi, Emma Mkonyi mbele ya hakimu Mkazi, Gabriel Mirumbe mshitakiwa alidaiwa kughushi, kula njama na kujipatia fedha hizo kwa njia za udanganyifu.
Tonny alidaiwa akiwa na wenzake wasiyofahamika katika siku na mahali pasipofahamika jijini Dar es Salaam walikula njama ya kuiibia kampuni ya SCI (TZ) LTD kiasi hicho cha fedha kwa njia ya ujumbe wa kuhamisha fedha kwa haraka.

Aidha katika shitaka jingine alidaiwa kughushi fomu ya benki ya kuhamishia fedha yenye namba E17 ya Agosti 29, 2008 kwa nia ya kuonyesha kuwa fomu hiyo ni halali imesainiwa na mkurugenzi wa kampuni hiyo,Ravishankar Rasiman.

Shitaka la tatu ilidaiwa Agosti 29, 2008 katika benki ya Barclay iliyoko mtaa wa Ohio, Dar es Salaam aliwasilisha fomu hiyo kwa mfanyakazi wa benki,Bituni Chiza ambaye huku akijua haikuwa halali.

Aidha katika shitaka jingine alidaiwa kati ya Septemba na Octoba 2008 katika benki ya CRDB tawi la Kijitonyama, Dar es Salaam alichota Sh 424,458,799.29 kutoka katika akaunti namba 01j014293000 ya SCI (TZ) LMD akionyesha kuwa fedha hizo ni halali zimetolewa na kampuni hiyo kwenda kwenye kampuni ya Temm Power Solution akijua haikuwa kweli.

Tonny alirudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza mashalti ya dhamana. Ili apate dhamana alitakiwa na hakimu huyo kuwa na wadhamini watakaotoa Sh milioni 10 pamoja na hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo. Kesi hiyo itatajwa Agosti 31 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Kukosea ni kitu cha kawaida . Ila hapo Ngombari mwiru ulimwaibisha kweli . Thanks though

    ReplyDelete
  2. kaka Michuzi pole sana. najua utakuwa ulipigiwa simu na kutakiwa kubadilisha title ya habari hii. Kweli nadhani ilipotoshwa kwa kusema Tony Kingunge, ilikuwa kama kumchafulia jina mzee.
    sasa afadhali tunaelewa

    ReplyDelete
  3. kaka michu lakini jana hakimu hakusita kumuuliza kama yeye ni mtoto wa kingunge na akajibu ndio tena ni baba yake wa kumzaa sasa inachanganya ebu wadau wa libeneke tusaidieni.

    ReplyDelete
  4. Ilivyoandikwa leo ndo sawa kabisa, jana aliyetuma habari alitaka tu kumchafulia mzee

    ReplyDelete
  5. Lakini mbona alivyouliza kama ni mtoto wa Kingunfe Ngombale Mwiru aliitika "ndio". Ametumia jina la huyo babu wa watu kuwaibia watu wengine. Na huo ndio mchezo tunaotakiwa kuutokomeza tanzania pia

    ReplyDelete
  6. Mbona picha umeichakachua?

    ReplyDelete
  7. I am a social analyst
    a. Toni kalelewa na Mzee Kingunge, so anahaki kumwita BABA

    b. Je Hakimu kumuliza kwanini anaharibu jina la Mzee Kingunge, ina maanisha amekwisha mhukumu? kusema kweli hapa sheria hailindi mtuhumiwa kabisa.Jana Anty yake Obama judge kamuokoa asirudishwe Kenya pamoja na kuwa ni illegal immigrant eti kuna 10% chance atakuwa prosecuted na polisi ni wakatili akirefer to vurugu za uchaguzi wa 2007

    c.Michuzi najua watakuwa wamekupaka sana ulivyokosea jana

    d. je Toni akidai sio yeye anayeshitakiwa,kwa sababu charge sheet inasoma jina Toni Kingunge Mwiru?

    ReplyDelete
  8. mzee ngombale amemlea tony tangu yuko mdogo ni kama mtoto wake ..ni mtoto wake wa kufikia so ni kama mtoto wake...

    ReplyDelete
  9. mzee kingunge amewalea akina tony, henry, marehemu jeska, flora na kisa aliyekuwa mke wa john mongela. japokuwa c watoto wake wa kuzaa lakini aliwapenda kama ambavyo alimpenda mtoto wake wa kumzaa kinje.

    kwa hili nampa 5 huyu mzee..mnyonge mnyongeni but haki yake mpeni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...