
Mmoja wa marehemu, Omar Ali Jadi
Wagombea wawili katika uchaguzi mkuu ujao wa nafasi za uwakilishi na udiwani kupitia chama cha wananchi CUF wamefariki dunia usiku wa kumkia leo.
Akizungumza na Zenji fm radio mkurugenzi wa mawasiliano ya umma CUF Salum Bimani amesema waliofariki ni mgombea wa nafasi ya uwakilishi jimbo la Kojani Omar Ali Jadi.
Amesema Jadi ambae ni mwakilishi wa zamani wa Jimbo hilo amefariki dunia katika hospitali ya Chakechake Pemba.
Bimani amemtaja mgombea mwengine aliefariki dunia katika nafasi ya udiwani wadi ya Kikwajuni ni Shani Ahmad Shani. Amesema mgombea huyo amefariki dunia kwa ajali ya gari alipokuwa akirejesha fomu za kugombea nafasi hiyo.
Bimani ameiambia Zenji Fm radio kuwa CUF inawasiliana na tume ya uchaguzi Zanzibar ili kupeleka majina mengine ya wanachama wao watakaogombea nafasi hizo
Source: http://zanzibarislamicnews.wordpress.com/
Ohooooooooo!
ReplyDeleteYale yale!!!