Kaka Michuzi kwanza pole kwa kazi ngumu unayoifanya.
Nikiwa kiongozi na Kocha wa Timu ya wa Tanzania wanaoishi UK, natoa taarifa kwa Watanzania wote kuwa tumeweza kupita stage zote na kuweza kufikia nusu finali za African Cup. Jumamosi hii tunakwaana na Wanaigeria kwa kiwango chao tutawalaza tu.
Dua. Mungu Ibariki Tanzania. Ameen

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. ndugu kiongozi na kocha wa timu ya wa Tanzania Uk hebu tueleze basi ni wapi mtakapo cheza hiyo nusu fainali, wakati na kiingilio nasi tuje kuona hiyo nusu fainali?

    ReplyDelete
  2. We coach hizi matches zinachezwa mji gani???????

    ReplyDelete
  3. Hang on! kocha wa timu ya taifa ya wa Tanzania UK? unahakika? haiwezekani hata siku moja na kusema kweli wala hatukutambui wewe na timu yako ya wa Tanzania.
    Unachotaka kusema ni kuwa timu yenu ya wa Tanzania wa sehemu fulani nchin UK hapo kidogo nitakubali lakini wa Tanzania wote uk hamtuwakilishi kwa timu hiyo maana hatujakuchagua wewe, kamati yako au hata hao wachezaji kutuwakilisha kama timu ya Taifa hapa uk.
    Nawe michuzi nawe nakulaumu pia kwa kuruhusu habari zisizo sahihi kutokea hapa.

    ReplyDelete
  4. Watanzania tuna matatizo makubwa ya ligi na mabishano yasio na msingi. Mwaka jana nikipitia michuzi blog nilipiga tarumbeta juu ya Watanzania millioni ukiwemo wewe anonymous wed 07:37pm kujitokeza sikuwaona. Juu ya kuacha namba zangu kazaa na mail address ni watu wachache tu waliowasiliana na mimi na walioweza kuja na nikiwa na akili timamu nimeamua kubakia nao na ndio wanaounda timu. Tulinyimwa hadi bendera ubalozini mwaka jana. Kama unauchungu sana sheikh tafuta wachezaji wako ita timu ya watanzania halafu basi. Sioni kama nitatizo maana nia zetu zakutangaza taifa letu litatimia bila mtafaruku.

    Kwa wale wanaotaka kuja ama kuchangia kiuchezaji mnakaribishwa. Hatutaki michango ya kifedha. Wasiliana na mimi kwenye E-mail ifuatayo: Sweety_s_2007@hotmail.com

    Link ya mashindano: www.uanu.co.uk

    Mashindano yapo East London na kama unataka kuja mdau nitumie mail nitawasiliana na wewe.

    Ni mimi kiongozi watimu na ambaye sikuchaguliwa.

    Shukran

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...