Year: 2001
Millage: 39,000
Cc: 1998
Transmission: Automatic
Location: DSM-Tanzania
Asking price: 21,000,000 (negotiable)
Engine type: VVTi
Contact
0754 573435
0655 657911

kwa ndani
kwa mbele



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. Usipoteze hiyo pesa ,kwani hapa nilipo unapata kwa mil 8-9 kusafirisha tsh 1600000,wasilaina na mimi georgekululetera@yahoo.co.uk nitakutumia gari ,Acha na huyo mwizi

    Mdau

    ReplyDelete
  2. Kweli Tz pesa nje nje.Kwa bei hiyo, year, millage. Eeh bwana eeeh!!!

    ReplyDelete
  3. Huu kweli ni utani na hela. Yaani gari RAV 4 ya 2001, bei yake ni TZS 21 million!!

    ReplyDelete
  4. hili siyo lile lililoibiwa pale Mlimani City..alafu mbona bei kubwa hivyo atawavunja moyo watu.

    ReplyDelete
  5. Una akili timamu wewe unayeuza RAV4 kwa milioni 24? Gari exactly kama hiyo nimeinunua recentlty kwa milion 8 hivi majuzi. Magqari bongo ni bwererereeeeeee.

    ReplyDelete
  6. nyie ni watu wa ajabu sana sasa kama bei yote hiyo kuna haja gani ya kutangaza hapo kwenye blog wakati kuna miyard kibao mtu unaenda kwa raha zako kuchagua kuweka hapo ndio isaidie nini tena kwa bei hiyo ya kifisadi kabisa hupati mtu hapo.

    ReplyDelete
  7. jamani bei hizo angalieni hivi utauza kweli?

    ReplyDelete
  8. waosha vinnywa bwana lazima wazungumze , sasa kama unaona gari bei kubwa kaa kimya , utapata nini ukimuharbia mwenzio biashara yake ???
    pambaffffff!!!!!!

    ReplyDelete
  9. Nyie kama hamna hela si kaeni kimya tuu. Tuacheni sisi wenye pesa zetu tununue hiyo gari. What is 21M? ukimnunulia mchuchu wako na kumpa zawadi kwa raha anazokupa?, Ebo?. Mshkaji subiri simu yangu kesho wasikukatishe tamaa

    ReplyDelete
  10. we unayesema uliyenunua mil 8.0 tunadanganyana(labda bajaji sio RAV4 hiyo!!). Mil. 16-18 is the range. Tuache kuosha vivywa jamaa kasema bei aliyotaja ni negotiable.

    ReplyDelete
  11. kwa kifupi wasanii wa bongo, shule hawana, kama mnabisha nitajieni wasanii wenye japo bachelor.

    Hivyo uwezo wa kufikili ni mdogo.

    wana kipaji cha kushambulia jukwaa tu.

    ReplyDelete
  12. HUo ni wizi, si Ghali kiasi hicho, kuna jamaa alikuwa anatoa za rangi nyekundu kwa ma shavu,unataka kuniambia alikuwa anazinunua milioni 21.

    kuna jammaa anayo alinunua milioni tisa acha bei za wizi kaka.

    ReplyDelete
  13. MASKINI BWANA NYIE WOOTE HAPO JUU MNAOSEMA BEI MBAYA MKAE KIMYA,NAONA MNAZUNGUMZA VITU MSIVYOVIJUA,KAMA HUYO ANAYESEMA AMENUNUA GARI MIL 8 NI BWEGE MTOZENI ANAJIFANYA ANAJUA KUMBE ANAUNGUA NA JUA...UNAJUA WABONGO KWA KUJIFANYA WANAJUA VITU..NDIO MAANA MNAISHIA KUNUNUA MCHINA TU SHENZI ZENU.....KWANZA KABISA NDUGU YANGU UNAYEUZA GARI HII GARI IMETOKA WAPI EUROPE AU NDIO ZILE ZA DUBAI MAANA QUALITY MATTERS ILA WABONGO HAWAJUI HILO WANADHANI GARI GARI....PUMBAVU KABISA,NA ISITOSHE NAONA LINA NAMBA YA BONGO JE UMESHALITUMIA?KAMA NDIO BASI HIYO BEI ITABIDI ISHUKE NA UZURI MMOJA UMESEMA MAONGEZI YAPO....KUSEMA UKWELI HIZI GARI BEI YAKE IPO JUU KIDOGO KAMA UK GARI KAMA HII BEI YA CHINI HUWEZI KUPATA CHINI YA POUND 3500 UKIWEKA KUSAFIRISHA SAY POUND 1000 NA USHURU NA GHARAMA NYINGINE NDOGO NDOGO INAFIKIA HUKO KWENYE MIL17 ILA KWA SABABU MTU HAFANYI KITU BILA FAIDA LAZIMA BEI IANZIE KWENYE MIL...NASHANGAA WAOSHA VINYWA WANAONGEA UTUMBO...SASA HAPO HAPO NENDENI KWENYE HII SITE www.tzadverts.com MUONE WABONGO WENZENU WANAWAUZIA GARI KAMA HIYO SHILINGI NGAPI...HATA UKIIAGIZA JAPAN BADO NI BEI KUBWA TOFAUTI NA WAJINGA WANAOSEMA MIL...LABDA KIWANDA CHA TOYOTA CHA BABA YAKO...WABONGO BWANA WANAKURUPUKA HATA BILA KUFANYA UDADISI NA KUONGEA UTUMBO...NDUGU MUUZAJI WASIKUKATISHE TAMAA KOMAA NA BEI HIYO HIYO MTU ANAYETAKA FANYA NAE MAONGEZI KWA BEI INAYOKURIDHISHA..WANAOJUA VITU WATANUNUA WAACHE WABONGO WASUKUMANE NA VI MARK 2 VYAO.

    ReplyDelete
  14. T REG is not 2001 that is 1999. hapo umenidanganya live and for that reg i doubt the millage...

    ReplyDelete
  15. vvt-i siyo engine type ni teknolojia ya kisasa katika injini za magari,ilianzishwa na toyota na wengine wanatumia pia. Google utapata historia ukitaka. Engine type inaweza kuwa 1AZ-FE or like.

    ReplyDelete
  16. We uliyesema T Reg ni ya 1999, mwone.. hiyo ni namba ya Tanzania sio UK.

    ReplyDelete
  17. Kuna waropokaji waliopitiliza, milioni 8 ununue rav 4 hii, na zile za version ya nyuma milango mitano utanunua milioni ngapi mbili?

    ReplyDelete
  18. hiyo bei ni kwa hela ya Zimbabwe au TZ? maana mimi nimenunua kama hiyo kwa sh.9,000,000. tu.

    ReplyDelete
  19. hiyo gari haita nunuliwa kamwe kwa bei hiyo mpaka ukamilifu wa dahari.amen

    ReplyDelete
  20. Kila mmoja anaongea lake lakini bei hiyo iko sawa kwani hapa uk itakuwa kati ya pound elfu tano au elfu nne na miatano, kusafirisha bei ni pound 850, ushuru wetu na miangaiko ya madalali wetu bandarini, na kama ni toyota europe ni sawa. Kuna mmoja anasema kanunua yake kwa 8 million, inawezekana lakini kwa Tanzania sishangai ukakuta hiyo gari ina namba za pikipiki na ushuru hakuna au examptation ya mwalimu aliyekufa lakini bado yupo kwenye payroll, hiyo ndiyo nchi yangu Tanzania, kila siku huwa nasema kuna watu wametoka Tanzania na kujifanya wakimbizi na hata wengine kujificha marakani na Europe bila kwenda nyumbani, leo nashangaa mchangiaji mmoja kasoma namba ya gari anasema ni T Reg, yaani hii namba ya Uk ya mwaka 1999, hajui kabisa kwamba namba Tanzania zilishageuzwa, huyu anahitaji msaada wa hali ya juu sana.
    Mdau uk.

    ReplyDelete
  21. VVTi - Variable Valve Timing with Intelligence. Hiyo ndio Toyota bwana.

    ReplyDelete
  22. Hii ni kwa waosha vinywa wote. Ukweli ni kwamba bei aliyotaja muuzaji ni sahihi ukiangalia model yenyewe ya RAV4, mwaka iliyotengenezwa, hali yake na mileage (kilomita iliyotembea). Kwa wanaojua magari bei hii haishangazi. Kama model za zamani za RAV4 (milango mitano) za miaka kati ya 1996 na 1998 na ambazo zimechapa zaidi ya kilomita 100,000 zinauzwa hadi shilingi milioni 17 katika showrooms za Dar, sembuse hii. Isitoshe, muuzaji ameweka bayana kuwa maongezi yapo.Tusipende kuzungumza sana bila kuelewa kile tunachokizungumzia.

    ReplyDelete
  23. we Ano unasema wasanii wa kibongo hawajasoma unataka nikutajie mwenye bacholar
    basi kwa taarifa yako JK ni msanii na ana PHd japo ya kupewa

    ReplyDelete
  24. Kama bei ya RAV4 model hii ACA21 AU ZCA26 ya mwaka 2001 ingekuwa 9Million basi taxi zote zingekuwa ni RAV4. Mimi niliagiza gari kama hii mwaka jana from Japan 2001 model sio VVT-i engine ilicost Tsh. 18M (Comprehensive insurance, full registered, Fire extinguisher, Triangle, kuandika vioo etc ) sasa hao wabeba mabox wanachonga tu hata hawana data. CIF ilikuwa $. 7700, Duty Tshs. 5.8M sasa huyo anayesema itacost 9 milion akanunue Mark 2 box !!

    ReplyDelete
  25. SIKIZA JAMANI,MI NISHAENDA KUIONA HII GARI NI EX-UK! TENA IMEINGIA MUDA SI MREFU NA KI INAVYOONYESHA HAIJATEMBEA SANA HAPA BONGO KWANI ANA MIKOKO KIBAO,LABDA NDO MAANA AMEAMUA KUIUZA,LAKINI GARI NI YA UK WALA SIYO ZILE ZA DUBAI REFURBISHED!!!!

    ReplyDelete
  26. I think this RAV4 is very well in condition. But I need to know more details about this RAV4.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...