Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa,Evarist Mangalla

Na Francis Godwin,Iringa

JESHI la polisi mkoani Iringa linawashikilia watu watano wakazi wa kijiji cha Kipera wilaya ya Iringa vijijini ambao ni ndugu kwa tuhuma za kuchoma moto nyumba ya mzee wa miaka 87 wakimhusisha na imani za kishirikina.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla aliwaeleza waandishi wa habari jana ofisini kwake kuwa tukio hilo lilitokea janamajira ya saa 7 usiku wakati mzee huyo ambaye pia ni ndugu katika familia yao akiwa amelala ndani.

Kwa mujibu wa Kamanda Mangalla mzee huyo Yolomini Nyakunga (87) alinusurika kifo kutokana na tukio hilo la kinyama dhidi yake na kuwa lengo la wana ndugu hao lilikuwa ni kumteketeza kwa moto mzee huyo.

Aliwataja ngudu hao ambao wamekamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuteketeza nyumba hiyo kwa moto kuwa ni Dotto Kipiki (29),Chesco Nyakunga (46), Vicent Nyakunga (30), Rusia Nyakunga (48) na Odosia Nyakunga (48).

Kamanda Mangalla alisema kuwa mali zote zilizoteketea kwa moto huo zina thamani ya shilingi 380,000 na kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi wa tukio hilo kukamilika.

Wakati huo huo watu wawili wamefariki dunia katika matuki mawili tofauti mkoani Iringa likiwemo tukio la wa mtoto Auguston Sanga (2) mkazi wa Kilimahewa wilaya ya Ludewa aliyepoteza maisha yake kwa kutumbukia katika kisima cha maji wakati akicheza jana majira ya saa 8.45 mchana.

Katika tukio la pili lililotokea eneo la Kihessa mjini Iringa juzi majira ya saa 5 usiku Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Angelina Kiwango (45) alianguka na kufa akiwa bafuni nyumbani kwake alisema kamanda Mangalla

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kwani miwani lazima hiyo lakini Afande ??? au basi tu unataka tucheke ??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...