Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM,Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Kilolo baada ya kumaliza mkutano wa kampeni katika Jimbo hilo la Kilolo la mgombea Ubunge Profesa Peter Msolla.
Wananchi wa Kijiji cha Kilolo Jimbo la Kilolo Mkoa wa Iringa, wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM,Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia wananchi wa jimbo hilo katika mkutano wa kampeni ikiwa ni pamoja na kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo hilo, Profesa. Peter Msolla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. CCM Bwana hawana maana! Kisa cha kukitesa kizee cha watu ni nini? Hiki kizee kinatakiwa kile pensheni nyumbani na kuwasimulia wajukuu zake hadithi. Tuweni na huruma jamani.

    ReplyDelete
  2. Lakini habari kutoka vyanzo vya uhakika ndani ya CCM zinasema kuwa hatua ya chama hicho kuondoa siku za mapumziko kwa mgombea wake huyo wa urais, imekuja ili kukabiliana na upepo wa kisiasa ulivyo kwa sasa.

    Vyanzo hivyo vimefafanua kwamba CCM imepokea taarifa za kiupelelezi zinazoonyesha kuwa iwapo Kikwete ataendelea na mfumo wa kampeni anaoutumia sasa wa kujipa siku za mapumziko, anaweza kupunguza kiwango cha kura anazotarajia kupata kumwezesha kuwa tena rais katika uchaguzi mkuu ujao, Oktoba 31.

    "CCM imeamua kubadili mfumo wa kampeni za Kikwete... sasa hatapumzika kama alivyopangiwa awali, atafanya kampeni kila siku kwa siku zilizosalia," alieleza mpashaji wetuo.

    Wapashaji habari hao walilidokeza gazeti hili kuwa taarifa ilizonazo zinaonyesha kuwa kuna wagombea urais wawili wa vyama tofauti ambao hadi sasa wameonyesha ushindani dhidi ya CCM, hali ambayo imekishtua chama hicho tawala na kuamua kuongeza nguvu katika kampeni zake kwa lengo la kulinda "ushindi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...