Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu muda mfupi baada ya kumalizika kwa swalla ya Iddi iliyoswaliwa katika Msikiti Mkuu wa Riyadh mjini Tanga leo asubuhi
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono wa Iddi na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati wa Swalla ya Iddi iliyoswaliwa katika Msikiti mkuu wa Riyadh mjini Tanga.Mzee Mwinyi ndiye mgeni Rasmi katika baraza la Iddi litakalofanyika kitaifa mjini Tanga.
Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Mufti Mkuu sheikh Issa Shaaban Simba wakati wa Swalla ya Iddi iliyoswaliwa mjini Tanga leo.Katikati anayeangalia ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaaban Simba wakati wa swalla ya Idd iliyoswaliwa kwenye Msikiti Mkuu wa Riyadh mjini Tanga leo asubuhi (picha na Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Nawapa mkono wa Eid Mubaraka kwa waislam wote popote walipo na pia kwa bin Adam wote wa dini zote na madhehebu yote.All of us who believe in one God, are on the same journey, we are just taking different routes.The events in Florida in America should have alerted us to the *smallness* of some human's mind and the hand of the prince of darkness. It reminds us that we should be tolerant to the intolerant, and its noble to disagree without physical conflict. Yarabi twaomba uongozi.
    Again EID MUBARAK TO YOU ALL
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  2. Kikwete kweli Kipenzi cha watu hasa hata kwa Nje mambo ya kichama, Inshallah mwenyezimungu atamfungulia ajue zaidi kuhusu dini.

    ReplyDelete
  3. Hiyo salamu ya mzee ruksa na jk imetiafola. inaonyesha ukaribu na upendo mkubwa uliopo kati yao.

    ReplyDelete
  4. NdumbaNangaeKamosingaSeptember 10, 2010

    Michuzi, mbona hatuoni picha ya Dr Slaa akila Eid au japo kutoa salaam za Eid? Au kaenda kula eid na pastor Johns wa Florida? Michuzi ukibania hii nitakasirika maana viongozi wote lazima waonyeshe kutofungamana na dini wakati kama huu na nimeshangaa kutosikia au kuona picha ya Dr Slaa.

    ReplyDelete
  5. mzee wetu ruksa mtoto wa mjini huyo tunampenda na tutaendelea kumpenda kwa yale aliyotufanyie baada ya kuichukua nchi ikiwa kavu kutoka kwa mwalimu na kuruhusu kila mwenye uwezo wa kuingiza kitu chochote kutoka nje aingize.

    mungu akujaalie uishi miaka mingi zaidi ameen.

    ReplyDelete
  6. Mkono wa Eid kwa waislamu wenzangu wote.Tumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutujalia kufunga na kufika siku hii Eid El Fitr.Back to Square One untill next year.

    ReplyDelete
  7. Waislamu tukae mkao wa kuleta amani duniani si vurugu.

    Dunua nzima inatuogopa kwa vurugu. Basi baada ya kumaliza mfungo mtukufu tubadirike: Tuachane na kujitoa mhanga maana wanakufa watoto, wazazi,wake na waume zetu.

    Tulete amani dunia ishangae. Imefika wakati sasa kila muislam akiingia pahala watu wanaingia woga wanaona kana kwamba ataacha mabomu.

    Dini ya Kiislam ni dini tukufu, waumini wake hatupaswi kuwa tishio, bali tuwe kimbilio.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...