Mr. Michuzi,
Bado unazunguka kwenye kampeni?
Mie nipo Dodoma na baadae Morogoro kesho, ila mwisho wa wiki ijayo nitaondoka. Kaka wajanja karibia wanilize kweli, na nimepata hasara kubwa sana.
Kuna mtu aliniagizia vitu vya bei kweli, yaani ghali mno, na baada ya kufika akataka nimpe alafu alete hela baada ya siku mbili, kumbe hakuwa hata na senti tano.
Sasa mimi nikamwambia aje na hela baada ya siku mbili avichukue hivyo vitu vyake lakini aliporudi ikawa ni viswahili vingi kama kawaida baada ya kuniingiza kwenye hasara ya $5,900 na huyu ni mtoto wa wanaoitafuna hii nchi. Hii saa ni moja ya vitu nilivyomletea na ndiyo ya mwisho, vingine vyote imenibidi nigawe tu.
Niliinunua $1,050 ila nalazimika kuiuza chini na ambayo sina hata uhakika nitaipata. Naomba niweke hii kwenye blog ya jamii
LUXURY WATCH FOR SALE
State of the Art, Fully Automatic Luxury, Eco Drive Men's Leather Watch, is up for a grab.This is a brand new model (watch) that functions automatically, does not need a BATTERY replacement and can store energy for over 300 days. IT is fully automatic and one of the best money can buy. $799 or best offer
For questions contact mbezi1980@yahoo.com or 0713-842-329
Wewe ndio mjanja wa mjini unayetaka kutuuzia saa kwa maneno mareeeefu. Wala hakuna mtu aliyetaka kukuingiza mjini, wala nini. Hiyo ni gia yako tu ya kutangaza saa.
ReplyDeleteHata kama Bill Gates atanunua hiyo saa, mimi naona yatakuwa matumizi mabaya ya pesa zake. Saa nzuri zaidi na ya bei rahisi inapatikana.
Next time akili kichwani.
ReplyDeleteWabongo ni wataka makubwa lakini hawana pesa.wanapenda sana kuwa take advantage watu wanoishi nje.Atleast vitu unavyo.Lasivyo ungepigwa chenga mpaka siku ya kuondoka.
Sio mchina hiyo dogo?mmmmmmmm?
ReplyDeleteUnaleta UTANI na USD 799...what? that kind of watch for that money..wizi mtupu..u deserve kutapeliwa..or we tapeli nini..go visit.
ReplyDeletehttp://www.nextag.com/citizen-mens-eco_-_drive-leather-watch/compare-html
sorry ila wewe ni mpumbavu aisee,sinunui hiyo saa juu ya dola 200 aisee tena hapo nimekuonea huruma na tena iwe ya ukweli sio mambo ya china aisee,wakamate wabongo huko africa hao ndio mang'ombe utawakamua tu,siku njema ila usirudie tena aisee.
ReplyDeleteDo you think us Tanzanians are STUPID? Wewe tapeli tuu. See http://www.citizenwatch.com/COA/English/detail.asp?Country=COA&Language=English&ModelNumber=AT0910-00E
ReplyDeleteThis watch is Model AT0910-00E inapatikana kwa $295 before discount!!
Think Again,
Mdau
Ndanda, Ntwara.
duh pole sana mkuu kama kweli jamaa alikuagiza hivi vitu,nakumbuka ulitangaza pia ipad.wabongo usiamini kupeleka kitu kabla hajalipa advance.
ReplyDeleteDuh, kweli,bongo usanii, kaanza kwa hadith ndeefu utadhani kweli, afu anataka ingiza watu mkenge, saa hiyo hiyo (rangi,materials na brand name) ni dola &210, weka na usafirishaji haizidi $300.
ReplyDeleteAseme anatafuta ticket ya kurudia si kudanganya watu.
Nenda www.amazon.com uhakikishe mwenyewe.
Mdau
Sweden
Maelezo yako hayana kichwa wala miguu, inaonyesha hujui hata kutoa maelezo ya kitu ulichonacho sana sana unaongea neno automatic tu as if umetoka kulijua jana, huelezei functionalities zake unaishia kusema ni fully automatic, tueleze inaautomate functions zipi. After all, japo Watanzania wengi ni wapuuzi ila hakuna atakayefikia kununua hiyo saa kwa zaidi ya milioni moja. Saa ya nini wakati siku hizi kila sehemu kuna saa. watu wanamiliki simu tatu tatu, zote zina saa, computer zina saa, magari yana saa, Tv zina saa, radio zina saa hata minara barabarani ina saa. Huo ni mzigo tu, kwa kukusaidia saaaaana mimi ntanunua kwa buku 3 ili nimwachie mwanangu achezee.
ReplyDeleteNi nzuri sana, lakini duka lenyewe tu, ikisinzia nikutafute kwenye yahoo.com? anuani ya makazi ya kudumu, sio hoteli ni nzuri zaidi angalau hata kama nisipokupata naweza nikang'a kadirisha kufidia hasara.
ReplyDeleteKaka acha usanii hiyo saa haiwezi kufika $1000 mie ninayo kama hiyo nimenunua kwa $300 sasa unauza $700 ndio punguzo mh!!! huo ni utapeli ama kweli bongo siku hizi matapeli kinoma utafikiri tuko nigeria!!!
ReplyDeleteUmeshagawa $ 5000 nzima hiyo dola 1000 unashindwa nini kumalizia kuigawa!!!Natania tu.
ReplyDeleteAcha usanii wewe,Misupu itabidi akulipe huyu kwa matangazo.
ReplyDeleteyaani hii saa sijui kama inavalika maana mbona makorokoro mengi?ipo complicated sana!ila kila la kheri watajitokeza watakayoipenda ila kuwa makini na wasanii wasije wakakuzuga kama huyo wa awali!
ReplyDeleteMbezi 1980, sasa nitakupataje? do you ship to U.S. ?
ReplyDeletenimekuwa nakifukuzia sana hiki chombo, kweli mimi nina bahati.
anyway.
nitakupigia, tuongee.
= = =
Buffalo,
New York
Wewe kama unauza kitu just hit it straight no one want to hear those mambo jambo or yari yarie. Too much information is unnessary au ndo kama kawaida yako kinda of showing off huh?
ReplyDeleteMdau Bariadi
wewe john mashaka acha ushamba kwa nini usirudi nayo uiweke kwenye ebay hapo Bongo watu wamechoka hiyo asking price yako trust me you will never get it labda ingekua I-fone au Blackberry ndo wangenunua si unajua wabongo tunajulikana duniani for Talking big but walking small
ReplyDeleteMdau Silver Spring (discover Chanel BLDG)
Sasa wewe unataka kutapeli. Hizo saa hazizidi $150 amazon.com
ReplyDeletehivi ni biashara gani mnayoifanya badala ya kufanya vitu vya maana mnaendekeza nini sasa? kumbukeni kuna watu hapa hapa tanzania wanakufa na njaa hawanachakula nyie mnafanya nini hii sasa ? kuweni wastaarabu na waungwana mungu hapendezewi na kufuru mnazofanya sas hiyo saa ndio yakununua kwa pesa zote hiyo ? au ukivaa ndio haufi?
ReplyDeletejohn mashaka pole sana wabongo ndo zao wanapenda kulalia sana, ukianza kudai linazuka bonge la ugomvi yani usanii mwingi mno next time usilete kitu hata iweje utalizwa bureeee!!!je ankal umeipenda nikupige present ya ukweli?
ReplyDeletePole sana John Mashaka.
ReplyDeleteNdio maisha.
Huyu Bwana tapeli. Kwanini andanganya watu kwa kusingizia wanaotafuna nchi kumbe yeye ataka kuwatafuna wengine! Saa hiyo hata ukiende kwenye website ya COSTCO utaiona kwa dola $115. Yaani karibu laki moja sabini! Nchi yetu kila mtu anajaribu kumla mwingine!!!
ReplyDeleteuda mwengine haina haja kuanza Kuongelea Historia nzima wewe sema tu unaiuza basi kuhusu huyo mtu mwengine haina haja kumzalilisha binadamu mwenzako ndomana kila kitu kina majaliwa ya mwenyezimungu, Mungu atakusaidia utapata mteja mpya.
ReplyDeleteEbo!! Huyu jamaa kanitoa tongox2, tangu nimezaliwa maeneo ya Bukoba miaka 27 iliyopita sijawahi kuona saa ya bei kubwa kiasi hii, au ni ushamba wangu? Ila inaonekana leather yake ni kiboko.
ReplyDeleteNkyabo - Bongo
MZEE WA MBEZI SI USEME TU KAMA UMECHACHA NA UNAUZA SAA YAKO? KAMA HIVYO VINGINE ULIGAWA KWA NINI NA HIYO USIGAWE?? KAMA ULIWEZA KUGAWA VITU VYA THAMANI ZAIDI YA DOLLAR 4000 KWA NINI HIYO YA DOLLAR 1000 USHINDWE???? WACHA UJANJA MZEE WA MBEZI WABONGO SIKU HIZI TUMEAMKA....
ReplyDeletenA HIYO TOA KAMA ZAWADI AU TUNZA TU KUNA SIKU ITAKUSAIDA KUANGALIA MAJIRA!
ReplyDeletewewe acha wizi yaani dunia hii matapeli mpaka kwenye Michuzi Blog.
ReplyDeleteHiyo saa kwanza inaweza kuwa fake pili bei uliyotaja labda ndani waweke diamond. Bei yake hapa ukerewe ni £189 na nasema hivyo sababu hiyo saa mimi nimenunua na ukiongeza £18 unapata extra three year warrant ontop oif two manufacture warrant nenda migodini huko ukawaibie siyo hapa mjini.
Huoni hata aibu mpaka namba ya simu unaweka tapeli mkubwa
mdau ukerewe
Yaani brother mie ninayo saa kama hii nilinunua pale Washington DC mwaka juzi kwa USD 899,hiyo bei ni ndogo sana yaani nakutafuta sasa hivi nimpelekee house boy wangu.
ReplyDeleteThat is a non-sense ever advertisement ever seen in my entire life. Kaka Michuzi hebu zingatia masuala muhimu yanayohusu "Future" ya Tanzania na sio huu upuuzi wa bling-bling. Unajua mwenyewe tumetoka mbali, tangia enzi za "MIDO"- Mission Quartet.
ReplyDeletehivi we jamaa una akili kweli! wewe unafikiri mtanzania na ujinga wake anaweza kununua saa kwa sh milioni moja ina nini cha zaid au ina hotel ndani?mjomba hiyo utapiganayo picha tu
ReplyDeleteSAA ZIKO MPAKA ZA DOLA 3000 WATU WANANUNUA,ZINA WARANTY RISITI YENYE DETAIS ZAKO ILI UIWEKEE INSURANCE NA IKIWA NA TATATIZI UNAWEZA KUIPELEKA KWA DELAR YOYOTE DUNUANI.BADO NAKUMBUKA 1997 WAKATI RADO ZA MCHINA ZINAINGIA ZIEUZWA SANA SALAMANDER TSH 500.000.BUT THIS IS 21 MILLENIUM BRO.
ReplyDeleteAcha kutupiga changa la macho embu angalia bei yake http://compare.ebay.com/like/170537554875?ltyp=AllFixedPriceItemTypes&var=sbar
ReplyDeleteUS $162.
wizi mtupu!na wewe kaka michuzi usikubali matangazo ya kitapeli kwenye blog yako, Usijiharibie uaminifu wako
wadau wadau msibeke ovyo zameni google muanalie bei ya rolex, haki ya nani unanunua kiwanja sinza lo lo loooo!!
ReplyDelete