DEAR MZEE MWENZANGU,

NAOMBA MSAADA HAPO KWENYE MATAA!

HIVI TUME YA VYUO VIKUU (TCU) KUNA NINI? MTAKUMBUKA KUWA WAKATI ULE VIJANA WETU WANATUMA MAOMBA KWA ULE UTARATIBU WAO MPYA KULIKUWA NA MALALAMIKO MENGI JUU YA UPATIKANAJI WA MTANDAO WAO NA PALE UNAPOPATIKANA ULIKUWA SLOW SANA NA MARA KWA MARA ULIKUWA UNAKATIKA. WAKATOA VISINGIZIO KIBAO AMBAVYO HAVIKUWA NA MSINGI.

SASA ORODHA YA VIJANA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU IMETOKA. MIMI NILIKUWA NA NIA YA KUJUA KIJANA WANGU KAPANGWA WAPI ILA TOKA SAA MOJA ASUBUHI MPAKA MUDA HUU SAA NNE ILE ORODHA AMBAYO IPO KWENYE PDF HAIJAFUNGUKA, KAFAILI KADOGO TU KA KAMA MB1.5. MIMI KWA UCHUNGUZI WANGU AMBAO NAAMINI NI WA KWELI. SERVER YAO KIMEO, ISP WANAYEMTUMIA KIMEO NA WEB MASTER WAO KIMEO PIA.

NAWASHAURI KUWA WA-COPY HAYO MAFAILI WAOMBE MSAADA YAWEKWE KWENYE MITANDAO YENYE AKILI KAMA UDSM, SUA, MZUMBE NA HATA WIZARA YA ELIMU.

NAOMBA KUWASILISHA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. INAKERA, LISAA LA TANO SASA HAMNA KINACHOFUNGUKA, WAWAULIZE NECTA HUA WANATUMIA MBINU GANI WANAPOTOA MATOKEO YAO ONLINE

    ReplyDelete
  2. Ni kweli server yao ni kimeo kaka na tayari wamepeleka selection za vyuo tofauti kwenye website za vyuo husika. Angalia www.udsm.ac.tz ama www.udom.ac.tz na utapata matokeo ya kijana wako.
    Pole sana na ndo mambo ya serikali hayo kwenye masuala ya mtandao.
    Mdau Faustin

    ReplyDelete
  3. ITABIDI BONGO WAANZE KUFUKUZA KAZI WATU WAZEMBE...LABDA ITASAIDIA. MIMI NI SIKU YA PILI SASA NAJARIBU KUDOWNLOAD HILO PDF FILE LAKINI WAPI, SAA ZINGINE HATA TOVUTI YENYEWE HAIFUNGUKI aibu ! HII INAONEKANA NI HOST ISSUE, SIKU HIZI KUNA HOST HADI ZA DOLA 2/MONTH WANASHINDWA HATA HIYO??INABIDI WAJUE KWAMBA KATIKA KARNE HII, TOVUTI SIYO KITU CHA STAREHE, NI SEHEMU AMBAYO WATU WANAKWENDA KUPATA INFORMATION...AU LABDA WANATAKA LAZIMA MTU AENDE PALE ILI ATOE RUSHWA? ANYWAY, KWELI BONGO BADO.....btw ninatumia T1/E1, XP, Pentium4, IE 8

    ReplyDelete
  4. Hilo ni kweli mdau mimi pia bado nasubiri toka jana jioni!. hata NECTA walikuwa na tatizo kama hilo siku za nyuma, wakalirekebisha. TCU rekebisheni kero hiyo haraka tafadhali, au waombeni wizara ya elimu, au hata faculty of education pale UDSM watawawekea bure chapchap!

    ReplyDelete
  5. Ukweli mtupu nilifikiri mwenye ghadhabu na hawa watu insensitive niko peke yangu. Seriously kuna haja ya huyu webmaster au whoever responsible ku-create mirrors nyingine au kutumia web za vyuo vingine au hata ya wizara ya elimu ya juu. Kafaili kenyewe ni 1.24Mb tu lakini hakashuki wala nini afu hapo ni kwamba umepata bahati kwamba web pia im-load vizuri hadi ukafika huko. Will someone do something?
    Ila mnaweza kwenda udom.ac.tz, saut.ac.tz, and mwuce.com kwa walioomba vyuo hivyo.

    ReplyDelete
  6. Ni kweli..., naungana na mdau hapo. Iweje website ambayo inakuwa accessed na watanzania walio wengi iwe inaleta shida kiasi hicho? Issue ya ku-download file dogo tu inaweza kukuchukua masaa 8 au zaidi. Huo ni kutokuangalia na kuboresha network infrastructure zao. Huenda wana bandwidth ndogo hivyo sisi tunaotaka kujua matokeo ya ndugu zetu tunanyang'anyiana hiyo bandwidth yao ndogo. Tunashauri kama watanzania tunapenda kuona maendeleo, wajiangalie na waboreshe huduma. Sio hatia kusikiliza feedback za users wa system yako. Customer satisfaction haipo katika private organizations tu hata Government Institutions zinahusika.

    ReplyDelete
  7. Kama unafanya trace kwa kutumi website hii http://network-tools.com/ utagundua wahusika wamechemshia wapi. Inaonekana wamepiga shorcut katika kufanya hosting na vile vile wamekosea kukadiria bandwidth waliohitaji. Kuhost website nje ya Tanzania kwenye server za uhakika zenye bandidth kubwa ni $10 kwa mwezi. Siajabu kuna fedha zimeliwa na wanaogopa kurekebisha. Swallow your pride and be responsible, jamani!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...