Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. Nchi ya Tanzania mambo mengi yana fanyika kienyeji zaidi. Ni kinyume cha sheria kwa raia wa kigeni ( au Mtu asiye raia wa Tanzania na taasisi za kigeni wakiwemo nchi, mashirika ya kigeni au yale ya UN na taasisi zake) ku-kampeni au kushabikia vyama vya siasa.

    Huyu Dada Ki-Kenya kama mnavyo mwona akijisheuwa unaona kabisa ni kilaza juu hili. Na Serikali yenyewe pia imevunja miiko na maadili ya kampeni kwa kumwalika raia wa kigeni kupanda jukwaani na kushabikia CCM. Na hii inaonyesha kuna wengi kama yeye ambao hata kupiga kura hiyo Octoba 31 si ajabu.

    Hii inatia kichefuchefu.

    Ni hayo tu.

    ReplyDelete
  2. Just one word for you lil girl, STUPID!!!!!
    Cant you talk sense? Eti JK ni handsome, so what?? Inakusaidia nini kwamba Jk ni handsome? Wake up wasanii!! Ungesema ukweli tuu kwamba ni njaa inayokuweka hapo!! Ngoja kampeni ziishe tuone kama JK ataendelea kuwa handsome wakati hakuna mtu wa kukaa na kusikiliza upuuzi unaoimba!!
    GROW UP!!

    ReplyDelete
  3. Tunavyopinga vitu tuwe na uelewa wa kutosha ili isionekane kama sisi ni mabingwa tu wa kulalama wakati wote, manaudhi!

    Hata vitu vidoooogo kama usanii mnashindwa kuelewa! Mnajuaje huyo ni raia wa kigeni? Huyo ni Mtanzania halisi na hiyo ni staili yake tu ya kuigiza, au kwa vile kasema alienda Nairobi?!

    ReplyDelete
  4. Nyinyi washabiki wa chadema (cha mgema) wacheni ujinga wenu. Mtu yeyote ana uhuru wa kusema anapenda chama gani. Pili, wacheni kutukana kila mtu ambaye hamuungi mkono mbowe. Hamna sheria yeyote inayosema kuwa mtu wa nje hawezi kusema anakipenda chama gani. Toeni sera na si matusi. Sisi wanaCCM hatuwaogopi wala hatuogopi nguvu zenu za soda. Kwanza jibuni: kina mbowe walipata vipi utajiri wao wakati wa awamu ya kwanza (enzi za ujamaa)? na phd ya slaa ni ya nini??? CCM tuko imara.

    ReplyDelete
  5. mijitu mingine kwa kukurupuka sasa aliyewaambia Dokii ni mkenya naniii? watu kujfanya wanajua mambo kumbe zero pumbavu kabisa, huyu dame hana hata tone la damu ya kinyenya ni lafudhi ya kikenya amabyo amekuwa akiitumaia kwenye michezo yake.

    ReplyDelete
  6. HUYU DOKII KACHANGANYIKIWA MARA ULOKOLE MARA SIASA....UKISIKIA MTU KICHAA NDIO UKO

    ReplyDelete
  7. JAMANI HUYU BINTI KACHANGANYIKIWA.. ILA MULOPITA HUYU SI MKENYA NI MTANZANIA DOKII NI JINA LA USANII NI MPOGORO HUYO WA KILOSA/KIMAMBA HANA LOLOTE. UNADHANI JK NDO ATAKUJALI UKIMALIZA HAPO... WE KAMATA HELA URUDI KILOSA UKALIME

    ReplyDelete
  8. Dokii si mkenya ni mbongo sema tu anaigiza kama mkenya na hapo ameongea kama dokii na sio kama Ummy ila kwa mashauzi ndio mwenyewe na she is also stupid!

    ReplyDelete
  9. Weweee DOKII wape wape vipande vyao! Huyo ndio Dokii wengine wote photocopy.

    Nyie nanyi si angalau mngeuliza kwanza huyo Dokii ni nani? Eti Mkenya mamluki? Mtu hata watoto wadogo wa chekechea wanamjua! lol! Mama mbavu zangu weee! Huyo Mpogoro kawa Mkenya leo! Haloo haloo haya pelekeni pingamizi lingine kwa Tendwa haya tumeni haraka wanasheria wenu wakamwekee pingamizi Dokiii! Uuuwi uuwi inawezekana kuwa nyie ndio mamluki maana hata hamjui Tanzania kinaendelea nini. Haya maboksi mema bandugu!

    Mwisho mtasema waimbaji wa Twanga nao ni Wakongo! haluu!

    ReplyDelete
  10. Pelekeni wanasheria wenu pori huko hata ToT walishawahi kwenda nchi jirani kufanya kampeni. Nyie mnaishi dunia gani. Au ndie wale aliens hawajui kinachoendelea duniani? Kwa taarifa yenu kwanza Dokii sio jina lake ni jina la kisanii, na hapo alipo ndiko kwao Morogoro, do your research first kabla hujaja kuonyesha ignoramus yako!

    ReplyDelete
  11. Michuzi nae akiikampenia CCM,Mbona hatujaona hata siku moja ukitangaza uzinduzi au tamasha la Dokii kwenye bulogu yako? Wasanii nao uelewa mdogo sana ndio maana hatuachi kuiba kazi zetu maana 2005 mliahidiwa mambo mengi sana miaka 5 imepita bado mpo katika mazingila yale yale, mnatumika tu, nasema hatutoacha kuwaibia kazi zetu kwani nyie ni wasanii na sisi wasanii na mnaowapigia kampeni ni wasanii vile vile

    ReplyDelete
  12. Pamoja na kuwa aliyoongea mengi ni pumba tupu, huyu dem si mkenya kama baadhi ya wadau wanavyodhani. Huyu ni Mtanzania isipokuwa umaarufu alioupata umetokana na yeye kuigiza kama Mkenya. Nadhani labda naye pia anapenda atambulike hivyo.

    Hata hivyo, ninashangazwa na kauli za watu ambao mi nilidhani wangetusaidia kubadilisha hii nchi lakini wanayotueleza ni utumbo mtupu. Kama wasanii wetu ndo wana mawazo haya, je wataweza kweli kutatua hata matatizo yao wenyewe? Ndio maana kila siku wanalalamika kuibiwa na wadosi huku wenyewe wakitegemea fadhila za watu mbalimbali kama wanasiasa kuishi. Si kosa lao hata hivyo. Wasanii wengi wamelazimika kufanya sanaa baada ya kushindwa maisha maeneo mengine.

    Tusikate tamaa lakini, hawataweza kutudanganya milele. Tanzania yenye watu wenye akili inakuja!!!

    ReplyDelete
  13. Acheni kubwabwaja sana bana mna uhakika huyu msichana ni mkenya?huyu ni msanii na hiyo accent ya kikenya ni ana act na toka zamani tu acheni kutuzingua bange! Halafu isitoshe kila mtu ana uhuru wa kushabikia chama gani hii mambo ya kutaka kila mtu aende huko mnakotaka haiko mahali yeyote mazee! Asanteni

    ReplyDelete
  14. Hapo juu! nyie ni waTZ AU? nani kasema dock ni Mkenya. huyo anaigiza sauti ya Kikenya yeye ni mtanzania halisi hapo anaonyesha usanii wake na anawakilisha umbumbumbu wa wasanii wetu kama MARLWA, tmk etc ambao wanatunga nyimbo kuimbia CCM wakati album zao zinaliwa na wadosi bila kikwete na serikali yake kuwatetea. DOCK NI MPOGOLO WA IFAKARA AU KILOSA HANA NASABA AU DAMU YOYOTE YA KIKENYA.

    ReplyDelete
  15. Hee nyie watu hapo juu, nani kawaambia kuwa dokii ni mkenya? hamumfahamu nini? au nyie ndio mlikimbia nchi kitambo?

    ReplyDelete
  16. Tarehe Tue Sep 07, 03:16:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymo

    umeongea kweli dada njaa huyu !!

    ReplyDelete
  17. Hakuna uvunjaji wowote hapo. Hiyo ni lugha tu ya kazi ya usanii iliyotukuka.
    Na kila mtu ana uhuru wa kupigia debe chama akipendacho waziwazi.

    wake up, Ummy si askari wala mtumishi wa ngazi fulani serikalini.

    Binti Wenslaus, mazee tuendelee kuandikiana:
    umkhontho2@hotmail.com

    ReplyDelete
  18. Sasa wewe Mkenya, Kampeni inakuwashia nini ya CCM, kweli hii njaa .Tuwachie wenye nchi au Ukenya wa makaratasi???

    ReplyDelete
  19. nafwa hukuuu wewee dokii ni funga kazi lol! ha ha haaaaaa!

    ReplyDelete
  20. nyie wadau hapo juu mtakereka sana huyo dokii ni mbongo sema amekulia kenya, kama hamkuwahi kutizama maigizo luningani enzi hizo akiwa mduuchu tajijuu, na huyo raisi wenu mtarajiwa mwizi wa mke wa mtu!!

    ReplyDelete
  21. huyo dada ni mtanzania sio mkenya. ila akili yake anaijua mwenyewe. no sense

    ReplyDelete
  22. Dokii kweli kilazi anamfagilia rais eti handsome nimecheka mpaka basi kwa mpango huu tutafika kweli kama wafikisha meseji wataenda na sera za uzuri. Anyway Mungu bariki Tanzania naamini iko siku na itafika tu watu watafunguka.

    ReplyDelete
  23. chakula ya mtu ndani ya ccm

    ReplyDelete
  24. Dokii ni Mtanzania kwa baba na mama. Kama hamjui kitu ulizeni!!!!

    ReplyDelete
  25. Upungufu wa chembechembe za kufikiria mwilini

    ReplyDelete
  26. Dokii na Marlaw njaa tupu.

    ReplyDelete
  27. Chakula ya nani hii?

    ReplyDelete
  28. Kwa nini mtu aki-support CCM wapinzani lazima watukane. Inaonyesha kuwa hao wapinzani si waumini wa demokrasia na wako desperate sana. Lakini sisi hatuwaogopi. Matusi ni ala ya mshenzi. CCM hatutukani wapinzani. Tutashinda tu watake wasitake. VIVA CCM.

    ReplyDelete
  29. huyu dada ni pure mtanzania....if u listen careful u can pick up kwamba ni mtanzania....usiache mbachao kwa msala upitao....ulishasikia mkenya anasema hivyo. people use ur head to think

    ReplyDelete
  30. Sishangai kuona watanzania mnaanza kutajana kwa utaifa na ukabila mpaka pingamizi kwenye uchaguzi wa mwaka huu kila mtu anamtaja mwenzio kama siyo rahia na dhambi hii imeanzia kwa General Ulimwengu sasa inakuwa taratibu kama kansa ya matiti, nimesikitika sana katika kata kijiji kagondo kata ya kagondo jimbo la Bukoba mjini mgombea wa ccm kamwekea pingamizi mtoto wa kaka yangu kuwa siyo raia, lakini mgombea huyu mama yake ni mtanzania wa mpakani na baba yake ni mganda, sisi ukoo wetu mpaka leo hii tuna vizazi saba sasa yupu siyo raia kati ya hawa wawili? nampongeza msimamizi wa uchaguzi alikataa pingamizi lakini hii inatia doha ukoo wa watu wanao jiheshimu katika jamii yetu, wanasiasa kuwa waangalifu.
    Mdau uk

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...