Mbwana Assa Mbwana (pichani juu), jana aliibuka mshindi wa saba katika mashindano ya 14 ya kimataifa ya tuzo ya kuhifadhi Qur’an (14th Dubai International Holy Quran Award – DIHAQ). Mashindano hayo ambayo ni makubwa na magumu ya kuhifadhi Quran hufanyika kila mwaka wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kushirikisha washindani kutoka nchi mbalimbali. Mwaka huu ni mwaka wa 14 tangu yalipoanzishwa.
Tanzania imewakilishwa na Kijana Mbwana mwenye umri wa miaka 16 mzaliwa wa Wingwi Pemba ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Kiislam Vikindu mkoani Pwani. Mbwana alikuwa ni miongoni mwa washindani 78 kutoka nchi mbali mbali duniani ambapo 4 walishindwa katika hatua za awali.

Mashindano hayo huambatana na tuzo mbalimbali ambapo mshindi wa kwanza alijinyakulia kiasi cha $70,000/-; wa pili $55,000/-; watatu $40,000/-; na waliobaki kati ya $20,000 – $10,000.

Orodha ya nchi washindi kumi wa mwanzo ni:
1. Algeria (Mlemavu asiyeona- Amehifadhi kwa Braille/tapes)
2. Bangladesh
3. Bahrain
4. Egypt
5. Yemen
6. Libya
7. Tanzania
8. Saudi Arabia
9. Kuwait
10. Morocco na Sudan (Wamefungana)

Ubalozi wa Tanzania UAE na Jumuia ya Watanzania wanampongeza kijana Mbwana kwa kuliwakilisha vyema Taifa letu. Hii ni mara ya kwanza kwa Mtanzania kufanikiwa kuwa miongoni mwa washindn kumi wa mwanzoni, miaka iliopita Tanzania imekuwa ikishiriki lakini haijaweza kufanya vizuri na kuishia daraja la chini sana.

Jumuiya ya Watanzania UAE ilimpa kijana Mbwana tuzo ya Ngamuzi Mpakato (Laptop Computer) pamoja na simu ya kiganjani. Pia ilimpa tuzo ya simu ya kiganjani Ustaadh Jumu Mfaki Mohamed ambaye ni Mwalimu wa Mbwana ambaye aliambatana naye kwenye safari ya Dubai.

Mbwana akikabidhiwa Ngamuzi Mpakato (Laptop Computer) na Bw. Ali Saleh, Consul General wa Tanzania ndani ya Dubai na Falme za Kaskazini za UAE na kulia ni Ustaadh Jumu Mfaki Mohamed.Picha ya pamoja na Consul General, baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Watanzania UAE na Watumishi wa Ubalozi Dubai.Picha ya pamoja na Consul General baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Watanzania UAE na Watumishi wa Ubalozi Dubai.
Mbwana akiwa na Ustaadh Jumu pamoja na baadhi ya Watanzania waliohudhuria siku alipotangazwa miongoni mwa washindi.








































Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. Mashallah,mwenyezi mungu akuzidishia.hongera pia kwa wazazi wako.jitahidi pia na shule upate master.tunataka vijana walosoma na dini na dunia waje kuongoza vyombo vya kiislam,kama bakwata.ili tuone maendeleo.

    ReplyDelete
  2. MashaAllah, hongera saaana Mbwana. This is so so inspiring ... Mungu atujaalie na sie tuiweke Qur'an vifuani inshaAllah na hatimaye tuishi kwa mujibu wa maandiko yake Allah Kareem.

    ReplyDelete
  3. Mashallah tujitaidi watanzania kunyanyua dini yetu hongela kijana uwe mfano kwetu

    ReplyDelete
  4. Mashallah,

    Hii ni dalili njema kwa kijana wa KItanzania kuonyesha umahiri wake. Kwa hakika hii ni heshima kwa Waislamu na Tanzania kwa ujumla wake.

    Hongera kijana na Hongera wote waliochangia kijana wetu kufanya mambo makubwa. Uusia wangu, BAKWATA na WaTZ wengine tuhakikishe tunajipanga vyema ili kufanya makubwa zaidi katika uislamu katika siku zijazo.

    Mdau.

    ReplyDelete
  5. Hongera kijana. Kwa sie tuliosoma Madrasa za kuunga kuunga this is inspiring. Piga sasa Ilmu dunia ili uweze kuwa advocate wa waislam ile kiyenyewe. Allah atakuzidishia InshaAllah.

    ReplyDelete
  6. mashallah! mungu akubariki. hongera kwa wazazi na ustaadh. uislam huyu kijana ni wakuakikisha anapata elimu zote mbili. jamani wafadhili msimuache hivi hivi.

    ReplyDelete
  7. MashaAllah, big up mwana.Speed ile ile.Tumia zaidi zako katika njia sahihi .Inshaalah ALLAH jaria wapatikane vijana wa namna hii katika jamii zetu,amiin

    ReplyDelete
  8. jamani tusichanganye dini na serikali. Kwanini balozi inatoa pesa za walipa kodi kununua laptop kwa ajiri ya mshindi wa kusoma quran? naomba nisieleweke vibaya kazi za balozi sio hizo

    ReplyDelete
  9. MaashAllah! Allah akuzidishie, hongera sana.

    ReplyDelete
  10. NIMEFURAHI KUFAHAMU KUWA LAPTOP COMPUTER KWA KISWAHILI INATWA NGAMUZI MPAKATO.

    ReplyDelete
  11. KINGAMUZI MPAKATO, kiswahili chakolea (yaelekea maneno yasiyo tata yameisha). Hakuna neno lenye maana ya moja kwa moja mpaka tutumie maneno ya kuunga unga. Basi tukope kwenye makabila yetu.

    ReplyDelete
  12. mabruk ya Allah....mbwana im proud of you umetuwakilisha vyema...kuzipita nichi kama saudi na nyingine ambazo zina msingi mzuri wa kufundisha quran..well done
    Na hii inaonesha kuwa tukii marisha misingi ya kufundisha watoto dini basi tunaweza kupata waalim wazuri wa dini

    ReplyDelete
  13. Hongera sana Allah akuongezee zaidi na zaidi na iwe chachu kwako kuwafundisha na wengine. Hongera!

    ReplyDelete
  14. Mashallah, hongera sana kijana

    ReplyDelete
  15. Najua hutatoa maoni yangu lakini poa tu!
    Ila ndio maana ya demokrasia, weka maoni hata kama hukubaliani nayo, au sio?

    Ukristu na Uislamu uliletwa kwetu waafrika ili waweze kututawala kwa ulaini.
    Walituteka in the heart and mind.
    Kabla hawa wenye hizi dini kutuletea tulikua na dini zetu, wakasema eti tunaabu mashetani! Na sisi hatukua na jinsi ila kufuata wakoloni na waliotufanya watumwa, walitufanyia unyama na ushenzi wa kila aina.
    Hamuoni ni wakati tukajikomboa na utumwa wa dini za watu?
    Sio kwamba wao walioleta wanazifuta tena anyway.
    Hebu angalia dini zilivyoambata na siasa, kutugombanisha kila kukicha.
    Hebu tufikirie jamani?

    ReplyDelete
  16. JAZAKA LLAAHU KHAYRA KIJANA MBWANA ALLAH AKUPE UMRI MREFU NA AKUJAALIE IDUMU QUR AAN KIFUANI MWAKO KWA MUDA WOTE UTAKAO ISHI KTK ULIMWENGU HUU,ALLAH AWAPE KILA AINA YA FAIDA NA MAFANIKIO WAZAZI WAKO WEMA MAASHALLAH AAAMIN

    ReplyDelete
  17. wewe ulielaumu ubarozi hovyooooooo.kwani huyo balozi si msilamu? pesa za walipa codi zinatumiwa kwa mafisadi. kununulia zawadi ya laptop kuna ubaya gani na walipa codi nao wapate baraka kulikoni pesa zao zikitumiwa kwenye ufilauni.
    nangoja kusikia kaalikwa IKULU mana hasipoalikwa haitokuwa vyema wanaalikwa wanaovaa vichupi miss TZ na wanamuziki wa bongo flavor.
    mwaliko wa kijana ndo wa mahana.

    ReplyDelete
  18. Mimi ni mkristu lakini sioni kuwa ni shida balozi kununua laptop.

    Kuna suala la PR ambalo halibagui imani wala tamaduni. Ndio sababu pesa za walipa kodi za wenzetu waislamu zinatumika kuwanunulia bia na wines viongozi mbalimbali kinyume na lengo la walipa kodi na hata kinyume na uislamu.

    Wakristu tuna asili ya ustaharabu so kuuliza pesa kununulia laptop ni matumizi mabaya ya blog na techonojia ya internet.

    Toa constructive hoja na sio zenye kuonesha tofauti zetu kiimani. Wamepewa zawazi wacheza vibisa, wanenguaji, wanamiziki, wanywa bombe nk hivyo sio mbaya kupewa muislamu.

    ReplyDelete
  19. maashallah maashallah......huu ni mfano bora kabisa wa kuigwa na jamii zetu na watoto wetu kwa ujumla....mwenyezimungu akujaze kheri wewe Mbwana,wazazi wako, maalim wako na kila aliochangia kwa kuweza kufikia hapo.....hakuna kilicho bora zaidi ya qur-an kulala kifuani mwako na huo ndio utajiri wa hapa duniani na akhera inshl

    ReplyDelete
  20. Stephen Hawking says universe not created by God

    • Physics, not creator, made Big Bang, new book claims
    • Professor had previously referred to 'mind of God'

    Adam Gabbatt
    * The Guardian, Thursday 2 September 2010

    Stephen Hawking Spontaneous creation is the reason there is something rather than nothing, why we exist, says Stephen Hawking. Photograph: Bruno Vincent/Getty Images

    God did not create the universe, the man who is arguably Britain's most famous living scientist says in a forthcoming book.

    In the new work, The Grand Design, Professor Stephen Hawking argues that the Big Bang, rather than occurring following the intervention of a divine being, was inevitable due to the law of gravity.

    In his 1988 book, A Brief History of Time, Hawking had seemed to accept the role of God in the creation of the universe. But in the new text, co-written with American physicist Leonard Mlodinow, he said new theories showed a creator is "not necessary".

    The Grand Design, an extract of which appears in the Times today, sets out to contest Sir Isaac Newton's belief that the universe must have been designed by God as it could not have been created out of chaos.

    "Because there is a law such as gravity, the universe can and will create itself from nothing," he writes. "Spontaneous creation is the reason there is something rather than nothing, why the universe exists, why we exist.

    "It is not necessary to invoke God to light the blue touch paper and set the universe going."

    In the forthcoming book, published on 9 September, Hawking says that M-theory, a form of string theory, will achieve this goal: "M-theory is the unified theory Einstein was hoping to find," he theorises.

    "The fact that we human beings – who are ourselves mere collections of fundamental particles of nature – have been able to come this close to an understanding of the laws governing us and our universe is a great triumph."

    Hawking says the first blow to Newton's belief that the universe could not have arisen from chaos was the observation in 1992 of a planet orbiting a star other than our Sun. "That makes the coincidences of our planetary conditions – the single sun, the lucky combination of Earth-sun distance and solar mass – far less remarkable, and far less compelling as evidence that the Earth was carefully designed just to please us human beings," he writes.

    Hawking had previously appeared to accept the role of God in the creation of the universe. Writing in his bestseller A Brief History Of Time in 1988, he said: "If we discover a complete theory, it would be the ultimate triumph of human reason – for then we should know the mind of God."

    ReplyDelete
  21. A response from British author Pat Regan

    Ok Stephen – first define what you call “God”!

    I have a sneaking feeling that Stephen Hawking seems to miss the important fact that everything has its own form of intelligence, its own essential essence.
    The insightful ancients realised this and gave everything and every action a tutelary deity. Life forces that impinge on any given being or object shape it into what it ultimately becomes.
    Sadly like many materialistic experts in their given fields, Hawking is blinded by his restrictive scientific limitations therefore he apparently misses out on a lot of what is right in front of him.
    I have a strong sensation that, one day in the far off future, humanity will start to peel away the layers of misunderstanding. We shall then realise that the intelligences residing in all things are not simply physical interactions between opposing forces but the footprints of the gods.
    We are in a similar position when we seek to understand the marvel of creation. It is there in front of us yet we can only see a diminutive part of the entire situation.
    Our Pagan ancestors gave each mountain, stone, tree, lake, hill and river its own tutelary spirit or deity. This spiritual concept is of course not only peculiar to the Gaelic or Brythonic (British) Celts, other Pagan races too viewed the world in a similarly parallel manner.
    Temples to each deity were commonly erected by the Roman peoples who fully realised the advantageous necessity of connecting with these vital aspects of divinity.
    Today, the old gods/goddesses and spirits given as patrons of natural things have largely been demoted by the all-conquering Church into lesser aspects such as saints, fairies, heroes or demons. The essential male/female spiritual balance has been eroded into an allegedly all powerful (and of course male – oriented) being, commonly known as “God”!
    Yes Stephen– things are not always as they at first appear, especially when the concept of “God” is added to any suitable equation.
    And concerning the top scientific brains, I feel that rather than them making asinine comments about what, or what not, the creative process really is they would do better to actually admit in the first instance that they are restricted by their own limited intellect and comfortable contemporary life styles.
    This way we have a fresh starting point and can keep an open mind about their public deliberations on “God” and creation etc.
    Alternatively, if Professor Hawking is being critical of the world’s mind-controlling, monotheistic faith systems then I can appreciate this fully and salute his efforts.
    For far too long established orthodoxy has successfully indoctrinated the masses on an immense global scale.
    Therefore if Professor Hawking is wishing to be taken seriously about the Big Bang, Creation etc then he must primarily tackle the concept of what “God” is supposed to be!
    Adonis, Attis, Osiris etc.
    Hawkins is therefore amazingly giving us an equivalent sparely constructed choice of God or Science. Can you perhaps see the similarity, which is possibly further evidence of the good professor’s limited capacity in this instance?
    Politicians, Scientists and the ruling Priesthoods have always been quick to give us their own tainted versions of the so-called Truth with their inherently limited choices, and this situation seems to fit the bill very well indeed.
    The old Evolution v Creation controversy will rage on with irate religious fundamentalists banging their heads against the wall with the scientists along side, kicking back.
    I believe that until we clear this matter up properly we cannot take the professor’s views that seriously.

    ReplyDelete
  22. Mashaallah kijana Mbwana. MwenyeziMungu akujaalie kila la kheri na ung'are pia katika elimu dunia. na hii iwe changamoto kwa wengine sie ambao hatuna elimu ya Quran tujitahidi kuitafuta kwa hali na mali kwani ni bora mno hapa duniani na kesho akhera.

    ReplyDelete
  23. Tarehe Fri Sep 03, 12:40:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Nakuunga mkono, mimi mkristo lakini sioni shida ya balozi kutoa hiyo zawadi ya laptop kwa kijana, huyo jamaa anayepinga naona kashindwa kuandamana kupinga ufisadi bongo, au ni sawa lkwa fedha za serikali kununullia mitambo ya kutayarishia mziki? ni sawa kuwapa nafasi wanaotembea na vichupi?

    Acha ubaguzi na wala watanzania hatupo hivyo hizi dini hazituzuii tusijumuike yakati nzuri wala mbaya

    ReplyDelete
  24. marshaallah hongera sana ndugu yetu

    ReplyDelete
  25. MAsha ALLAh, Mwenye Ez Mungu akuzidishie wewe na vizazi vyote vya kiislam, ALLAHUMMA AMIn...sasa ujikite katika Elimu ya Dunai as said before ili uwe mfano mzuri kwa watoto wengine wa Kiislamu,..ALLAHUMMAAMIN..

    ReplyDelete
  26. ni kingamuzi ama king'amuzi??

    ReplyDelete
  27. Mashaallah Mbwana mola akuweke na akuzidishie fahamu na imani ya uislam inshallah, nasi tunatamani tungekua kama wewe ila ni majaaliwa yake Allah (SW).
    Nakuja kwenu waosha vinywa mnaokerwa na uislam, hivi serikali inaposaidia makanisa mbona waislam hatulalamiki iweje ubalozi kumzawadia kijana laptop iwaume mpaka mnatoa cheche za moto midomoni mwenu, suala la imani kama halikuhusu usilitie mdomo, waachie waislam wenyewe. na huo mwanzo mtalia sana itakapoanza mahkama ya kadhi.
    Hongera shemegi yangu Suba kwa kua mdau, mungu atakupa kheri zako na wewe. michuzi usiibanie hii.

    ReplyDelete
  28. upumbavu mtupu badala ya kutuandikia watu wamefanya mambo scientifuc watuonesha mambo ya dini sisi ya nini..haya mambo ya waarabu hayana maana yoyote sana sana kijana atajiingiza mambo ya kigaidi tu na kujiua kama kawaida ya quran inavyofundisha

    ReplyDelete
  29. wewe unaelaumu kuwa huyu mtoto kupewa LAPTOP na ubalozi wa tanzania ....unaishi katika dunia gani wewe, kwanza kama ni mtanzania unatakiwa ujigambe kifua mbele kuwa huyu kijana wetu katotangaza ulimwenguni kuipepea bandera ya tanzania katika mashindano haya magumu na nchi ambazo asili yao ni lugha hio ya kiarab
    pili ujuwe kuwa kwa alivyofanya huyu kijana sio ubalozi kumpa laptop tu ...kuna hata watu binafsi wengi sana tu wanaweza kutowa laptop kwa huyu mtoto kama wewe limbukeni kiasi hicho wa laptop mpaka wakati huu bora unyamaze kimya
    kwani naungana na wengine wengi waliosema kuwa pesa nyingi zinatumika kwa mambo ambayo hayana hata maana leo imefikia hadi wanamuziki wanakula pesa ya taifa je hii wewe haikuumi, au inakuuma hii ya laptop tu wewe ...nnaimani unasababu zako za kibinafsi kama si kidini itakuwa ni zakisiasa na ukumbuke kuwa hapa tunaangalia nini kakifanya huyu kijana wetu sio ubinafsi wako ambayo ni wakiroho mbaya na kimaskini na hautakupeleka popote wewe zaidi kukuangamiza na roho yako ya kimaskini
    huyu kijana kama ingekuwa katoka nchi za wenzetu siku ya kurudi tanzania angepokewa kama mfalme na kuenziwa ili adumishe na kuwahamasisha wengine kwani jambo alilolifanya sio lakawaida
    na binafsi nataka nifuatilie hili suala kiundani kama hakualikwa IKULU huyu mtoto basi bi wazi kuwa hakufanyiwa uadilifu kwani ikulu wanakaribishwa watu walokuwa hawana mbele wala nyuma
    huyu kijana ni dhahabu na niwakumtunza serikali ya tanzania na kuwa karibu nae ili aendelee zaidi kwa manufaa ya taifa zima la tanzania sasa WEWE unaezungumzia suala la huyu kijana kupewa LAPTOP ..nahisi kuwa wewe umepungukiwa na akili au hujui watu wanazungumzia nini katika mada kama hii ya kuiwakilisha NCHI ..iangalie picha yake pembeni kuna bendera ya taifa hapo sasa wewe huoni faghari kuiona bendera ya nchi yako ikipepea nje ya nchi yako na iko juu ya bendera nyengine ambazo kimtazamo nikuwa wanatupita kwa kila hali,
    wewe mtowa mawazo na roho mbaya ya kimaskini jifunze kuishi na towa tofauti zako za roho kwenye kuutangaza UTANZANIA

    ReplyDelete
  30. MIMI SI MPENZI WA KUTOA MAONI KWENYE BLOG,ILA HUYU BWANA ALIYEONA UBALOZI WA UEA KUTOA LAPTOP NA SIMU NI KWA KIJANA ALIYELIWAKILISHA TAIFA LA TANZANIA NA HATIMAYE KUIBUKA MIONGONI MWA WASHINDI KUMI WA MWANZO NI KOSA,BASI MASIKINI WA MAWAZO,YEYE SABABU TU SI MUISLAMU BASI KWAKE IMEKUWA SHIDA,HIYO LAP TOP NA SIMU NI TSH NGAPI?JE,NI TSH NGAPI ZA WALIPA KODI HUTUMIKA VIBAYA NA HAJAWAHI KUHOJI?MWALIO FISADI NJI SI YEYE HUYO HUYO ANAYE WAPIGIA DEBE KUWA RUDISHA MADARAKANI?WATANZANIA TUBADILIKE,BALOZI ANA MAMBO MENGI LIKIWEMO HILO,ACHA USHAMBA,NA UDINI,HAUTA KUFIKISHA POPOTE.
    KIJANA HONGERA SANA.MUNGU AKUJAALIE UWE NA AFYA BORA MAISHA MAREFU NA UENDELEE KUSOMA NA KUHIFADHI KURAAN ILI BAADAYE UWEZE KUWARITHISHA JAMII

    ReplyDelete
  31. mimi sina dini, huyu kijana kupewa laptop na ubalozi ni sawa kabisa, lazima tuwazadi vijana wetu kwa sababu hapa anawakilisha TZ hata kama angekuwa mristo,baniani,isamailia nk kama jamaa kajitahidi kukariri dini yake. najua kuna wakristo wengi wataelewa vibaya just get over it!!!!

    ReplyDelete
  32. Alhamdulillah! Kijana ushindi huu ni picha halisi kiasi gani wazazi wako walitia msisitizo katika kukulea katika maadili ya kidini, pamaba usikate tamaa inshaalah mwakani utashika nafasi yakwanza. wish you all the best.

    Ramadhani karim

    Chef Issa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...