Chifu Mwailemale (Ridhiwani Kikwete) akiwa amekalia kigoda baada ya kutawazwa kuwa chifu wa kinyakyusa.
Machifu wa kinyakyusa Ernest Mwailemale (kushoto) na Glasswell Mwakalukwa wakimvisha golole,Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa,Ridhiwani Kikwete, alipotawazwa kuwa chifu wa kinyakyusa na kuitwa Chifu Mwailemale juzi katika mkutano wa kampeni za ndani za kuweka mikakati ya kuipatia CCM ushindi wa kishindo,juzi katika Kata ya Ipinda, Kyela.
Chifu Mwailemale (Ridhiwani Kikwete) akihutubia baada ya kutawazwa kuwa Chifu wa Kinyakyusa.
Chifu Mwailemale akishangiliwa alipokuwa akikhutubia baada ya kutawazwa kuwa chifu wa kinyakyusa.Picha na Richard Mwaikenda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Duh..bongo mpaka raha..kuna vitu vingine inabidi ucheke tuu.....

    This pictures and accompanying explanation has made my morning jamani...

    ReplyDelete
  2. Kama kuna watu wanaonisikitisha hapa kwetu Tanzania ni hawa wanaotawaza watu kuwa machief wa makabila yao wakati hata hawana uhusiano na kabila lao lakini ni kwa sababu tu ya siasa au kupewa kitu kidogo. Watu hawa hawana tofauti na machief waliopewa zawadi kidogo na wazungu wakauza nchi zao. Ila kinachonisikitisha ni kuwa, machief wa zamani wao walikuwa hawajui wanachofanya, hawa wanamjua Ridhiwani sio Mnyakyusa lakini wamemnyima uchief Mwakyusa ambaye ni Mnyakyusa mwenzao wakampa Kikwete ambaye ni Mkwere. Ndio maana hata maliasili na utajiri wetu mpaka sasa tunatoa bure kwa wageni. Huu ni ujinga na sio uzalendo hata kidogo.

    ReplyDelete
  3. Huu ni upotoshaji wa hali ya juu, hakuna mtu anaitwa chifu wa wanyakyusa. Na pia chifu katika jamii ya Kinyakyusa ya leo is just a symbol with no significance at all.

    Jamii ya kinyakyusa ina chifu karibu kila kata. Kuna machifu zaidi ya mia ndani ya Rungwe na Kyela. Sasa ni lini hao machifu wote walikutana na kwa utaratibu upi kumtawaza Ridhwani kuwa chifu wa wanyakyusa?

    Ridhwani amuulize huyo chifu Mwailemale kama alipata ridhaa ya Waziri Mwakyusa? Maaana naye ni chifu. Jamani hizi desperation sasa zitawapeleaka kubaya..........

    Michuzi pls usiminye hii!!!!

    ReplyDelete
  4. mwailemale twambombo maana yake hajiwezi bora angepewa jina jingine

    ReplyDelete
  5. MICHUZI ANGALIA SANA POSTS ZAKO, UNAPOSEMA RIDHIWANI KATAWADHWA KUWA CHIFU WA WANYAKYUSA NINAAMINI HUFAHAMU UMEMAANISHA NINI, UNAPOSEMA WANYAKYUSA UNAMAANISHA NINI? FOR SURE MIMI NI MNYAKYUSA NINAYEFAHAMU CHIFU MAANA YAKE NINI? HIVYO HATA SIKU MOJA MJANGA(RIDHIWANI) HAWEZI KUWA CHIFU WA KINYAKYUSA USIJE UKAMSABABISHIA MATATIZO(SPIRITUALLY.

    Hii coment usiibane wewe (m)ichuzi na (r)idhiwani hamtaielewa lakini Wanyakyusa wamenipata vizuri sana

    ReplyDelete
  6. Huyu jamaa anamiela sijui kaipata wapi mimi na wewe hatujui ila Mungu mwenyewe anajua

    ReplyDelete
  7. Malafyale Mwailemile! waslimie akina Mwakajonga, na Mwankenja Tuntufye!

    ReplyDelete
  8. Mwe, akalumyana aka kokanyafyale ka Banyakyusa, Mwakalinga upilike isyo?

    ReplyDelete
  9. NJANGA HAWEZI KUWA MALAFYALE WA WANYAKYUSA, HAO NI WAPAMBE WA CCM, NA MKITAKA HIVYO WATAKUJA NA WA CHADEMA PAMOJA NA TIELOPIIIIIIIIIIIII MTAWAPA HUO UCHIFU. MLEKE IMBOSYA ISYO.

    ReplyDelete
  10. Hivi Kaka,

    Hivi haya mambo watu wamenyamaza kimya mnafikiri hawayaoni au?

    Hivi kwa nini mtu mzima unasubiri mpaka uambiwe badala ya kurizon wewe mwenyewe tu?

    Haya tuendelee kuangalia.
    Matokeo yake tutayaona.

    ReplyDelete
  11. Naomba kuuliza kama sherehe hizi zilihudhuriwa na Mbunge wa sasa wa Kyela Mheshimiwa Dr Harrison Mwakyembe?

    Jingine zamani nilikuwa nafikiri Walugulu ndiyo ambao wanaweza kufanya mambo yasiyomkinika katika siasa kumbe na Wanyakyusa nao! Maana tumeyaona yaliyotokea kwenye kura za maoni Rungwe Magharibi na sasa tunayaona ya Chifu Mwailemale!

    ReplyDelete
  12. Hello, I remember Baba Lizi to have been crowned the Chief of Wanyakyusa and now the mtoto has been crowned too to be the chief of Wanyakyusa. Is the 'tenure in the office' of Baba Lizi as the Chief of Wanyakyusa gone? Nisaidie.

    ReplyDelete
  13. Umaskini kazi kweli kweli!

    ReplyDelete
  14. Wanahistoria wa Tanganyika naomba msaada hapa. Nimeshuhudia na kusoma kwenye vyombo vya habari kuhusu watu maarufu wakiwemo wanasiasa KUSIMIKWA UCHIFU WA MAKABILA FULANI. Je, uchifu hasa unapatikanaje?

    ReplyDelete
  15. Ankal,

    Usikose kurusha swali langu kama Mbunge wa Kyela Mheshimiwa Dr Harrison Mwakyembe alikuwepo katika sherehe za kusimikwa na kutawazwa uchifu wa Chifu Mwailemale?

    Pia kuhusu Mbeya kuanza kugeuka kuwa kama Morogoro katika medani ya siasa maanake tumeanza kuona katika kura za maoni za Rungwe Magharibi na sasa tunaona ya Uchifu Kyela.

    yale matatizo matatu ya ujinga, maradhi na umasikini yalioainishwa na Azimio la Arusha ni lazima yapangiwe mkakati madhubuti wa kuyaondoa, kuyatibu na kuyakinga. haya mambo ni kati aya athari za hao maadui watatu. Inawezekana yanaanza, au yashaanza kuwa hatari au yashakuwa hatari!

    ReplyDelete
  16. duniani kuna mambo!

    ReplyDelete
  17. Naungana na wadau wengine hapo juu. Huwezi kutawaza kabwana mdogo kuwa Chief. Unless awe amerithi. Mkwere na wanyakyusa wapi na wapi

    WAKOME

    ReplyDelete
  18. Imbombo ngafu??!!! lubunju ngafu?!

    uchifu wa kinyakyusa ni wa kujizolea tu

    ReplyDelete
  19. Sasa huyo ni chief Mwailemile II au? Halafu mbona huyo Mwailemile mwenyewe kavaa kofia kama Mrema? Ni CCM kweli huyo au?

    ReplyDelete
  20. Inabidi munisubiri Baba anipe uridhi!

    ReplyDelete
  21. Etaaaaaatah!!!!!


    Mweumweumweumwemweeeee!

    ReplyDelete
  22. haya ni mambo ya aibu tupu. Mimi ni mnyakyusa, unyakyusani kuna machifu wengi sana, lakini siyo wa kusimikwa.uchifu huwa ni wa kurithi. Baba yangu alirithi uchifu kutoka kwa baba yake

    Kama hao wachache wa Kata ya Ipinda, Kyela wameamua kumpa huyo kijana uchifu, inabidi wawe specific waseme ni chifu wa kwao wao, siyo chifu wa wanyakyusa. Kwa mfano waziri mwakyusa ni chifu wa kwao, lakini si chifu wa wanyakyusa wote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...